Tunamsihi Rais au Waziri Mkuu atuambie hatima ya Kwala Dry Port ni ipi.
Juzi tu kulikuwa na mjadala kuhusu mabasi kutokuingia mjini kwa lengo la kupunguza msongamano katikati ya jiji. Cha ajabu, sasa tunasikia taarifa kwamba Kata 10 za Wilaya ya Temeke zimetengwa kwa ajili ya shughuli za bandari, jambo ambalo linaweza kusababisha malori kuendelea kurundikana mjini na kuongeza msongamano.
Wananchi tumekuwa tukipiga kelele na kuomba shughuli za bandari zihamishiwe Kwala, lakini viongozi wanaonekana kama hawalioni hili na wamekaa kimya bila kujibu hoja za wananchi.