Kimya cha CCM katika matatizo makubwa ya kijamii ndiyo mwanzo wa kifo chake

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,653
Reaction score
31,010
CCM sasa hivi ni kama bubu.

Kuna matatizo makubwa ya kijamii, chenyewe kimya kama bubu.

Watu wameuwawa wakati wa uchaguzi. CCM haijatoa tamko rasmi.

Sasa hivi maji hakuna sehemu nyingi nchini, CCM kimya.
Inaelekea sasa CCM ni gulio tu la uongozi na haisimamii matakwa na kero za wananchi.

CCM ikifa, haitapata waombolezaji, isipokuwa wafaidika wachache.
 
Unaitegemea ccm ikupe maisha borra ? Pole.
 
KWA MAZINGIRA YA SASA GEN Z WAKITANGAZA MAANDAMANO HATA KAMA HAWATAFANYA, VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA LAZIMA VIWEKE LOCK -DOWN.

KUWEKA LOCK-DOWN MAANA YAKE NI KUKWAMISHA SHUGHULI NYINGI ZA KIUCHUMI; UTALII UNADORORA ZAIDI, BANDARI KUNASIMAMA, USAFIRI WA ANGANI NA ARDHINI UNADORORA ZAIDI NA MAPATO YA SERIKALI YANAPUNGUA.
 
Hakuna tofauti na seikali ya kikoloni iliyokuwa ina react to circumstances badala ya kuwa pamoja na wananchi kimaendeleo.
 
CCM sasa hivi ni kama bubu.

Kuna matatizo makubwa ya kijamii, chenyewe kimya kama bubu.

Watu wameuwawa wakati wa uchaguzi. CCM haijatoa tamko rasmi.

Sasa hivi maji hakuna sehemu nyingi nchini, CCM kimya.
Inaelekea sasa CCM ni gulio tu la uongozi na haisimamii matakwa na kero za wananchi.

CCM ikifa, hsitspata waombolezaji, isipokuwa wafaidika wachsche.
Discern the reality. Kiuhalisia CCM sio chama cha siasa; bali ni koti la kisiasa linalovaliwa na genge lenye dola ili kupambana na vyama vya siasa, asasi za kijamii na wananchi wanaohoji mamlaka kwa ujumla.

Tangu 29 Oktoba hilo koti limepumzishwa - limening'inizwa pale Lumumba. Mazingira ni magumu sana. Koti hilo halihitajiki wakati huu. Halina umuhimu. Dola yenyewe ndio iko kazini kudhibiti hali. No pretence.

Mambo yakikaa sawa - endapo yatatulia na maisha kurejea kama kawaida - koti litavaliwa tena na utasikia tena shamrashamra za "CCM OYEE!" zikirejea kwa bashasha zote. Utashuhudia malori na matrekta yakirejea kazini kujaza mafuriko ya nyomi kila kona. Pengine hata wasanii kupanda majukwaani tena! Yatakuwa ni maajabu mengine ya Tanzania - kisiwa cha amani na utulivu minus Haki! 🤔 😳
 
Spot on!
 
CCM sidhani kama kuna kitu wanafikiria zaidi ya kupata vyeo vya umma.
 
Kinachosikitisha ni kwamba CCM sasa inaitumia serikali kukandamiza wananchi.
Hatujasikia CCM ikilaani wala kuomboleza vifo vya wananchi katika uchaguzi wa Oktoba 29.
CCM imebaki kuwa chama cha kuitumia serikali kulinda maslahi ya wachache.
 
Discern the reality. Kiuhalisia CCM sio chama cha siasa; bali ni koti la kisiasa linalovaliwa na genge lenye dola ili kupambana na vyama vya siasa, asasi za kijamii na wananchi wanaohoji mamlaka kwa ujumla.

Tangu 29 Oktoba hilo koti limepumzishwa - limening'inizwa pale Lumumba. Mazingira ni magumu sana. Koti hilo halihitajiki wakati huu. Halina umuhimu. Dola yenyewe ndio iko kazini kudhibiti hali. No pretence.

Mambo yakikaa sawa - endapo yatatulia na maisha kurejea kama kawaida - koti litavaliwa tena na utasikia tena shamrashamra za "CCM OYEE!" zikirejea kwa bashasha zote. Utashuhudia malori na matrekta yakirejea kazini kujaza mafuriko ya nyomi kila kona. Pengine hata wasanii kupanda majukwaani tena! Yatakuwa ni maajabu mengine ya Tanzania - kisiwa cha amani na utulivu minus Haki! 🤔 😳
CCM bye bye, kuna mtu kasema CCM ni idara ya serikali kama vile Magereza, JKT na Polisi.
 
CCM imeamka kwa kutetea wananchi kuhusu kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kupanda bei za mafuta.
Lakini bado, kulaani Oktoba 29 au kutoa tamko hatujaisikia CCM.
 
Back
Top Bottom