Kifaurongo
JF-Expert Member
- Jan 18, 2010
- 4,221
- 2,359
Hizo unazoziita kashfa zimejadiliwa sana humu na zimetolewa sana ufafanuzi lakini sababu ya mihemko ya mahaba ya kivyama hakuna anayekubaliana na mawazo ya mwenzie.mkuu tuelewane kdg..hata mimi napenda tanzania tuache habar ya misaada ili tujenge msingi mzuri wa kujitegemea na kuondo foreign influence kwe mambo yetu..ila mi nashangaa watu wanataka kuficha sababu ya sisi kusitishiwa misaada ni nini badala yake wanadandia ooh inabidi tujitegemee misaada haina maana..kabla hatujafika huko kwanza tumezikosa hz pesa kwasababu ya mambo yaliotajwa.......tuache misaada sawa ila sio tusitishiwe misaada kwa vikashfa flan tutofautishe hapo mkuu..haijalishi rais ni nani..lets say yalitokea lets say tusitishiwe misaada kisa yalitokea mauaji ya halaiki halafu c tujisifu eti hatutaki kuwa tegemezi noo...km tumeamua kutopokea hapo sawa ila sio tusipokee kisa tumepiga blanda flani
Sababu ya kwanza ni kunyimwa msaada huu ni kutoridhishwa ni jinsi ulivyoshughulikiwa mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar na kurudiwa kwa uchaguzi huo ambao haukuwa shirikishi. Mtanzania gani leo ni kipofu wa juhudi zilizofanywa kushughulikia mgogoro huu? Yale mazungumzo ya kutafuta muafaka haikuwa juhudi ya kushughulikia tatizo? aliyekwamisha mazungumzo yale alikuwa nani aliyeenda Serena Hotel na kutangaza hana shida ya maridhiano? Kurudiwa kwa uchaguzi ni matokeo ya mtu kudanganywa ajitoe katika mazungumzo kuna mataifa yatakuunga mkono huo ni utumwa wa kifikra katika siasa za Kiafrika. Marekani wenyewe waliwahi kufuta matokeo ya Jimbo zima la Texas sababu ya utata wa utoboaji wa karatasi za kupigia kura yaliyoelekea kumpa ushindi mmoja wa wagombea katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki.
Madai mengine ya kijinga ni ya uchaguzi kutokuwa shirikishi. Ushirikishi kwa wenzetu hawa ni kulazimisha wale walioamua kwa hiari yao kutoshiriki washiriki. leo hawaamini mtu kuamua kushiriki au kutoshiriki mchakato wa uchaguzi nayo ni Demokrasia. Na wanaoshangilia uamuzi huu wa MCC ni wale waliokuwa wakilalamika wasilazimishwe kushiriki kitu ambacho wao hawakitaki. sijui walitaka nchi ikae bila Rais kwa muda gani mpaka hapo wanaotaka kubembelezwa kushiriki wajisikie sasa wanataka kushiriki.
Suala la Cyber crime law ni la taratibu na sheria za kibunge zaidi, Serikali ilishatoa maelezo kama kuna mapungufu katika sheria ile mapendekezo ya marekebisho yanatakiwa kupitia katika taratibu za kawaida za kibunge. Sasa mtu utashangaa walitaka uchaguzi uahirishwe mpaka marekebisho hayo yafanyike? na yangefanywa na chombo gani hali kuwa muda wa wawakilishi wetu umeisha? Hivi tufikirie kana Watanzania mswada ule ungalikuwa haujapitishwa, uchaguzi wa 2015 ungalikuwaje ukizingatia uhuni na uchochezi uliokuwa ukifanywa kupitia mtandao? kama ilifikia waharifu wa mtandao kuaminisha kuwa sasa nchi haina mkuu wa majeshi ati amekufa, lengo lilikuwa nini? Ukizingatia na wageni walioletwa kusaidia baadhi ya vyama kitekinologia kujaribu kuharibu matokeo Ni lazima tukubali hii sheria imesaidia sana uchaguzi huu kuwa wa Amani kama si hivyo kungalitokea machafuko makubwa.