Tuna mfumo wa ubaguzi wa sheria ambayo naona unapply kwa wakubwa na watu wadogo kitofauti!
Angalia hata leo Ditto aliua mtu na yupo na anafanya biashara kuuza asali na JK anaona kwa vile ni rafiki yake ni poa tu!
Nachoweza kusema.. Tz ukiiba kuku ni lazima utafungwa tu ndugu yangu!
Nakuunga mkono juu ya hoja yako kwamba TANZANIA KUNA MFUMO MATAPISHI WA UBAGUZI WA SHERIA UNAOWAPENDELEA VIONGOZI WA SISIEMU.
Watanzania tulipeleka ndugu zetu kupigana huko Afrika ya Kusini ili kupambana na mfumo wa Ubaguzi wa rangi chini ya Serikali ya Makaburu wa Afrika ya kusini.
Tumepoteza muda wetu,rasilimali zetu na uelekeo wetu wa kufikiri kwa sababu ya kupinga mfumo huo wa ubaguzi wa Rangi.
Ina maana tulifanya kazi bure???
Leo hii Chama cha SISIEMU chama chenye historia ya kupinga ubaguzi wa namna yeyote ile Afrika na kwingineko duniani kimekengeuka na kuikumbatia siasa matapishi ya Ubaguzi.
Sheria zetu zinatumika kwa namna tofauti kwa watu tofauti juu ya makosa ya namna moja.
MWizi ni mwizi.
Tendo la wizi likifanywa na Waziri ni wizi.
Tendo la wizi likifanywa na Askofu ni wizi
Tendo la wizi likifanywa na Mufti ni wizi.
Mkuu wa mkoa akiua ni kosa la jinai
Jambazi akiua ni kosa la jinai
Hata Rais akiua ni kosa la jinai( Japo katiba ya Sir Richard Turnbull inamlinda)
Mtuhumiwa wa wizi siku zote anashitakiwa chini ya sheria ya jinai na ni lazima afikishwe mahakamani kujibu mashitaka ya tuhuma za wizi.
Ni Mahakama pekee yake ndiyo yenye mamlaka ya kuamua mwizi huyu afanywe nini.
Rais wa nchi,Waziri,Mwanasheria mkuu au kiongozi yeyote ndani ya serikali hana mamlaka ya kuamua mwizi afanywe nini.
Zaidi hawana mamlaka ya kuamua kilichoibiwa kifanywe nini. Ni kinyume cha sheria mtu au kikundi au cha cha siasa kuchukua majukumu ya mahakama kwa kisingizio chochote kile.
Kitendo cha kuwaruhusu Viongozi wa serikali na watu wengine wajionao maarufu kurudisha fedha moja kwa moja mahali wanapotuhumiwa kuiba ni kinyume cha sheria zaidi ni UBAGUZI WA KISHERIA NCHINI TANZANIA.
Wezi wa kuku,mbuzi,ndoo,mikungu ya ndizi na mahindi mabichi na wezi wa mifukoni na wezi wengine wote wasio vingunge tunajua wazi kwamba kamwe serikali ya sisiemu haiwezi kuwapa starehe hiyo ya kurudisha fedha na kuendelea kutembea kifua mbele.
Kitendo hiki zaidi ya kuwa ni cha kibaguzi na kikaburu kinazusha maswali mengi
Je ni kweli fedha zinarejeshwa?
Kwa nini wezi hawa wa mabilioni hawashitakiwi?
Waziri mkuu kajihudhuru kwa wizi wa wazi je hii si dalili kwamba viongozi wakuu wote wa serikali wamo kwenye wizi wa EPA sasa wamejipa kinga ili wasichukuliwe hatua?
Tunajuaje fedha hizi si zile za makusanyo ya kawaida ya kodi ambazo serikali imeamua kuweka huko kwenye fuko la EPA ili kuhararisha wizi wa fedha za EPA?
Hivi leo nikichukua Tinga Tinga au TNT na kwenda kubomoa kuta zote za Gereza la ukonga ili niwaachie vibaka na wezi wa kuku kosa langu chini ya utekelezaji wa iana hii wa sheria litakuwa nini?
Ni kiasi gani cha chini ukiiba sheria ya wizi Tanzania inakubana ili wananchi wote tujihadhari kuiba fedha ndogo ndogo?
Kuna mtu au kundi la watu au chama nchini Tanzania ambacho kiko juu ya sheria?
Watanzania tuko wapi kupinga Ubaguzi huu wa sheria unaowapendelea Viongozi wa serikali wafanyao makosa ya jinai,tena hadharani?
Hivi Watanzania tunadhani kuna mtu atakuja kupigania haki zetu kwa niaba yetu?
SAA YA UKOMBOZI NI SASA NA WAKOMBOZI NI MIMI NA WEWE.