KERO Kinachofanya bandari kavu ya Kwala isitumike ni nini? Tunaomba maelezo

KERO Kinachofanya bandari kavu ya Kwala isitumike ni nini? Tunaomba maelezo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunamsihi Rais au Waziri Mkuu atuambie hatima ya Kwala Dry Port ni ipi.

Juzi tu kulikuwa na mjadala kuhusu mabasi kutokuingia mjini kwa lengo la kupunguza msongamano katikati ya jiji. Cha ajabu, sasa tunasikia taarifa kwamba Kata 10 za Wilaya ya Temeke zimetengwa kwa ajili ya shughuli za bandari, jambo ambalo linaweza kusababisha malori kuendelea kurundikana mjini na kuongeza msongamano.

Wananchi tumekuwa tukipiga kelele na kuomba shughuli za bandari zihamishiwe Kwala, lakini viongozi wanaonekana kama hawalioni hili na wamekaa kimya bila kujibu hoja za wananchi.

Soma Pia: Mbunge Shabiby: Kwanini Bandari Kavu ya Kwala haitumiki au kuna michezo ya rushwa inayoendelea nyuma ya Pazia?

Hivyo basi, tunaomba Rais, ambaye alizindua ile bandari kavu ya Kwala, atuambie kinachofanya Kwala isitumike ni nini?
 
Back
Top Bottom