Kina baba wakibongo huwa mnaogopa kina mama wajawazito?

FirstLady1

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2009
Posts
16,789
Reaction score
5,401
Nimekuwa nikiangalia tofauti kati ya wanaume wa kizungu na wa kibongo the way wanavyo wa treat ,care wake ,wachumba au wapenzi wao ktk kipindi chote cha kulea ujauzito...
Kwanza anafeel kama hiyo Preg iko kwake ...kila sec anamcheck atafanya juu chini uwe na mapumziko ya kutosha ..atapapasa hilo tumbo kama vile sijui liamie kwake kumjali akiumwa kidogo ndo basi utadhani anaumwa yeye kila kona atakopita leo my wife kawa hivi mala vile na hata kazini anaweza shinda kutwa akiongea kuhusu wife ataongelea ujauzito wa mwenzi wake kwa furaha kila mala today 1 month ,2,3, 4,..9 akikaribia kujifungua ndo usiseme na akijifungua sasa mtasimuliwa nyie mpaka loh..!!

hata siwezi kuielezea hali hii ...

ila nyie wakibongo huwa mnaogopa kina mama wajawazito au mnaona ni hali ya kawaida tu??
FL1
 
Labda mmeo tu FL1. Mie wife alipokuwa na katumbo, nlikuwa sichezi naye mbali mpaka alipojifungua kabinti ketu. Hakuna raha kama kujivinjari na bibie mjamzito, unajidai naye kinoma. Dunia inajua we rijali bana. Hahahaha! Sijui tutafute katoto kengine(off point hii)
 
Mambo Chriss,kama ni kweli mkuu ulikua unamfanyia hayo mrs wako hongera sana.
 
Mambo Chriss,kama ni kweli mkuu ulikua unamfanyia hayo mrs wako hongera sana.

Poa Msindima. Weekend ilikuwaje? Serious! Msizichukulie serious hizi blahblah za humu jamvini. Sisi waume bora kabisa. Wake zetu wako proud na sisi. Najaribu kutafakari labda tufanye mpango wa kengine. Problem uchumi. Mtu unashindwa hata kunywa kabia kwa sababu ya malezi ya watoto. Lol!
 
hapa siongelei swala la ngono bwana hilo lipo tu ..naongelea vile unavyofeel mwenzio akiwa mjamzito kuna wengine utakuta anamfokea ,hathamini ile hali aliyo nayo anaona kawaida tu na mengineyo
 
hapa siongelei swala la ngono bwana hilo lipo tu ..naongelea vile unavyofeel mwenzio akiwa mjamzito kuna wengine utakuta anamfokea ,hathamini ile hali aliyo nayo anaona kawaida tu na mengineyo

Hebu soma post yangu vizuri uone kama kuna sehemu nimeongelea ngono!
 
Ni kweli FL1 ila tatizo linalojitokeza mpaka iwe hivyo ni kwamba baadhi ya mimba huwa haziwapendi waume yaani mke akipata mimba mume akirudi mama anachukia mara hiki mara kile mara nataka mahindi yakuchoma wakati ni kiangazi mara mlenda mara unanuka mara sitaki hata kukuona.

Yaani unakuta ni vurugu mai.
We acha tu tofauti na wao sijui ni kasumba au lahh
 
Hebu soma post yangu vizuri uone kama kuna sehemu nimeongelea ngono!

asante basi mie nilivyosoma nikajua ni hivo

haya nambie how do you feel wife anapokuwa na preg ..
maana kuna mmoja hapa nilimuona alichanganyikiwa wife alivyomwambia ana mimba ..

ilikuwa ni kama kuimba wimbo wa Taifa kila inaposhushwa bendera
 
Hahahaha! Nakumbuka nilishaamshwa saa sita za usiku nikamtafutie mamsap mahindi ya kuchoma. Bahati nzuri nilikuwa na stock ndani, ingekula kwangu. Hahaha! Mimba bana! Acheni mwanamke aitwe mama. Ndio maana mapenzi yangu kwa wanawake hayatakaa yaishe. I love them all.
 
Weekend ilikua poa kabisa,jana nilienda kuwasalimia wazazi wangu,kwa hiyo nilipotoka tu kanisani nikaenda,kwa ushauri ongeza kengine haraka.
 
kweli chaku
mie zama hizo nilkuwa na ka mood kangu leo nimeamka na furaha kesho nimenuna kila kitu kibaya mradi visa tu ...
mala mzee ashindwe kutabiri nyakati
 
Weekend ilikua poa kabisa,jana nilienda kuwasalimia wazazi wangu,kwa hiyo nilipotoka tu kanisani nikaenda,kwa ushauri ongeza kengine haraka.

Hahaha! Lol! Haka kamoja tu jasho linantoka. Ngoja kwanza tumalizie honeymoon yetu na mamsap. Honeymoon kwanza then malezi yatafuata.
 
Hahaha! Lol! Haka kamoja tu jasho linantoka. Ngoja kwanza tumalizie honeymoon yetu na mamsap. Honeymoon kwanza then malezi yatafuata.

Ha hahaaaaaaaaaa,
ulilianzisha kabla ya honeymoon, nini! maana wababa wa siku hizi ndo zenu
 
Ha hahaaaaaaaaaa,
ulilianzisha kabla ya honeymoon, nini! maana wababa wa siku hizi ndo zenu

Actually tulipanda madhabahuni tukiwa watatu. Si unajua mambo ya kutest zali? Sasa tunachumbiana upya. Hahahaha!
 
kweli chaku
mie zama hizo nilkuwa na ka mood kangu leo nimeamka na furaha kesho nimenuna kila kitu kibaya mradi visa tu ...
mala mzee ashindwe kutabiri nyakati

Ila sometimes tunaamuaga tu kuwakomesha hawa wababa, hakuna cha kamood wala nini (ingawa kuna ambao waka vimood vya kikweli kweli), ili wajue tupo kazini.
Kuna rafiki yangu huwa ananihadithia kwamba mumewe huwa hana time naye, kwa hiyo anapokuwa preg ndo ana-take advantage ya kuwa spoiled na husband wake, kwa hiyo anahakikisha miezi yote 9 anadeka kikweli kweli
 
Actually tulipanda madhabahuni tukiwa watatu. Si unajua mambo ya kutest zali? Sasa tunachumbiana upya. Hahahaha!

ha ha haaaaaaaaaaaa, afadhali lakini uliamua kujisalimisha madhabahuni mkiwa 3, wengine wana-produce tu wala hawakumbuki kama kuna kwenda madhabahuni. Hongera sana
Ila sasa unaona madhara yake? huyo mtoto anahitaji care yenu, nyie mpo busy kumalizia honeymoon
 
[/QUOTE] Wanawake Ni Wasanii?
PakaJimmy
31st July 2009, 07:41 AM
Awali nilikuwa naambiwa, lakini baadaye nikaja kuhakikisha kwamba Wanawake pindi wawapo wajawazito huwa wasumbufu saana, na wanadeka ajabu!

Mwanamke mmoja akaja kunambia kwamba huwa wanafanya hayo mambo makusudi, maana ni nafasi yao ya pekee ya kutesa, kuomba kila watakacho, na kuwaonyesha mabwana zao kwamba ile shughuli ya kubeba mimba ni ya pekee, maana wanajua kwamba wanaume hawana uzoefu, na wala hawatakaa waijue!

Ni kweli mara chache huwa wanaumwaumwa, lakini asilimia kubwa huwa ni matatizo ya kupangwa na yanaandaliwa na kupikwa kitaalam!

Je wanaJF, tudhibiti vipi hii hali ya kuonewa na hawa raia wa kike?
[/QUOTE]
 
Hahaha! Kabinti kanaweza kujifunza tabia mbaya! Manake bado tunabebana mgongoni na kukimbizana kama paka na panya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…