Kina dada wa kitanzania

Kina dada wa kitanzania

nyumba kubwa;Kujipamba kwa mwanamke ni wajibu. Ila kujichubua ni dhana potofu na kwa mtazamo wangu ni elimu ndogo inayofanya wanawake wajichubue kwa kuwa hawajuhi madhara yake including ngozi kuchakaa upesi. Kuna kitu ambacho mimi pia sikifagilii japo ni mwanamke. KUFUGA KUCHA. Utakuta dada anafuga kucha tena wakati mwingine mikono yote miwili. Mimi siwezi kula chakula cha mtu aliyefuga kucha kwani siamini kuwa hizo kucha ni safi ukizingatia maswala ya toilet. Na sijuhi wanajiswafi vipi na makucha.

Nyumba Kubwa,


Hapo kwenye nyekundu na mimi kwakweli huwa nashangaa. Unakuta mdada kafuga au kaweka makucha marefu, nabaki kujiuliza kwa jinsia yenu wadada usafi unafanyikaje na hayo makucha marefu. Kwakweli huwa naona uchafu na kinyaa. Sifagilii!
 
kaka unaishi karne ipi? au unaelimu kiasi gani? Unasound kama bully umfujaji wa wanawake. au wewe ndio wale design ukishaoa you posses your wife like your slave? mkeo afunike hadi macho anapotoka? Huyo ni mkeo si mtumwa wako, anahaki ya kujipamba apendavyo na sio sababu watu wengine watamuangalia. Amka usingizini kaka, MWANAMKE NI PAMBO LA DUNIA, KAMA ILIYVO MAUA PAMBO LA BUSTANI. NA aCTUALLY NI WANAWAKE WA DUNIA NZIMA HUJIPAMBA SIO TU WATAZANIA.
 
Mi nazan wazungu wanajipamba zaidi kuliko sisi, msiseme tunawaiga no! Its natural. Muulizen Cleopatra na Malkia wa Sheba enzi za Mfalme Suleman. Wanawake wa kizungu wamezidi! Lakini haisemwi! Ni wanawake weusi tu ndio wanasakamwa wakati hiki kitu ni natural. Yaani hata kama mume sina, nikiamka asubuhi naanza kujipamba tu. Angalia kabinti kako au kadada kako kama huna kabinti ka ndugu yako au jirani, kakifikisha miaka 5 hadi 9 hivi utakaona kanahangaika kujipamba. Kakivunja ungo ndio kabisaaa! Na hii ni wanawake wote dunia nzima. Sasa labda useme tu kwamba, wewe binafsi hupendi mwanamke anayeweka makucha ya bandia, mawigi n.k. lakini nakwambia, hata wanawake wa kizungu wamezidi tena wamezidi haswaaaa, sie tuna unafuu maana urembo wa asili tunao. Ukiwa hupendi, tafuta asiyeyapenda hayo pia, hayo manyongeza nyongeza yaliyozidi kwa upande wako.
 
Back
Top Bottom