Kinachoendelea Moshi, Hakuna Hali Ngumu

Tembosa

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,487
Reaction score
3,978
Wakuu, Amani iwe nanyi!!
Nimekuwepo Kilimanjaro kuanzia mwanzoni mwa Mwezi huu wa December.
Na bahati nzuri nimeyaona maisha ya kijamii kabisa ya wachagga...
Nchi yetu raia wanalalamika sana kuwa hali ni ngumu kila kona, lakini hawa jamaa wa huku sivyo kabisa, nilitegemea kuona mkwamo wa sherehe msimu huu

Lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa, wachagga bado wanafanya masherehe makubwa kabisa, Harusi nyingi zinafanywa kwa sherehe kubwa kubwa kabisa, ubarikio na ubatizo bado vinafanyika kwa masherehe.

Hawa watu wao wanapata wapi pesa za kufanya yote haya tena kipindi hiki! Ambapo kila mtu analalamika pesa haionekani?

Tuseme ndiyo Magu kashindwa kuwabana vizuri hadi wanaendelea na matumizi ya aina hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…