Tetesi: Kimenuka! mtawala wa Emirati alishwa sumu, tetesi kaaga!

Tetesi: Kimenuka! mtawala wa Emirati alishwa sumu, tetesi kaaga!

tubalayya

Senior Member
Joined
Apr 16, 2010
Posts
117
Reaction score
203
Amepachikwa jina la utani: "Shetani wa Waarabu", kutokana na uovu wake alioueneza nchi zote za Kiarabu. Mohammed bin Zayed, anapumulia mashine, na taarifa nyingine zinasema "kisha kitoa". Ulimwengu mzima wa Kiarabu uko katika shamra shamra za kufurahia, hata kama haijathibitishwa rasmi kifo chake.

Mohammed bin Zayed, hadi sasa, ndiye anayefadhili kundi kuu la waasi Sudan, "Al Daama" linalohusika na kuuteketeza mji mkuu wa Khartoum na mauaji ya kimbari kwenye jimbo la Darfur ambapo watu Wasudani weusi milioni 2 hadi sasa wameuawa, na wengine milioni 8 kuacha makazi yao.

Kabla ya Sudan, alifadhili machafuko ya Libya yaliyopelekea kifo cha Al Qadhafi. Pia mauaji makubwa ya Algeria, na vita vya Yemeni, ambapo Emirati, hadi kufukuzwa hivi karibuni na majeshi ya Saudia, imekuwa inashikilia kwa mabavu Mkoa wa Kusini ya Yemen na Jimbo la Socotra.

Yeye pia ametoa pesa kuleta machafuko Somalia, vita vikuu vya Syria vilivyopelekea mauaji ya mamilioni na mamilioni mengine kukimbia nje....na hivi karibuni Gaza, ambapo majeshi ya Emirati yameshirikiana bega kwa bega na Israeli kuwauwa Wapalestina.

Bwana huyu huupiga vita kali Uislamu na Waislamu, kiasi mahali popote penye mzozo dhidi ya Waislamu alitia mkono wake. Ameunda dini mpya akaiita " Dini Ya Ibrahim" akaamuru dini zote ziswali kwenye Kanisa moja alilolijenga Abu Dhabi!
Hawa ndio marafiki wa Tanzania!

Wakati mwingine naona serikali yetu imetupilia mbali kabisa maadili ya kibinadamu na haki za binadamu, kiasi kwamba lau Utawala wa Makaburu ungekuwepo hivi sasa basi tungeuunga mkono na kuachana na Mandela! Yote haya tunaambiwa eti ni kwa kutuletea maendeleo!

Mwalimu Nyerere, kwa ubinadamu wake, alikataa katu uhusiano na Israel na akawatimua nchini. Lakini leo twawakumbatia waovu hawa, wanaofanya mauaji ya kutisha Palestine, na kukataa amri ya UN ya kurudisha ardhi walizozitwaa kwa nguvu 1967 na kuwafukuza wenyeji. Yote hayo eti kwa sababu ya kutuletea maendeleo....... !

Mohammed bin Zayed, inasemekana, alinyweshwa sumu na ndugu yake. Si ajabu. Tangu ilipopata uhuru na kuungana mwaka 1971, viongozi wote wa UAE waliopita waliondolewa madarakani kwa kuuawa, hata kuna aliyemwua kakaye apate kiti! Naye huyu Mohamed bin Zayed alikuja kwenye kiti kimagumbashi baada ya kumkwapua kakaye, Khalifa bin Zayed Al Nahyan, ikasemwa alizirai kwa miaka kadhaa akawa katika coma!
 
Mohammed bin Zayed, hadi sasa, ndiye anayefadhili kundi kuu la waasi Sudan, "Al Daama" linalohusika na kuuteketeza mji mkuu wa Khartoum na mauaji ya kimbari kwenye jimbo la Darfur ambapo watu Wasudani weusi milioni 2 hadi sasa wameuawa, na wengine milioni 8 kuacha makazi yao.
Uzi mzuri ila hapa umeweka propaganda!! Unataka kusema miji yenye jamii zingine hazijadhurika? Ila weusi tu?
 
Mwalimu Nyerere, kwa ubinadamu wake, alikataa katu uhusiano na Israel na akawatimua nchini. Lakini leo twawakumbatia waovu hawa, wanaofanya mauaji ya kutisha Palestine, na kukataa amri ya UN ya kurudisha ardhi walizozitwaa kwa nguvu 1967 na kuwafukuza wenyeji. Yote hayo eti kwa sababu ya kutuletea maendeleo....... !
Nyerere alikua sahihi sana sijui kwanini tulirejesha uhusiano na hao genocidaires.
 
Mohammed bin Zayed, hadi sasa, ndiye anayefadhili kundi kuu la waasi Sudan, "Al Daama" linalohusika na kuuteketeza mji mkuu wa Khartoum na mauaji ya kimbari kwenye jimbo la Darfur ambapo watu Wasudani weusi milioni 2 hadi sasa wameuawa, na wengine milioni 8 kuacha makazi yao.
RSF ndio wanaitwa Al Daama?..
 
HUYU MBWA SI AAGE TU ANASUBUR
I. NN
PENGINE ANAFADHILI NA M23
 
Hapo kwenye kuupiga vita uislam yupo sahihi inshort Kwa kuwa yeye ni mwarabu anajua undani zaidi wa hiyo dini kuliko Mimi na wewe , Anajua ukweli kwamba hiyo dini ni magumashi ni kinyanja na chanzo Cha uwepo wake ilikuwa ni kuipa power jamii ya watu wasaudi kuweza kuwa na influence ya kubwa Ya civilization kuliko jamii ya Waarabu wote , ndio maana mafundishi Yao yamejaa Udanganyifu ulio kubuhu
 
Back
Top Bottom