Kimei amlilia Prof. Shao, asaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole kwa familia

Kimei amlilia Prof. Shao, asaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole kwa familia

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
65
Reaction score
81
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei leo ametia saini Kitabu cha maombolezo ya Kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Msamaria Mwema (GSF) na Hospitali ya KCMC Profesa John F. Shao katika viwanja vya hospitali ya KCMC.

Akiwa katika viwanja vya KCMC baada ya kusaini kitabu cha maombolezo Dkt Kimei amesema kuwa kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Vunjo na familia yake amefika hapo kutoa pole na Salamu za rambirambi kwa familia, jumuiya ya GSF, KCMC, chuo kikuu cha Tumaini Makumira, uongozi wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), UDSM na wote walioguswa na kifo cha Prof Shao aliyefariki tarehe 06 Oktoba mwaka huu.

Amesema kuwa Prof Shao alikua moja ya wanasayansi mahiri, mwanataaluma na mbobezi katika uongozi wa sekta ya afya Nchini aliyekuwa mwenye bidii ya kazi, mnyenyekevu na mzalendo hivyo atakumbukwa kwa matunda na alama alizoziacha ikiwemo kuasisi chuo kikuu cha Tiba KCMC.

Soma Pia: Profesa Shao Mkurugenzi mstaafu hospitali ya KCMC azikwa, madaktari wamlilia

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe. Apumzike kwa Amani.

IMG_20241008_161106_134.jpg
IMG_20241008_161019_769.jpg
IMG_20241008_161046_044.jpg
 
Back
Top Bottom