Uyole CTE
Member
- Apr 17, 2015
- 7
- 12
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa, Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 12, kilianguka ndolezi, kijiji cha isela wilayani mbozi katika mkoa wa Songwe, Tanzania.
Kipo kati ya vimondo vizito kumi (10) vinavyojulikana duniani, kimondo hiki ni cha nane (8) kwa ukubwa duniani Lakini ni cha pili (2) kwa ukubwa barani Afrika, kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22. Lakini pia Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine.vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki hasa cha chuma ambacho chaundwa na Chuma 90.45%, nikeli 8,69%, sulfuri0,01% na fosfori 0,11% ya masi.Kimondo hiki kina sifa za upekee sana mosi ni kuwa na ubaridi katika msimu wote wa mwaka hata kama jua kali likiwaka hii ni kutokana na utofauti wa madini kiliyonayo, Pia ukiweka sumaku inanata kana kwamba inagusa chuma kitu ambacho ni tofauti na mawe mengine ya kawaida tunayoyafahamu, Tatu ukigonga gonga kinatoa Mlio kana kwamba ndani kinauwazi mithiri ya Debe tupu
Kihistoria hakuna binadamu aliyeshuhudia kimondo hiki kikianguka kutoka angani, Katika pitapita za bwana yenga yenga mjini akakutana na William Helman Nott, Soroveya (Mchora Ramani) kutoka Johannesburg ambaye akawa rafiki yake ndipo akamueleza kuwa kijijini kwetu tuna jiwe (Nyota) ya maajabu ambayo wazee wa kimila hulitumia kuabudia, Ndipo mzungu akaomba kwenda kuliona jiwe hili, Mara baada ya kuona aliandika hekaya ya kwanza kutokana na masimulizi aliyoyasikia kwa wenyeji na akaweza kuchorea michoro mbalimbali mnamo mwezi Oktoba mwaka 1930 na kasha kuiwasilisha kwa Serikali ya Kikoloni
Mnamo mwaka 1931, Walitumwa wataalam wa miamba kwa ajili ya kufanya tafiti wakiongozwa na Dakt. D. R. Grantham wa Chama cha Jiolojia walikata sehemu ya kimondo nambacho kilikuwa na Kilo Tano (5) ambacho kilisaidia sana kujua uzito wa kimondo, Pamoja na aina ya madini yaliyomo katika Kimondo hiki. Kisehemu hicho kinaweza kuonekana katika makusanyo wa vimondo kwenye Jumba la Makumbusho la Uingereza huko London.Anasema mnamo mwaka 1967, kimondo hiki kilionekana kinadidimia taratibu kadri siku zinavyoendelea ikabidi waweze kukijengea kwa kimtaro kukizunguka, na kufanya kionekane kana kwamba kimeinuliwa na kuwekwa juu ya madhabahu ya mawe.Namna ya Kufika, Kimondo hiki kipo umbali wa kilometa kumi na mbili (12) kutoka barabarani katika kijiji cha mahenje, kusini mwa Tanzania, katika barabara kuu ya Tanzania- Zambia, njia kuu ya kwenda Tunduma.
For more details and booking please contact us via.
Email: info@uyoleculturaltourism.com
Phone: +255783545464
P. O. Box 475 Uyole Mbeya.
Website: www.uyoleculturaltourism.com
Facebook: Uyole cultural tourism enterprise
Facebook: Uyole CTE
Instagram: @uyoleculturaltourismenterprise
Twitter: @uyolecte