Inawezakana mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kuwa waziri wa kawaida?
Hebu nifahamisheni!
KAKA MASAKI ..KATIKA HISTORIA YA TANZANIA MAWAZIRI WAKUU WOTE WAMEWAHI KUWA MAWAZIRI WA KAWAIDA HATA BAADA YA KUWA MAWAZIRI WAKUU...EXCEPT SOKOINE..na malecela
1.RASHID MFAUME KAWAWA [amewahi kuwa makamu wa rais.,waziri mkuu ..waziri asiye na wizara maalum,waziri wa ulinzi ...waziri asiye na wizara maalum]
2.CLEOPA DAVID MSUYA[waziri wa biashara, waziri mkuu na makamu wa pili wa rais ,waziri wa fedha, waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais, na waziri wa biashara na masoko]
3.SALIM AHMED SALIM[waziri wa mambo ya nje,waziri mkuu na makamu wa pili wa rais,naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi..]
4.JOSEPH SINDE WARIOBA[mwanasheria mkuu,waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais,waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa]
5.CYGEMWISI JOHN SAMWEL MALECELA[WAIRI wa mambo ya nje,waziri wa mawasiliano na uchukuzi,mkuu wa mkoa iringa,balozi london,waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais,..nadhani after that akarudi chamani tu...
so sioni ajabu kwa FREDERICK TLUWAY SUMAYE kama rais atamteua kuwa mbunge na baadaye waziri na yeye akaukubali uteuzi ...kwani hatakuwa waziri mkuu wa kwanza wa nchi hii kuwa waziri baada ya kuwa waziri mkuu....sumaye ana rekodi ya kuwa waziri mkuu kwa muda mrefu zaidi na bado umri wake ni wa kadiri....kwa rais ambaye hatataka upinzni wa ndani lazima asicheze mbali na watu kama sumaye,mwandosya na kigoda.