Kimetulamba kwenye written interview

Kimetulamba kwenye written interview

Ebwanaa eeh..Leo kwenye interview (DUCE) picha linaanza Hilo hall tuloingia limeshona balaah!
Yani hamna upenyo watu Kama wote almost kama 600..na hapo Kuna wengine wamezuliwa kuingia kwa kukosa vigezo..

Picha lenyewe Sasa....👇
Kwa upande WA lab technician Mtihani waliyotuletea ni WA maabara za viwandani😂 yani hamna hata swali Moja la afya.

Yani wametuletea ma volumetric analysis, ma elasticity,vernial calliper Yale ya O-level...yani .zile practical za form 4 ndo tumeletewa hamna swali Moja la afya 🥺ule Mtihani kwa mwanafunzi wa form 3&4 alokwiva vizuri anapata yote.

Halafu Mtihani ni multiple choice na dk 40 yani Kila jibu unaliona sawa 😁 Licha ya kubanana ila Ukisema upige Chabo kwa mwenzako kimekulamba unaangalizia nini uongo au maana Kila mtu amestaajabu tu anakuna kichwa

Na wasimamizi hawakuwa na muda wa ku tu supervise yani...limetushuka balaah. Baada ya kutoka nkamuuliza rafiki yangu wa pharmacy akanambia nao ndo vile vile hawwjatolewa swali Moja la afya..

My take...hayo maswali tuloletewa ingebidi waletewe walimu wa sayansi kwa hili tumeonewa au basi wangetuchanganyia ila sio kutufanyia hivi. Kama ni lengo ni kutupunguza basii limetiki haswaaa😒
jamaa wanambinu nyingi sana za kupunguza watu sisi wali tuletea maswali ya Easy 3 na moja kujieleza alafu mda dk 40 asilimia kubwa ya watahiniwa hawakuweza kufanya maswali yote wengi waliishia swali la 2na 3 aisee
 
We ni Lab sience au Health Laboratory?
Maana hayo maswali yanawafaa Lab science vinginevyo mmemixiwa mitihani kama sio walioandaa interview ni wamechanganyikiwa🤣
 
Back
Top Bottom