Kimei ni mzigo kabisa.
Hakuweza kuwasaidia chochote watu wa Vunjo kiuchumi kama alivyohaidi au kutegemewa na hakuweza kulisaidia taifa kiuchumi.
Kuwakumbusha tu watu, kimei alitoa ahadi kubwa tatu za kiuchumi ķwa watu wa Vunjo ambazo zote hakuweza hata kujaribu kuanza kuzitekeleza.
1. Kuwezesha kujengwa kwa masoko makubwa matatu ya mazao ya kibiashara (Soko la Himo/Njia panda, Marangu/Mwika, Kirua/Vunjo). Kumbuka jimbo la vunjo ndio mlango mkuu wa kuuza mazao kwenda Kenya (kupitia mpaka wa Holili) na kuleta Dar.
2. Kufungua na kukuza mifumo imara ya kifedha (kibenki) kila kata na kijiji kwa ajili ya kuweka na kukopa(Saccos). Watu walitegemea kuibuka na kuimarishwa kwa Saccos. Hili halikuhitaji hata senti tano bali utashi na utaalamu wake wa kiuchumi na uzoefu aliotoka nao huko CRDB. Mwamba hapa alipata 0%.
3. Kulifungua kibiashara eneo la njia panda kuwa kitovu kikuu cha kiuchumi kwa mkoa wa Kilimanjaro. Hilo ndio eneo potential zaidi kiuchumi kwa Kilimanjaro kuliko maeneo ya Boma Ng'ombe na Moshi mjini, lakini ndio limedorora zaidi kuliko hapo awali huku mengine yakichanua. Kwa sasa hata stendi ya njia panda imekufa kabisaa.