Oh mkuu, ni vyema ukiangalia hiyo thread nadhani maelezo yamejitosheleza muungwana ila kwa kujazia tu ni kwamba kuna ardhi ambazo ziko maeneo ya Loliondo hivyo tangu enzi zilikuwa zikimilikiwa na wazawa wa hayo maeneo ambao ni wamasai, hivyo kulikuwa na kampuni ya kimarekani iliyokuja kuwekeza Tanzania katika sekta ya utalii miaka mingi sasa na kila siku zilivyokuwa zinasonga mbele wao walikuwa wanamega ardhi za wazawa kwa mabavu na pia kushirikiana na serikali yenyewe kuwaumiza wananchi na pia kuwafilisi wananchi, hivyo hiyo hali iliendelea kwa muda mrefu sana tena sana wakati huo serikali ilikuwa ikifumbia macho hiyo tabia, mpaka ilipofika mwaka 2008 alikuja mwandishi wa habari kutoka New Zealand ndipo alipokutana na huo mkasa ndipo hapo yeye alipoamua achunguze hayo madai huku akichukua picha na videos kama attachment juu ya hayo matukio yaliyokithiri, kabla ya kumaliza alihisi kutaka kuuliwa na askari wa serikali wakishirikiana na hao askari wa Thomson Safaris, yeye alipoona hivyo aliamua aondoke zake kwenda Kenya ikiwa alikuwa njiani kuchukua ndege kurudi kwao hivyo wakamuua alipokuwa akitokea bar kwenda hotelini kwake na hivyo serikali ya Tanzania inaficha huo uharamia walioufanya kwa huyo mwandishi na pia wananchi wake na hata hivyo inaonekana wanabadili vipengele vya sheria ili kujiweka mahala ili wasishtakiwe ndio maana unaona tunaumia sisi ila wao NOPE