Kimondo cha Mbozi ni kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
KIMONDO CHA MBOZI
1605687773920.png

Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kilianguka kutoka anga-nje karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa takribani tani 16, kilianguka katika kilima cha Mlenje, wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe, Tanzania. Kipindi hicho Songwe ikiwa ni moja ya wilaya ya Mbeya.

Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.

Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8.69%, sulfuri 0.01% na fosfori 0.11% ya masi yake. Ndani yake vipande vidogo vya silikati vinapatikana.

Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za kasoko; kwahiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa pembe butu sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na mmomonyoko.
 
... tani 16 za chuma si haba! Kwanini kisiuzwe serikali ya mkoa ikapata mapato? Kama chuma chakavu mtaani tunauza kg sh. 500 tani 16 x 1000 x 500 = 8,000,000/= hiyo.
 
Sasa hiyo milioni nane itafanya shughuli gani kubwa itakaonekana kizazi hadi kizazi? Halafu hiyo milioni 8 inaweza kupatikana kwa wataliii wanaoingia pale kwa mwaka mmoja, hebu ongeza bei
 
... tani 16 za chuma si haba! Kwanini kisiuzwe serikali ya mkoa ikapata mapato? Kama chuma chakavu mtaani tunauza kg sh. 500 tani 16 x 1000 x 500 = 8,000,000/= hiyo.
Huenda wanapata zaidi kutokana na utalii.
 
Sasa hiyo milioni nane itafanya shughuli gani kubwa itakaonekana kizazi hadi kizazi? Alaf hiyo milioni 8 inaweza kupatikana kwa wataliii wanaoingia pale kwa mwaka mmoja....hebu ongeza bei
Milion mia.
 
1_20250303_092433_0000.png

Kuna tukio kubwa lilitokea mwaka 1930 ambapo Tanzania kiliweza kutua kimondo kikubwa maeneo ya nyanda za juu ya kusini Mkoa wa Mbeya nchini Tanzania.

Kimondo hicho kinaitwa Mbozi ni kimondo ambacho kiligunduliwa miaka ya 1930 kina ukubwa wa Tani 12 ni Cha nane kwa Ukubwa Duniani.

2_20250303_092433_0001.png

Kimondo hichi ni kikubwa Cha upili barani Afrika baada ya Kimondo Cha Hoba kilichopo nchini Namibia ndicho kimondo kikubwa Afrika na Dunia kwa ujumla.

Kwa Mara ya kwanza Mtu wa kwanza kukiona alikua jamaa mmoja anaitwa Halele Sambaya , Halele baada ya kugundua kimondo hicho alitoa taarifa kwa uongozi wa Kijiji na wenyeji wakaanza kuabudu katika shimo ambalo linahifadhi maji na wenyeji wanatumia kunawa na kuabudu wakaanza kutumia kwa kusafisha nyota.

Moja wapo ya maajabu ya Kimondo hicho ni kuwa hakipati Joto hata wakati wa jua Kali katika msimu wa kiangazi. Watu walikua wanakikata kata na kukitumia kwenye mambo ya ushirikina.

3_20250303_092433_0002.png

Kwa sasa kinatumiwa kama utalii kikiwa na shimo kubwa linalozunguka eneo Hilo la kimondo Cha Mbozi ambapo wakati kilianguka kilitoa mshindo mkubwa na mwanga pamoja na sauti ya Ajabu.
 
Moja ya vivutio vyanavyo sahauliwa, nakumbuka zamani tulifanya safari ya Shule tukafika hapo kwaajili ya kukiona na kujifunza zaidi.
 
KIMONDO CHA MBOZI
View attachment 1629019
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kilianguka kutoka anga-nje karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa takribani tani 16, kilianguka katika kilima cha Mlenje, wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe, Tanzania. Kipindi hicho Songwe ikiwa ni moja ya wilaya ya Mbeya.

Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.

Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8.69%, sulfuri 0.01% na fosfori 0.11% ya masi yake. Ndani yake vipande vidogo vya silikati vinapatikana.

Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za kasoko; kwahiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa pembe butu sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na mmomonyoko.
Nilishafika huko mkuu,kuna maprofessa Duniani wanafika hapo!
 
Back
Top Bottom