HIvi vyombo vya habari vinastahili kuwa na watu wa ethics! Wanatoa matangazo yaliyobuniwa kuwalaghai wananchi yaonekane ni taarifa muhimu ya kitaifa. Ni mengi, ikiwa ni pamoja na yale ya tatu mzuka, Biko,... Kwa mwananchi wa kawaida anahadaika kwamba ni tangazo la kitaifa, kumbe ni utapeli wa aina fulani.
Miaka ya zamani EAC ilikuwa na matamngazo ya dawa ya Aspro, ikisema aspro mbili kwa magonjwa ishirini. WHO ilipiga marufuku tangazo la aina hiyo kujitokeza kwenye vyombo vya habari. Hawa ni washenzi tu na vijineno vya uchumi eti economies of sclale.
Kwa mwenye uelewa kama mimi, nikisikiliza mahojiano ya mkuu wa mkoa na huyo anayejiita muwekezaji, hitimisho ni kwamba muwekezaji ameingiza utapeli, simple. Kivutio ni bei ya milioni 1 kwa kilogram ya vanilla, ambayo amesema ni uongo. What NEXT??
Angalia dakika ya 6:07 ya video hii kama bado umeshupaa shingo.