Suluhu sina uhakika kama ipo kwa hali ya nchi yetu ndugu
Pasco, maana kwa nchi za wenzetu ambao wameweka uzalendo mbele na wanajua haki zao, hakuna chombo chochote kinachothubutu kwenda nje ya makubaliano. Wananchi wangeisha ingia mitaani na kugomea mchakato usiendelee. Ila kwetu sie tunaendelea kubaki kupigia kelele kwenye keyboard zetu ile za computer au simu.
Huwezi kupata katiba kwa kama hakuna maridhiano na wanaoona mbali walisema mapema hawa ndugu zetu wamepitisha sheria ya kutumia wabunge waliopo kwenye BMK kwa sababu wanaandaa mazingira ya kupindua ili mambo watakayoyataka wao kwa kwa masilahi yao ndio yashamiri. Tunawashukuru kwa kuendelea kuwaamsha watanzania maana wengi wetu bado tumelala na hata wengine ukitaka kuwaelimisha juu ya katiba watakuambia hayo mambo ni ya wanasiasa tuwaachie wao bila kujua katiba ni ya kwetu na sio ya wanasiasa.
Dodoma kwa sasa ni business as usual mwisho wa siku wajiandae kuja kujibu hoja ya kutafuta mabilioni yetu bila kutupatia katiba mpya. na wala wasije na hoja dhaifu kuwa waliokwamisha kupatikana kwa katiba ni wajumbe wa ukawa waliogomea mchakato, tutawacheka, kuwadharau, na labda tunaweza kutumia hyo kama fimbo kwenye uchaguzi mkuu ujao.