Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
Mnyukano wa kugombania madaraka ndani ya Chadema sasa umethibitika. Tayari Hilda Newton na Devotha Minja wameanza kukinyemelea kiti cha Halima Mdee Bawacha. Wanafanya kila mbinu kuhakikisha kwamba Mdee na wenzake hawarudi. Wanatumia nguvu kubwa kupamba na kundi la kina Mdee kuliko nguvu ambayo imewahi kutumika kupambana na chama tawala cha CCM.
Juzi 29 Desemba 2020, Hilda Newton aliandika meseji ya twitter ifuatayo: "Aliyewaandikia Barua za rufaa Mzee Halima na wenzake Mungu anamuona yani maelezo yao wote yanafanana cha tofauto ni sahihi tu."
Anachosahau Hilda Newton ni kwamba, hata barua za tuhuma kwenda kwa kina Mdee zote zinafanana isipokuwa sahihi pekee!
Na hapo awali, Devotha Minja aliongoza maandamano ya kuilazimisha Kamati Kuu kuwafukuza kina Mdee. Maandamano hayo yalichukuliwa na kamera kama ifuatavyo:
Kwa hiyo sasa, BAWACHA imemeguka katika sehemu mbili: Bavicha ya Mdee na Bavicha ya kina Hilda. Hii maana yake ni kwamba, sasa Baraza Kuu linayo kazi ya ziada.
Linapaswa kuhakikisha kwamba BAWACHA inasimama kwa kutenda haki bila kuzingatia shinikizo lolote. Hoja zilizo katika rufaa ya kina Mdee ni nzito.
"Kuwabatiza majina mabaya kina Mdee, kama vile COVID19 na mengine hakusaidii kumaliza tatizo. Badala yake kunazidi kuongeza mpasuko ndani ya Chadema. Kwa hakika mie naona kuwa kina Hilda na Devotha ni hatari kuliko kinachoitwa covid19. Nashauri tangu sasa tuwaite kina Hilda na Devotha covid19+," alisema mwana Chadema mmoja kwenye kundi moja la whatsapp.
Nao wajumbe kadhaa katika kundi jingine la whatsapp wameonekana wakiandika maneno yanayofanana na hayo.
Mmoja anasema:
"Ninachojua kuna kina mama wa Bawacha walitaka kwenda Bungeni ila baada ya majina yao kutokuwemo kwenye list ya Halima, sasa hivi ndio vinara wa kushambulia waliokwenda kuapa kwa hoja eti wamesaliti chama."
Mwingine anaandika hivi:
"Ndio maan nasema haya mambo yaacheni tukutane nao kwenye vikao. Tutaelewana vizuri huko kwenye vikao. Hapa mtararuana bure. Haisaidii."
Mchangiaji wa tatu anasema:
"Katika suala ka kupeleka wabunge wa viti maalum Bawacha hhaikuwa na mpango wa kususia nawaambieni. Haya mengine tumshukuru Mungu nafasi zimekuwa chache. Wamegawanyika na hapo ndipo tulipoponea kama chama. Vinginevyo hawa akina Mama walikuwa wamoja before."
Hii maana yake ni kwamba, kelele za kina Hilda na Devotha ni kama kelele za sungura aliyesusa ndizi mbivu kwa kisingizio kwamba ni mbichi. Alikuwa ameshindwa kukwea na kuzifikia.
Baraza Kuu la Taifa la Chadema litapaswa kuyazingatia haya yote kusudu liweze kuwatendea haki covid19 bila kuwapendelea covid19+ wanaoungwa mkono na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe.
Magazeti ya Saed Kubenea yakuza mpasuko ndani ya Chadema
Wakati mpasuko kati ya kambi ya covid19 na kambi ya covid19+ ukichomoza taratibu magazeti yanayoendeshwa na Saed Kubenea, yakiwemo Mwanahalisionline.com na Raia Mwema, yamekuwa yanachukua hatua za kupanua mpasuko huo kwa kasi.
Kwa mfano, mtandao wa mwanahalisioniline.com umewashutumu wabunge hawa ukidai kwamba, kwa sababu ya uamuzi wao wa kukata rufaa mbele ya Baraza Kuu badala ya kuandika barua ya kuiomba Kamati Kuu ufanye marejeo ya uamuzi wake wa kuwafutia uanachama, "kina mdee wameanzisha vita mpya Chadema."
Habari hii ya gazeti la mtandaoni ilichapishwa tena kwenye gazeti la karatasini la Raia Mwema, tarehe 30 Desemba 2020, kama habari kuu iliyosomeka "Mbowe, Mdee waingia vitani," kwenye ukurasa wa mbele na ukurasa wa 3.
Ukurasa wa mbele wa gazeti jipya la Saed Kubenea, liitwalo Raia Mwema, ukimtuhumu Mdee kuanzisha vita dhidi ya Mbowe, ndani ya Chadema (Raia Mwema, Toleo Na. 744, 30 Desemba 2020, ISSN 1821-6250)
Katika habari hii, kina Kubenea wanasema yafuatayo, kati ya mengine:
Kwamba, "waliokuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18, wameingia katika vita mpya ya kisiasa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ... kutokana nahatua yao ya kuishtaki Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, inayoongozwa na Mbowe, kwa Barza Kuu la Taifa (BKT), kupinga kuvuliwa uanachama. (uk.3)"
Kwamba, "... [mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu anasema kuwa] ikiwa mwenyekiti atashindwa na kina Mdee katika jambo hili maana yake ni kuwa Mdee na wenzake wana nguvu kuliko yeye na Kamati Kuu jambo ambalo hataruhusu kutokea. (uk.3)"
Kauli hii inayo dosari kubwa kwani, sio Mdee wala Mbowe aliye juu ya Katiba ya Chadema. Katiba ikisimama, yeyote kati ya Mboowe na Mdee anaweza kuonekana mkosefu. Kufikiri kuwa Mbowe ni malaika ni upofu wa hali ya juu wenye asili yake katika falsafa ya mkubwa huwa hakosei inayokumbatiwa na Kamati kuu ya Chadema kimakosa.
Aidha, gazeti la Raia Mwema linasema kwamba, "[Mwenyekiti wa Chadema, Jimbo la Segerea, Patrick Asenga, amesema kuwa] ikiwa Mbowe ataamua kuwa busara itumike na watuhumiwa hao walipachikwa jina la covid19, wasamehewe na kurejeshewa uanachama wao... Mbowe atalazimika kujiuzulu. (uk.4)"
Na linasema kwamba, "uchunguzi uliofanywa na gazeti hili [la Rai Mwema] umebaini kuwa baadhi ya wajumbe wasiompenda Mbowe [na wafuasi wake kina Hilda Newton na Devota Minja waliopachikwa jina la covid19+] wameanza kuungana na akina Mdee na kuahidi kuwa wanasubiri kwa hamu chama kiitishe Baraza Kuu [ili wamshughulikie Mbowe na kambi yake ya covid19+] (uk.4)."
Wanachofanya kina Kubenea hapa ni kutengeneza matabaka hasimu ndani ya Chadema na kuyaba lebo zinazopingana kimaana.
Tabia ya kutengenza lebo za majina mabaya dhidi ya kambi ya watu baki, kama yanavyofanya magazeti ya kina Saed Kubenea, imewahi kuwa na madhara makubwa sana katika historia ya dunia.
Mfano, huko Rwanda Wahutu walitumia gazeti la Kangura kuwabatiza Watusi jina la MENDE ili waonekane ni binadamu hafifu.
Huko katika Ujerumani ya Hitler chama cha NAZI kiliwabatiza wayahudi jina la PANYA ili kuonyesha kuwa wayahudi ni binadamu hafifu.
Na wafanya biashara ya utumwa waliwabatiza watumwa majina kama vile "shwine (nguruwe)" ili kuonyesha kuwa ni binadamu hafifu.
Mchakato wa kubatiza watu majina yanayowashushia hadhi ni hatua ya kwanza katika msululu wa matukio ambayo huzalisha mauaji ya halaili kwa sababu za ama kidini, kisiasa, kinasaba, au vinginevyo.
Yaani, mauaji ya halaiki kwa sababu ya kisiasa (politicide), kinasaba (genocide), kikabila (tribocide), au sababiubaki zinazoweza kuhalalisha mauaji ya halaiki (democide), hupitia hatua nane, ambazo ni: "classification, symbolisation, dehumanisation, organisation, polarisation, identification, extermination and denial." Yaani:
- Kutengeneza matabaka (Classification): Kuzalisha matabaka ya watu, kama ambavyo Kamati Kuu ya Chadema imefanya kwa kutengeneza tabaka la wasaliti, waasi, na wavurugaji (Mdee na wenzake) dhidi ya kambi ya watiifu, waaminifu na wastaarabu (kina Hilda Newton na Devota Minja)
- Kutengeneza nembo za utambulisho (Symbolisation): Kutumia alama maalum kuyatambulisha matabaka, kama ambavyo kina Devotha Minja wamefanya kuwatambulisha kina Mdee kama kambi ya kirusi cha covid19, na kama ambavyo wafuasi wa kina Mdee wanafanya kuwatambulisha kina Hilda na Devota kama kambi ya kirusi cha covid19+
- Kudhalilisha tabaka baki (Dehumanization): Kutengeneza na kusambaza propaganda zinazodhalilisha tabaka baki, kama ambavyo kina Devotha walifanya kwa kutengeneza mabango na kuratibu maandamano yaliyowatambulisha kina Mdee kama kambi ya kirusi cha covid19.
- Kujipanga kwa ajili ya kulishughulikia tabaka baki (Organisation): Kutengeza vikundi vya utendaji ili kutekeleza malengo ya pamoja dhidi ya tabaka baki, kama ambavyo baadhi ya viongozi wa Chadema walifanya kuhamasisha na kuwafadhili kina Devotha waingie barabarani kupambana na kina Mdee.
- Kugawanya watu wote katika makundi ya nani mwenzetu na yupi sio (Polarisation): Kuwagawanya watu katika kundi la anayetupinga na anayetuunga mkono, kama ambavyo magazeti ya Kubenea yanafanya kwa kuwachonganisha kambi ya kirusi cha covid19 aliko Mdee dhidi ya kambi ya kirusi cha covid19+ aliko Mbowe.
- Kuwatambua watu wanaopaswa kushughulikiwa (Identification): Kutengeneza orodha ya watu wanaopaswa kushughulikiwa.
- Kuwashughulikia watu wa tabaka baki (Extermination): Kuwamaliza watu wasiokubaliana nasi.
- Kuharibu ushahidi na kukana tuhuma za kuhusika na uhalifu (Denial): Kuharibu ushahidi kwa kuchimba makaburi, kuunguza miili ya maiti, kuwatisha mashuhuda wa uhalifu na kuzuia uchunguzi huru.
Kwa hiyo, magazeti yanayomilikuwa na Saed Kubenea, yaani gazeti la Raia Mwema na MwanaHalisionline.com, yanapaswa kuchunguzwa sana.