Kimenuka mbaya: Shehe amtolea uvivu Jaqueline Wolper Gambe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
TABIA ya staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper kubadilibadili dini mara kwa mara imeonekana kuwakera watu mbalimbali akiwemo Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum ambaye amemcharukia vikali.

Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper akipozi.
Wolper kiimani ni Mkristo lakini hivi karibuni alibadili na kuwa Muislam kabla ya kurejea tena kwenye imani yake ya awali ya ukristo.
Sababu ya Wolper kubadili dini ilikuwa ni kufunga ndoa na aliyekuwa mchumba wake Abdallah Mtoro ‘Dalas', walipoachana akaamua kurudi kwenye ukristo.
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzikati, Shehe Salum, alisema Wolper anapaswa kujichunguza na kubadilika haraka kwani kitendo anachofanya ni kinyume na taratibu za dini.
"Siyo vizuri hata kidogo na hata dini zote zinakemea kitendo cha kuchezeachezea dini kwani ni chukizo kwa Mungu.

Jacqueline Wolper akiwa kazini.
"Kwa upande wa Dini ya Kiislamu, kuna sheria kali zaidi kwa mtu akionekana na tabia hiyo, anaweza hata kuuawa hivyo wanaofanya mchezo huo waache kwani siyo vizuri. Huko ni kumfanyia Mungu dhihaka," alisema Shehe Salum na kuongeza:

"Unajua suala la imani ni kitu kinachomhusu mtu binafsi, ni vyema kufanya uamuzi wa hakika na kushika njia moja na siyo kufanya dhihaka na dini ya Mwenyezi Mungu. Ni kitu kibaya sana."

Naye Juma Suleiman, mkazi wa Ilala, jijini Dar es Salaam alimwambia mwandishi wetu kuwa, katika imani ya kiislam kunakatazwa watu kucheza na dini huku akisisitiza anayefanya hivyo anaweza kulaaniwa.

"Dini siyo kitu cha kuchezea, ni daraja la kumfikisha mtu kwenye haki, si mahala pa kuingia na kutoka, kuingia na kutoka. Huko ni kucheza na Mungu. Namshauri huyo mtoto (akimaanisha Wolper) abadilike. Asifanye mchezo na imani, Mungu anaweza kumlaani kwa kumchezea," alisema Suleiman.chanzo.http://jocyberspace.blogspot.com.tr/2014/06/kimenuka-mbaya-shehe-amtolea-uvivu.html
 
Hapa tatizo sio huyu dada bali ni mungu mwenyewe.

Kama mungu anaju yote na hata yale ambayo hayajatokea, basi lazima alijua kuwa huyu binti ata rudi ukristo baadae.
Sasa kwanini aliruhusu hiyo ndoa itokee na huyu dada ahamehame dini?

Pia ni lazima mungu karuhusu huyu dada kurudi ukristo maana kama isinge kuwa hivyo, basi kurudi kwake ukristoni kungezuiliwa na mungu mwenyewe. Mungu si wa dini zote, au hataki ukristo tena? Inaonekana mungu wenu hajapinga ili swala; ni binadamu tuu mnatafusiri mambo kivyenu....
 
Ni sahihi, dini ni mtu mwenyewe na si kubadili kwa ajili ya kufuata maslahi kama ya mapenzi, lilikuwa ni gamba tu na sasa kalivua.
 
Hapa tatizo sio huyu dada bali ni mungu mwenyewe.

Kama mungu anaju yote na hata yale ambayo hayajatokea, basi lazima alijua kuwa huyu binti ata rudi ukristo baadae.
Sasa kwanini aliruhusu hiyo ndoa itokee na huyu dada ahamehame dini?

Pia ni lazima mungu karuhusu huyu dada kurudi ukristo maana kama isinge kuwa hivyo, basi kurudi kwake ukristoni kungezuiliwa na mungu mwenyewe. Mungu si wa dini zote, au hataki ukristo tena? Inaonekana mungu wenu hajapinga ili swala; ni binadamu tuu mnatafusiri mambo kivyenu....

Ni kama unaandika usichokijua. Mungu hawezi kuwa tatizo. Binadamu una free will ya kuchagua.
 
Hapa tatizo sio huyu dada bali ni mungu mwenyewe.

Kama mungu anaju yote na hata yale ambayo hayajatokea, basi lazima alijua kuwa huyu binti ata rudi ukristo baadae.
Sasa kwanini aliruhusu hiyo ndoa itokee na huyu dada ahamehame dini?

Pia ni lazima mungu karuhusu huyu dada kurudi ukristo maana kama isinge kuwa hivyo, basi kurudi kwake ukristoni kungezuiliwa na mungu mwenyewe. Mungu si wa dini zote, au hataki ukristo tena? Inaonekana mungu wenu hajapinga ili swala; ni binadamu tuu mnatafusiri mambo kivyenu....

Una laana kali wewe. Eti tatizo ni Mungu!!!!. Enzi za Mungu kutoa adhab za papo kwa papo zilipita zama wakina Nuhu, wakati huu Mungu katupa Relief, instant punishment alipunguza kwa watu wake. Hata wewe huu utumbo ulioandika ingekuwa zaman ungeshakula punishment kali ila hilo wewe huoni, unavuta pumz hujalipia bado unaongea lugha za kufuru, kwa kufuru hii, ni halali kuitwa KAFIRI- Mtu aliyekufuru!
 
CHAZA umesema ukweli sitii neno hapo.
 
Last edited by a moderator:
Hapa tatizo sio huyu dada bali ni mungu mwenyewe.

Kama mungu anaju yote na hata yale ambayo hayajatokea, basi lazima alijua kuwa huyu binti ata rudi ukristo baadae.
Sasa kwanini aliruhusu hiyo ndoa itokee na huyu dada ahamehame dini?

Pia ni lazima mungu karuhusu huyu dada kurudi ukristo maana kama isinge kuwa hivyo, basi kurudi kwake ukristoni kungezuiliwa na mungu mwenyewe. Mungu si wa dini zote, au hataki ukristo tena? Inaonekana mungu wenu hajapinga ili swala; ni binadamu tuu mnatafusiri mambo kivyenu....

Una laana ww

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Hakika Mwenyezimungu amemjaalia binadamu njia mbili, ima ashukuru neema za Mungu na amuabudu yeye au akufuru.

Yeye kaamua kuchagua kukufuru, huyo Sheikh amuache, Kwanza Waislamu tuna mambo kibao yao ya kuzungumzia eti ye anaenda kuzungumzia kuhusy hawa wajaa laana.

Kwa baraka ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhan...Ewe Allah wasamehe BAKWATA, yatie nuru macho yao na uziongoe nafsi zao...amiiiin
 
Sheikh hakujua kuwa yule ni msanii?anafuata maslahi tuuhana chembe ya upendo kwa mtu
 
Back
Top Bottom