Kimewaka Kendrick Lamar VS Lil' Wayne. Unadhani nani anastahili kuperform Super Bowl 2025?

Kimewaka Kendrick Lamar VS Lil' Wayne. Unadhani nani anastahili kuperform Super Bowl 2025?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Wakati Waandaji wa Tamasha la Super Bowl Halftime wakimtangaza Kendrick Lamar kama mtumbuizaji mkuu, mjadala umeibuka Mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimtaka Rapa Lil Wayne

Katika mijadala hiyo, wapo wanaodai Kendrick ni msanii mkali sana lakini, si chaguo sahihi kufanya tamasha katika mji anaotoka Lil Wayne (New Orleans), ambaye amefanya makubwa zaidi kwenye muziki

Ikumbukwe, Mastaa wanaotumbuiza kwenye tamasha la Super Bowl Halftime hawalipwi isipokuwa hupata fursa ya kutangaza biashara zao na kuchochea mauzo ya muziki wao

Mdau wewe unadhani nani anafaa kuperform kwenye tamasha hilo na kwanini?
 
Kama ni Bure mondi na kiba wasingekubali
Ile ya Dre na snoop ilikuwa legendary
 
Japo Show ya Super Bowl ya Beyonce ya mwaka 2013 inatajwa kuwa ni Show Bora, nakubaliana nawe Mheshimiwa haitakuja itokee Show Bora ya Super Bowl kama iliyofanywa na Dr Dre ft Snoop, Eminem, Mary J, 50 Cent nk 👏👏👏👏👏
Hiyo nk si ungeandika tu Kendrick Lamar!
Maana umetaja wote kasoro yeye.
 
Back
Top Bottom