Kimenuka! Rais Putin atoa kitisho, asema anaweza kutumia nguvu za kijeshi kwa Marekani na NATO kutokuzingatia mistari miekundu (red lines) za Urusi

Kupigana kusikie kwa jirani. Unaweza kujawa jazba unampandishia mtu humjua, kanaonekana kalegevu unakuwa na maamuzi ya haraka eti nitakupiga, ukianza unakutana na muziki ambao hukutarajia, wapambe wameshaongezeka walioshuhudia majigambo na vitisho vyako vya awali, nguvu zinakuishia kajamaa kanaanza kukudhalilisha aibu kubwa inakupata kukimbia huwezi kusitisha uwezi....mkwara wooote limwili lòote kifua cha jim kumbe unarusha ngumi za kike!!!!😀😀😀😀 karne ya sasa hivi usipende kupigana tatua matatizo yako kidiplomasia acha jazba zisizo na maaana utaumbukaaaaa!!!!!!
 
Nani huyu mkuu?
 

Labda taarifa hii itakusaidia sana kuelewa kinachoendelea.
 
Hiyo measure ya military ataweza? Kwanza kazungukwa kabakia kulia Lia kama Iran..

Kwamba open door policy ya NATO inatishia usalama wa Rassia.

Hivi Russia hajiulizi kwa nini majirani zake hawamtaki badala yake wanataka NATO? Huu ni Wehu.
 
What happened to crimea?
 
walimpiga biti US na mashost zake VENZUELA wakawapiga biti SYRIA wakaitwaa CRIMEA na bado watamtwanga na UKRAINE labda asijiunge na NATO
 
Wanaosapoti Russian humu jf wengi mashabiki wa ali kiba na wale wa USA na NATO ni wa Diamond [emoji16][emoji16][emoji16]. Yaani wanajua kabisa Russia hawezi kitu lakini wanakomaa kisa tu hawaipendi USA
 
Putin anajua hawezi kupigana na NATO/US na akitumia nuclear itakuwa ni suicide, na wakimpiga ban kwenye World financial system ndio kwisha habari yake
 
Kwanza hana washirika,ni kama vile Nchi za Kiafrika utakuta zinasema tuko nyuma yako afu vita vikianza hakuna msaada.
Sio kweli, Russia kaichukua Crimea na wote wamebaki kumuogopa.
Us walitaka kumtoa raisi Syria, Ila alivyoingia Russia tu US wakarudi nyuma
Us alitaka pia kumtoa Maduro kule venezuela, Ila alipoingia Russia tu US wakarudi nyuma
Us ni wanawaogopa russia
 
Mrusi akitunisha misuli lazima Marekani na Nato waingie baridi. Hii barua iliyobandikwa hapo juu alipewa marekani, na marekani aliona hata aibu kusema hadharani alichoambiwa na urusi. Urusi ikaamua kuiweka yenyewe hadharani!!
Wewe umeambiwa US na NATO wala hawakuwa na muda kujibu hoja Urusi ilizoziita ni "red lines". Urusi anaona kama wamempotezea, mwenyewe anawaza hajajua akianzisha vita ni kipi atakutana nacho.
 
Watamaliza kwa njia ya kidiplomasia tu maana vita sio mchezo. Effect yake inaweza kuwa ya miaka mingi sana
 
Issue kubwa kuliko zote hapo ni jimbo la Crimea .ukraine wakiingia NATO kwa vyovyote watataka jimbo la crimea lirejeshwe mikononi mwao jambo ambalo litaingiza NATO kwenye vita ya moja kwa moja na Urusi. Ndio maana kuna vinchi vinapakana moja kwa moja urusi na vimeingia NATO (Lativia, Slovenia, lithunia, poland) lakini kelele hazikuwa kivile.. Urusi haitakubali kamwe ukraine iingie NATO iwe kwa diplomasia ama kwa vita mwamba Putin ashaiweka clear hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…