Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Kwanza naomba nianze na pongezi za dhati kabisa kutoka ndani ya moyo wangu, kwa Mtangazaji Doto Bulendu wa Star TV kwa kipindi chake cha "Jicho Letu Ndani ya Habari" kinachorushwa live kila Jumamosi saa 1:00-3:00. Japo Tanzania tunao watangazaji wengi wa medani za siasa, huyu ni mmoja wa watangazaji wachache mahiri kabisa katika medani za siasa!. Hongera sana Dotto Bulendu!.
Leo katika kipindi chake kumekuwa na mjadala mkali sana ulioanzia kwa tuhuma za baadhi ya headline kama "Rais Kikwete Anywea Kwa Ukawa!", mmoja wa wageni wake wawili akisema huo ni udhalilishaji, huku mgeni mwingine akisema iko ok, Doto Bulendu kama moderator, akamaliza uvutano kwa kuelemisha kuwa uandishi ina makosa mawili tuu,
1. Uchochezi (sedition) 2. Udhalilishaji (defamation) japo kiukweli kuna makosa mengi zaidi ya hayo, ila kwa hoja iliyopo mezani, ufafanuzi wa mtangazaji ulitosha kumaliza ubishi kuwa kama hakuna uchochezi, na hakuna udhalilishaji, then hakuna kosa lolote the headline is ok!.
Ukafuatia mjadala wa uwezo wa Bunge la Katiba kukusanya maoni na "Samuel Sitta kuelezwa kuwa ndie "muuaji wa Katiba Mpya!" hapa pia mzungumzaji mmoja alimtetea Sitta na mwingine alikubaliana na hoja ya "Sita ndie Muuaji wa Katiba Mpya!', hapa napo Mtangazaji Dotto Bulendu akamuokoa Sitta kiaina kwa kusema BMK lina wajumbe zaidi ya 600!, huwezi kumtishwa mzigo mtu mmoja tuu!.Pia alimpongeza Kubenea kufungua shauri mahakamani ya kuomba ufafanuzi wa Mahakama Kuu kuhusu uwezo wa BMK kuendelea kukusanya maoni.
Kiini cha uzi huu ni closing remarks za Mtangazaji Dotto Bulendu ambaye amechambua sheria iliyounda BMK haikutoa mamlaka yoyote kwa Bunge hilo kuendelea kukusanya maoni mapya na kubadili rasimu ya Warioba, bali bunge hili limejitungia kanuni na kujipa mamlaka hayo kinyume cha katiba ya JMT.
Akahitimisha kwa hoja ya akidi kuwa sheria Bunge la JMT, inasema 2/3 ya wajumbe wote wa BMK, lakini BMK likajitungia kanuni inayosema 2/3 ya wajumbe waliopo!. Mtangazaji amesisitiza kanuni hiyo inakwenda kinyume cha Ibara ya 98 ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977, na kumalizia kuwa bila UKAWA kurejea bungeni, hakuna akidi itakatotimia hivyo kinachoendelea kwa sasa bungeni Dodoma kwenye BMK, ni kutafuna tuu kwa fedha za Watanzania! na hakuna Katiba Mpya itakayopatikana!.
My take.
Nimeguswa sana na jinsi Mtangazaji huyu anavyojenga hoja based in taratibu, sheria na kanuni, watangazaji wa aina hii, ndio wanaohitajika zaidi kipindi hiki cha kuelekea mchakato wa katiba mpya, kisi kwamba nilijitamani enzi zangu za utangazaji "talk show" kama "Kiti Moto" zingerudi!.
Kwenye huu Mchakato wa Katiba, Watanzania, wanahitaji zaidi "Kuhabarishwa, Kuelimishwa na Kueleweshwa" ili utakapofikia muda wa kufanya maamuzi, wafanye "informed decisions!".
Jee Wangapi kati yetu tunaungana na Dotto Bulendu kuwa kinachoendelea Dodoma, "Hakuna Katiba!" bali ni kutafuna tuu fedha zetu?!, what do we do?!, tuzidi kuwaacha tuu waendelee kutafuna tuu fedha zetu au?!.
Wasalaam.
Pasco