Kinachoendelea katika Mkutano wa 17 wa Bunge la 12, Kikao cha 8 Novemba 7, 2024 Asubuhi

Kinachoendelea katika Mkutano wa 17 wa Bunge la 12, Kikao cha 8 Novemba 7, 2024 Asubuhi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Bunge linaendelea hivi sasa kwa kipindi cha maswali na majibu ambapo wabunge wanapata fursa ya kuuliza maswali kwa mawaziri, huku mawaziri wakitoa ufafanuzi na majibu kwa maswali hayo. Endelea kuwa nasi kufuatilia yanayoendelea kutoka Dodoma, kwenye kikao ambacho kinahusu pia Kamati ya Mipango.

Wanywaji wa Bia wamepungu, hali yatishia kukua kwa Uchumi wa nchi​

Makusanyo ya mapato ya makampuni ya bia nchini yameshuka kwa karibu asilimia 20, hali inayoonekana kusababishwa na kupungua kwa wanywaji wa bia kufuatia ongezeko la ushuru wa bidhaa lililowekwa na serikali. Ongezeko hili la ushuru limewafanya wanywaji wengi kuhamia kwenye vinywaji mbadala ambavyo vinaweza kuwa na madhara makubwa kiafya.

Akizungumza bungeni leo, Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Philip Mwanyika ameeleza kuwa hali hii ina athari kubwa si tu kwa afya ya wananchi, bali pia kwa uchumi wa taifa.


View: https://www.youtube.com/watch?v=_U68-UVqEVk
 
Back
Top Bottom