Pre GE2025 Kimei amtaja Samia kinara wa mageuzi ya elimu nchini ikiwemo maarifa ujuzi, asema Vunjo yanufaika

Pre GE2025 Kimei amtaja Samia kinara wa mageuzi ya elimu nchini ikiwemo maarifa ujuzi, asema Vunjo yanufaika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
65
Reaction score
81
Jimbo la Vunjo ni kati ya majimbo 100 nchini ambayo yamenufaika na mradi wa ujenzi wa shule mpya za sekondari Mafunzo ya Amali Uhandisi, ili kuwawezesha Vijana kupata ujuzi na kuwa mahiri. Kwa Jimbo la Vunjo shule hii inaendelea na ujenzi katika kijiji cha Koresa kata ya Kirua Vunjo Kusini kwa gharama ya shilingi milioni 584.

Wanafunzi watakaomaliza Sekondari mafunzo ya Amali watapata cheti cha Kidato cha Nne na cheti cha VETA, na wanaweza kwenda kufanya kazi za ufundi sehemu yoyote.

Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kusimamia mageuzi ya Elimu, ikiwemo kuweka msukumo wa mafunzo ya amali yanayojikita kwenye maarifa ujuzi.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mbunge wa Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ameendelea kuwa sauti na mtetezi wa kweli juu ya mahitaji ya wananchi waliompa imani kuwa mwakilishi wao, wajibu anaoutekeleza kwa uaminifu ambapo wingi wa miradi ya maendeleo katika jimbo lake ni kielelezo cha dhahiri.

Mbunge Kimei anamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa mageuzi ya elimu nchini hususani maarifa ujuzi pamoja na kuwekeza fedha nyingi katika sekta hii ya elimu. Dkt Kimei amesisitiza kuwa kwa kazi kubwa ya maendeleo iliyofanyika Jimbo la Vunjo kwa kila sekta hakuna wasiwasi juu ya ushindi wa kishindo kwa CCM na Rais Samia kwenye jimbo hilo.

IMG-20250218-WA0076.jpg
IMG-20250218-WA0078.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250218-WA0077.jpg
    IMG-20250218-WA0077.jpg
    79.6 KB · Views: 3
  • IMG-20250218-WA0072.jpg
    IMG-20250218-WA0072.jpg
    67.7 KB · Views: 2
  • IMG-20250218-WA0073.jpg
    IMG-20250218-WA0073.jpg
    72.6 KB · Views: 3
  • IMG-20250218-WA0074.jpg
    IMG-20250218-WA0074.jpg
    78 KB · Views: 3
  • IMG-20250218-WA0075.jpg
    IMG-20250218-WA0075.jpg
    78.6 KB · Views: 1
Ndio Tanzania ilipofikia Hapa sasa, usipopongeza unafukuzwa uanachama
 
Back
Top Bottom