Kimenuka Diamond

Kimenuka Diamond

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Anadaiwa kufuatiliwa kwa ukaribu na polisi akihofiwa kusafirisha 'unga' kutokana na shoo za nje ya nchi, kumiliki fedha nyingi katika akaunti.

==========

attachment.php

NIkweli kimenuka! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz' yupo kikaangoni, habari zinadai kwamba kila anaponyanyua miguu, kikosi cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini chini ya kamishna wake, Godfrey Nzowa nao wananyanyua miguu yao kumfuatilia, Amani limesheheni.

Habari za kiintelijensia zilidai kwamba, kisa cha kikosi hicho kufanya hivyo kinadaiwa kuwa, serikali inamhofia kujihusisha na biashara hiyo haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga' nje ya nchi kwa kutumia kivuli cha kwenda kufanya shoo.

Akizungumza na wanahabari wetu jijini Dar, Jumatatu iliyopita, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kitengo hicho ambaye hakupenda kuchorwa jina gazetini, alisema Diamond amepewa maelekezo yote muhimu.

MAELEKEZO ALIYOPEWA
"Tumempa maelekezo Diamond, atuletee mikataba ya shoo zote anazokwenda kuzifanya nje ya nchi ili tujiridhishe kama kweli ni halali au anakwenda kwa ajili ya biashara nyingine.

"Hiyo yote inatokana na uchunguzi wetu kwake kuhusu akaunti zake za benki kuonesha kwamba ana fedha nyingi sana zinazotia shaka kama amezipata kihalali," alisema afisa huyo.

KUNUNUA NYUMBA
Afisa huyo aliendelea kusema kwamba, uchunguzi wao pia umebaini kwamba, msanii huyo wa Bongo amekuwa akinunua nyumba kila anaporejea kutoka kwenye shoo zake nje ya nchi, jambo ambalo taasisi haiamini kama kweli analipwa pesa nyingi kwa shoo moja, kiasi cha kumwezesha kununua nyumba jijini Dar.

"Tumebaini kwamba Diamond kila akirudi nchini kutoka kwenye shoo zake hununua nyumba. Analipwa kiasi gani cha fedha kule kwenye shoo? Hapa ndipo tunaposimamia sisi," alisema afisa huyo huku akigongea msumari kuwa Diamond mwenyewe amekatazwa kuzungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu kutakiwa kuwasilisha mikataba ya shoo zake za nje.

KUNA UKWELI?
Amani lilifuatilia na kubaini kwamba, Diamond aliporejea kutoka kwenye safari yake ya Marekani hivi karibuni, alinunua nyumba kwa Sh. milioni 80 iliyopo maeneo ya Mwananyamala-Magengeni, Dar.

Siku za nyuma, msanii huyo aliwahi kuripotiwa kununua nyumba zaidi ya mbili maeneo ya Kijitonyama, Dar, kiasi cha kuandikwa na vyombo vya habari kwamba amenunua mtaa.

KUHUSU AKAUNTI YA BENKI
Diamond mwenyewe aliwahi kuhojiwa katika Kipindi cha Take-One kinachorushwa hewani na CloudsTV ambapo alipoulizwa akaunti yake inasomaje, alijibu kuwa ina zaidi ya bilioni moja hivi.

DONDOO ZA UWEZO WA DIAMOND
1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.
2. Yupo kwenye mazungumzo na promota wa Rwanda kufanya shoo moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 (zaidi ya Sh. milioni 190).

3. Malipo ambayo hupokea kwa shoo zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000 (zaidi ya Sh. milioni 40).
4. Tangu mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya Sh. milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa jijini Dar ambazo amepangisha watu.
6. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake, Papa Misifa ilibidi amlipe Sh. milioni 18.

NZOWA AZUNGUMZA NA AMANI
Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Nzowa ambapo alipopatikana na kuulizwa, alisema:

"Ni kweli! Sisi kila mtu mwenye kipato cha kutia shaka lazima tumchunguze. Diamond kama ana mali zote kwa nini tusimchunguze. Ikithibitika anajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ama zake ama zetu huo ndiyo utaratibu wetu."

DIAMOND SASA
Amani lilimsaka Diamond na kumuuliza kama analijua kasheshe hilo ambapo alisema:
"Najua, ila nimegundua kuna watu wamepanga kunishusha chini kisanii ndiyo wanaoeneza taarifa kwamba mimi nasafirisha unga."

Amani: Sasa unadhani kwa nini hao watu unaosema wamependa kukushusha kisanii wasitumie njia nyingine, hasa ya sanaa wakatumia hiyo ambayo unasema si kweli?
Diamond: We elewe hivyo kaka (akakata simu).

SAFARI ZA NJE
Kwa kipindi kirefu sasa Diamond ambaye ni mpenzi wa Wema Isaac Sepetu, amekuwa akisafiri nchi mbalimbali kwa shoo na mambo binafsi ambapo mbali na nchi kibao za Bara la Afrika, ameshasafiri nchi nyingi zikiwemo Marekani, Uingereza, China, Norway, Ujerumani, Dubai na nyinginezo.

Chanzo:
GPL
 
... anadaiwa kufuatiliwa kwa ukaribu na polisi akihofiwa kusafirisha 'unga' kutokana na shoo za nje ya nchi, kumiliki fedha nyingi katika akaunti!

Inaonekana unasoma vichwa vya habari vya kurasa za kwanza many magazeti na kwenda kusimulia habari iliyomo ndani ila kujua nini kimeandikwa... A cha umbea Dogo
 
Bongo bwana hakuna jema' ukiwa huna kazi watasema mzembe, mvivu; ukijituma na mafanikio yakianza kuonekana utaskia mara hoo freemason, mara kaenda kwa waganga na saiz wameanza kumsakama kijana eti anasafirisha unga. Sasa sijui ni unga gani wanaongelea hapa? Anyway inawezekana ikawa dona, sembe au unga wa ngano. Kama vile wanefumba macho hawaoni jitihada za huyu kijana kimziki.

Inavyoonekana mnapenda kuona vijana wanahangaika mtaani au wawe mateja ili muendelee kuifirisi hii ardhi sio bure. Maana hata wewe mleta uzi umekuja kiushabiki na hili swala' kwamba umefurahaia na ndio maana umekimbia kuleta uzi kiumbeambea bila hata kueleza vizuri kilichojiri.

Kila lakheri Diamonds achana na hizi fitna' fanya yako. Kwenye mafanikio majungu, fitna na wivu havikosekani. Fanya kulingana na mapenzi ya Mungu.
 
Attachments

  • diamond.jpg
    diamond.jpg
    76.9 KB · Views: 2,104
hivi diamond "ANA PESA NYINGI KWENYE ACCOUNT YAKE ENHEEE? "...MIE NILIKUWA SIJUI...KWANI ANA TSH NGAPI AU USD AU EURO NGAPI VILE?.....ANAMZIDI MZEE BAKHRESA?..AU MZEE MENGI AU METL?......HIVIANAFANYA SHUGHULI GANI KIASI CHA POLISI KUACHA KAZI ZAO WAMFUATILIE YEYE.....

KWANI UNAMUONGELEA DIAMOND YUPI...YULE ALIYEIMBA WIMBO WA "TATIZO KWETU MBAGALAAAAAA....MBELE NYUMBA NYUMA JALALAAAAAAAAA"....SIO YULE ALIYEIMBA KITORONDO...ANATEMBEA NA WEMA SEPETU?

KAMA NI HUYO BASI POLISI WETU HAWANA KAZI...MAANA SIAMINI KAMA ATAKUWA HATA NA TSHS 200M KWENYE ACCOUNT YAKE.....PESA UJUWE SIO MAKALIO KILA MTU ANAZALIWA NAYO...INATAFUTWA ILE TENA KWA AKILI KWELIKWELI......

MUSICHANGANYE UMAARUFU NA PESA....INGEKUWA PESA NA UMAARUFU VINA UHUSIANO KAMA MUNAVYODHANIA...BILL GATES ANGEKUWA MAARUFU KULIKO MICHAEL JACKSON NA KINA TUPAC....AU MZEE BAKHRESA ANGEKUWA MAARUFU KULIKO MZEE MAJUTO NA STEVE KANUMBA.

TUWE SERIOUS BANA....ARGHHHHHH...SORRY KUMBE HILI NI JUKWAA LA HABARI MCHANGANYIKO..FULL MIXED UONGO UKWELI MAJUNGU UZANDIKI FITNA NA KILA AINA YA TRASH HUTUPWA HUKU....SORRY GUYS FOR BEING SERIOUS ON STUPID ISSUE.

at least for now i do care......
 
Wivu tu unawasumbua nyie viongozi wa serikali mbovu ya buku 7,hamtaki kutuona vijana tunafanikiwa kimaisha,eti unga,washe.nzi wakubwa nyie,yaone kwanza hayooooooo! mnafikiria kujenga magereza badala ya viwanda,nyambaf zenu wote...
 
hivi diamond "ANA PESA NYINGI KWENYE ACCOUNT YAKE ENHEEE? "...MIE NILIKUWA SIJUI...KWANI ANA TSH NGAPI AU USD AU EURO NGAPI VILE?.....ANAMZIDI MZEE BAKHRESA?..AU MZEE MENGI AU METL?......HIVIANAFANYA SHUGHULI GANI KIASI CHA POLISI KUACHA KAZI ZAO WAMFUATILIE YEYE.....

KWANI UNAMUONGELEA DIAMOND YUPI...YULE ALIYEIMBA WIMBO WA "TATIZO KWETU MBAGALAAAAAA....MBELE NYUMBA NYUMA JALALAAAAAAAAA"....SIO YULE ALIYEIMBA KITORONDO...ANATEMBEA NA WEMA SEPETU?

KAMA NI HUYO BASI POLISI WETU HAWANA KAZI...MAANA SIAMINI KAMA ATAKUWA HATA NA TSHS 200M KWENYE ACCOUNT YAKE.....PESA UJUWE SIO MAKALIO KILA MTU ANAZALIWA NAYO...INATAFUTWA ILE TENA KWA AKILI KWELIKWELI......

MUSICHANGANYE UMAARUFU NA PESA....INGEKUWA PESA NA UMAARUFU VINA UHUSIANO KAMA MUNAVYODHANIA...BILL GATES ANGEKUWA MAARUFU KULIKO MICHAEL JACKSON NA KINA TUPAC....AU MZEE BAKHRESA ANGEKUWA MAARUFU KULIKO MZEE MAJUTO NA STEVE KANUMBA.

TUWE SERIOUS BANA....ARGHHHHHH...SORRY KUMBE HILI NI JUKWAA LA HABARI MCHANGANYIKO..FULL MIXED UONGO UKWELI MAJUNGU UZANDIKI FITNA NA KILA AINA YA TRASH HUTUPWA HUKU....SORRY GUYS FOR BEING SERIOUS ON STUPID ISSUE.

at least for now i do care......

kibongobongo dogo yupo vizuri
 
mbona bakhresa anatengeneza unga hawamsemi ......... anatengeneza unga wa azam poa, azam chapati n.k

Grand PA
 
mbona bakhresa anatengeneza unga hawamsemi ......... anatengeneza unga wa azam poa, azam chapati n.k

Grand PA
huyu anatengeneza..but NDOMO wana m suspect anatransport...!?
Nzowa nae hana cha kufanya au nae katumwa na magamba!
 
kibongobongo dogo yupo vizuri

yupo vizuri wapi..

dogo anatambaa na media kujipa promo...unajuwa pesa ina styles zake za kuonge...MATENDO MAKUU YA PESA NI MATUMIZI NA INVESTMENTS...dogo kafanya nini?...

tuache ushabiki mandazi na magazeti pendwa...aseme kapiga mishe ipi kafunga mtonyo upi au ka-invest wapi?...mbona kina jigga kina p-diddy MONEY TALKS FOOLS WALKS ....mie sikubali bado.

misifa kibaoo mara ohhh dangote mara ohhhh.....aache peche mingi...wewe mtu kashindwa hata kumpa shorty wake mchongo wa maana anakaa kuzunguka naye kukata uno madisco vumbi bana.....ANGALIA P-SQUARE WAO WANAMILIKI PRIVATE JET. huyu wetu anamiliki nini?

MWAMBIENI AACHE KUCHEZA NA MEDIA..APIGE PESA AFANYE MAMBO YANYOFANANA NA PESA.

at least i do care for now.
 
Kusoma magazeti ya Shigongo niwkukosa kayi ya kufanya na kujisajili kwenye kundi la wajinga.
 
yupo vizuri wapi..

dogo anatambaa na media kujipa promo...unajuwa pesa ina styles zake za kuonge...MATENDO MAKUU YA PESA NI MATUMIZI NA INVESTMENTS...dogo kafanya nini?...

tuache ushabiki mandazi na magazeti pendwa...aseme kapiga mishe ipi kafunga mtonyo upi au ka-invest wapi?...mbona kina jigga kina p-diddy MONEY TALKS FOOLS WALKS ....mie sikubali bado.

misifa kibaoo mara ohhh dangote mara ohhhh.....aache peche mingi...wewe mtu kashindwa hata kumpa shorty wake mchongo wa maana anakaa kuzunguka naye kukata uno madisco vumbi bana.....ANGALIA P-SQUARE WAO WANAMILIKI PRIVATE JET. huyu wetu anamiliki nini?

MWAMBIENI AACHE KUCHEZA NA MEDIA..APIGE PESA AFANYE MAMBO YANYOFANANA NA PESA.

at least i do care for now.

Mkuu umemaliza kma angekua na uwezo tungeona investment zke c kujenga nyumba miaka 4 kma daraja la kigamboni,mtu unakaa nyumba y kupanga y laki 4 sinza na ukoo mzima then unasema una 1bn.

Wajinga wenzake ndio watamsifia pesa ni kma mafua au kikohozi huwezi kukificha lazma utaumbuka.halafu mtu ukisema ukweli unaambiwa unamchukia pumbaf....u zao
 
Nyumba ya million 80 mwananyamala si gofu tu jamani, maana mwananyamala kiwanja tu cha robo heka ni pesa ndefu.
 
yupo vizuri wapi..

dogo anatambaa na media kujipa promo...unajuwa pesa ina styles zake za kuonge...MATENDO MAKUU YA PESA NI MATUMIZI NA INVESTMENTS...dogo kafanya nini?...

tuache ushabiki mandazi na magazeti pendwa...aseme kapiga mishe ipi kafunga mtonyo upi au ka-invest wapi?...mbona kina jigga kina p-diddy MONEY TALKS FOOLS WALKS ....mie sikubali bado.

misifa kibaoo mara ohhh dangote mara ohhhh.....aache peche mingi...wewe mtu kashindwa hata kumpa shorty wake mchongo wa maana anakaa kuzunguka naye kukata uno madisco vumbi bana.....ANGALIA P-SQUARE WAO WANAMILIKI PRIVATE JET. huyu wetu anamiliki nini?

MWAMBIENI AACHE KUCHEZA NA MEDIA..APIGE PESA AFANYE MAMBO YANYOFANANA NA PESA.

at least i do care for now.
Anamiliki kijiji kijitonyama nyumba za uswazi mim mwenyewe mpangaji wake kodi 30,000 kwa mwezi, kodi iko juu sana.
 
Hawa Police wa Bongo jamani,wana wacha Mapapa wanavua Vidagaaaa,wamuache na agange njaa mweneywe chuki na roho mbaya tuu,kuna wanao nunua majumba masaki hao hawaulizwi yeye wa Mwananyamala imekua mwao.....
 
Back
Top Bottom