Kimenuka mbaya: Shehe amtolea uvivu Jaqueline Wolper Gambe

majidid kahtaan toa ufafanuzi, naamin hutotukana sababu ya Ramadhan
 
Last edited by a moderator:
Jacqueline Wolper kubadilibadili dini mara kwa mara imeonekana kuwakera watu mbalimbali akiwemo Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum ambaye amemcharukia vikali.
mkuu ningeomba uweke bayana Jack Wolper alikuwa anaswali msikiti gani hasa... kabla haja-apostacy,..Isije ikawa changa la macho alikuwa anaigiza filamu ya mapenzi na dulla?Na je sheria inamchukuliaje Dulla kuwa na mahusiano(intimacy) na binti wa kikristo .

"Siyo vizuri hata kidogo na hata dini zote zinakemea kitendo cha kuchezeachezea dini kwani ni chukizo kwa Mungu
Nadhani hapa penye red: unge-omit tu ili sentensi ieleweke vyema isilete sintofahamu nyinginezo.

"Kwa upande wa Dini ya Kiislamu, kuna sheria kali zaidi kwa mtu akionekana na tabia hiyo, anaweza hata
kuuawa hivyo wanaofanya mchezo huo waache kwani siyo vizuri. Huko ni kumfanyia Mungu dhihaka," alisema Shehe Salum na kuongeza:
penye red: nadhani..unge-delete pia tu ili sentensi ieleweke vyema (call a spade a spade ..not a big spoon).
Asante kwa uzi.
pia ungetuelewesha kuna wale wakristo wenye tabia ya kuvaa kanzu,misuli na vibarakashia kama waislamu, JE sharia inasemaje ,je wao wanachezea imani za watu ama hakuna tatizo.. nauliza tu mkuu.


 
Hapa ndipo nnapowakubali shemeji zangu wachaga kwa kuabudu pesa..
 
Dini ni suala la Mtu binafsi....ni la hiari
 

Bora niwe kafiri kuliko kuabudu mungu ambae kaumba dunia yenye matatizo, magonjwa, na ushetani. Dunia ya mungu ina upungufu mkubwa maana ina ruhusu ukatili, ukoloni, utumwa na ubakaji wa watoto wadogo kufanyika! Binadamu wasinge weza kufanya uovu kama mungu angeweka mazingira bora duniani toka mwazo. Si wanasema mungu ndiye mjua yote na mwenye uwezo wote?

Mimi ningekuwa mungu nisinge ruhusu ubaya wowote utokee kwenye dunia yangu. Hata fikra zote mbaya nisinge ruhusu watu wawe nazo akilini - ningeumba ubongo perfect. Alafu kwakuwa mimi ni mungu na ninajiamini, nisingetaka kusujudiwa,kutukuzwa, au kuwatia majaribuni watu wangu. Ningetenda mema tuu na kusheherekea umbaaji wangu tukufu.

Engineer/mhandisi akitengeneza ndege ya abiria nilazima aitest kwanza kabla haija beba abiria. Sio kuiacha kuruka alafu kuilaumu Engine ya ndege kama chombo hicho kikianguka toka angani!!!

Kwahiyo mkuu, kama mimi ni kafiri, basi iliyeniumba kachakachua.......kwasababu kaumba binadamu mpungufu.....
 

Ramadhan kareem majidid kahtaan, pilgrim in faith
 
Last edited by a moderator:
Ndugu daima unapoandika Mungu anza na herufi kubwa!
 
Ndugu daima unapoandika Mungu anza na herufi kubwa!

Huyu kachupa mipaka. Angalia comment yake karudia herufi ndogo, katoa lawama, mara kamfananisha Mungu na Engineer ili mradi anazidi kupotoka tu. Nitaquote alichoandika hapa chini!:-
 

Kweli mtu na akili zake anaweza kuandika maneno haya ya mtoto wa Pharao? Huyu ana matatizo si bure. Kuna watu wanakufuru lakini huyu kapitiliza
 
sidhani kama watu watakuelewa, binafsi nimekuelewa sana. Asante kwa kutazama mada kwa jicho la tatu!

Asante sama ndugu kwa kutambua hilo.
Nimuhimu sana kuelimisha jamii pale fursa inapojitokeza.
Ni ngumu lakini tujitahidi...
 
Sioni mahali unapoonyesha kuwa Alhaji Salum amemtaja Wolper, sanasana naona umehitimisha kwa maoni ya mkazi wa Ilala.

Nadhani Sheikh atakuwa amekemea kwa ujumla tabia ya kuhama dini moja kwenda nyingine, na kwa maoni yangu sioni kosa lolote kwa mtu kutumia uhuru wake wa kuabudu...mwisho wa siku hizi zote ni imani, na ndio maana kuna imani za kihindu, kibudha n.k na wote hao wanaamini kuwa wao ndio wako sahihi kuliko mwingine.

Mfano rahisi tu, chukua watoto watatu wa dini/imani tofauti (hata mlozi) wanaofanya vizuri kwenye masomo....kila mmoja kati yao atakwambia na kusisitiza kuwa imani yake (ulozi au tambiko) ndio siri ya yeye kufanya vizuri kwenye masomo.....tafsiri yake ni nini ? ni kuwa, hakuna haja ya kudhania kuwa yupo mwenye haki ya kumuwakilisha Mungu duniani kuliko wengine.

Hivyo wale wanaodhani kwamba adhabu kwa mtu kuhama imani moja kwenda nyingine ni kumtoa uhai, wajiulize mara mbili.....Mungu hayupo kama wengi mnavyojitahidi kumdhania...na kama ni adhabu nadhani hilo ni jukumu lake.
 

lakini majuzi tu, tumejionea Human right watch ikitangua Sharia kule Sudani - mwanamke akiachiwa huru kwa kosa la kuolewa na mkristo.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…