Kimsingi tozo bado hazijafutwa kwa sababu zifuatazo

Tozo hazitatupeleka popote, its just a shoft term solution, wanasiasa mlioshika usukani wa kuongoza dira ya taifa tumieni hizo bongo zenu kuwaza namna ya kugenerate long term solutions za kulikomboa hili taifa kutoka kwenye utegemezi.
 
Kiukweli tutamkumbuka sana hayati JPM, pamoja na yote, alisaidia watu kufikiri kabla ya kutenda kwa hofu ya kutumbuliwa. Hata kama wanaiita nidhamu ya uoga, ila ilisaidia sana!
Viongozi wa sasa ni waonevu sana!
Majibu na maamuzi yao yanakatisha tamaa
Jenga hoja bila kumtaja huyu dikteta muuaji, mtekaji na mporaji
 
Hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanywa. Nani anaenda kwenye ATM kutoa elfu 30?
amesema mabadiliko hayo yataanza tarehe 01 mwezi wa 10 ila hii nchi ni ngumu sana watu tunapelewa pelekwa tu kama mazombie na hawa wanasiasa
 
Kutakuwa na nafuu kidogo kwenye miamala ya simu..

Pili hivi kama kwenye ATM wamefuta tozo inamaana gharama zitabakia kama zamani,huenda wakapandisha Kodi kwa makampuni ya banks na simu so pesa itabakia pale pale..
 
Kutakuwa na nafuu kidogo kwenye miamala ya simu..

Pili hivi kama kwenye ATM wamefuta tozo inamaana gharama zitabakia kama zamani,huenda wakapandisha Kodi kwa makampuni ya banks na simu so pesa itabakia pale pale..

Hakuna nafuu yoyote
 
Ngoja niendelee kusoma ni nini kilijadiliwa,nielewe vizuri....
 
Heko kwa uchambuzi murua sana.
 
Huyu mwizi wa vyeti ana kichwa kigumu sana. Ana tuona Watanzania ni wajinga hawafuatilii mambo yao.
Yaani amemdharau Mh. Rais na Chama chake cha Mapinduzi.
Iko siku yaja atajua hajui.
 
Natoa ushauri wa bure kwa Mh. Rais wetu na mwenyekiti wa Chama Cua Mapinduzi,
Asije huko alikoenda kwa papara akazungumzia huu utumbo wa Mwigulu kwamba wamepunguza tozo. Awaite wasaidizi wake wa karibu wamueleze ukweli kwamba Mwigulu haja punguza tozo bali ame wahadaa Watanzania.
Kinyume na hivyo atadharaulika na Watanzania wote.
Mie nashauri ambadilishe Mwigulu akiwa kwenye ndege kabla ya kutua hapo Dar. Hii ita mjengea heshima kubwa sana.
 
Jenga hoja bila kumtaja huyu dikteta muuaji, mtekaji na mporaji
Siwezi mkuu.
Siwezi kuwa mnafiki!
Ukiwa mnafiki ujanani, uzeeni utakuwa mchawi!

Sasa hivi ziara na safari za viongozi ndani na nje ya chini zimeshika kasi.
Hii kitaifa haina tija bali inamnufaisha mtu mmoja mmoja na familia yake.

Pengo kati ya walionacho na wasionacho linazidi kuongezeka.

Viongozi wengi wameziba maskio kusikia kilio cha wananchi maskini!
Kila kitu bei juu!

Utanisamehe bure, ila siwezi kuacha kumtaja na kumkumbuka!
 
Ndo maana wengine tumeshashtukia hizo ni danganya toto tu, madelu jambo sahihi analopaswa kufanya kwa sasa ni kujiuzulu.....
Ajiuzulu? Uliona wapi walamba asali wakajiuzulu? Akale wapi? You must be joking
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…