Kinachofanyika kwenye kutekwa, kupotezwa au kuuawa bila kujulikana kwa watu popote ulimwenguni


Hapa mimi siongezi kitu ila naomba msome hizi aya kutoka kwenye maandiko matakatifu.

Yakobo 2:25 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

25 Hali kadhalika Rahabu, yule kahaba, yeye je, hakuhesabiwa haki kwa matendo yake alipowapokea wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine?

Yoshua 6:25 BHN
Lakini yule kahaba Rahabu pamoja na watu wote wa nyumba ya baba yake, Yoshua aliyaokoa maisha yao. Rahabu akaishi miongoni mwa Waisraeli hadi leo, kwa kuwa aliwaficha wajumbe ambao Yoshua aliwatuma kwenda kuupeleleza mji wa Yeriko.

Yoshua 2
Rahabu Na Wapelelezi

1Kisha Yoshua mwana wa Nuni kwa siri akatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Kwa hiyo wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba jina lake Rahabu na kukaa humo.
2Mfalme wa Yeriko akaambiwa, “Tazama! Baadhi ya Waisraeli wamekuja huku usiku huu kuipeleleza nchi.” 3Hivyo mfalme wa Yeriko akatuma huu ujumbe kwa Rahabu: “Watoe wale watu waliokujia na kuingia nyumbani mwako, kwa sababu wamekuja kuipeleleza nchi yote.”
4Lakini huyo mwanamke alikuwa amewachukua hao watu wawili na kuwaficha. Akasema, “Naam, watu hao walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka. 5Kulipoingia giza, wakati wa kufunga lango la mji, watu hao waliondoka. Sijui njia waliyoiendea. Wafuatilieni haraka. Huenda mkawapata.” 6(Lakini alikuwa amewapandisha darini akawafunika kwa mabua ya kitani aliyokuwa ameyatandika darini.) 7Basi hao watu wakaondoka kuwafuatilia hao wapelelezi katika njia ile inayoelekea vivuko vya Yordani, mara tu wafuatiliaji walipotoka nje, lango likafungwa.
8Kabla wale wapelelezi hawajalala, Rahabu akawaendea huko juu darini, 9akawaambia, “Ninajua kuwa BWANA amewapa nchi hii na hofu kuu imetuangukia kwa sababu yenu, kiasi kwamba wote waishio katika nchi hii wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yenu. 10Tumesikia jinsi BWANA alivyokausha maji ya Bahari ya Shamu kwa ajili yenu mlipotoka Misri, pia lile mlilowatendea Sihoni na Ogu, wafalme wawili wa Waamori mashariki ya Yordani, ambao mliwaangamiza kabisa. 11Tuliposikia juu ya hili, mioyo yetu iliyeyuka na kila mmoja alikosa ujasiri kwa sababu yenu, kwa maana BWANA Mungu wenu ni Mungu juu mbinguni na duniani chini. 12Sasa basi, tafadhali niapieni kwa BWANA, kwamba mtaitendea hisani jamaa ya baba yangu, kwa kuwa mimi nimewatendea hisani. Nipeni ishara ya uaminifu 13kwamba mtayahifadhi maisha ya baba yangu na mama yangu, ndugu zangu wa kiume na wa kike, pamoja na wale wote walio wa kwao na kwamba mtatuokoa na kifo.”
14Wale watu wakamhakikishia Rahabu, “Uhai wetu kwa uhai wenu! Ikiwa hutatoa habari ya nini tunachofanya, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutawatendea kwa hisani na kwa uaminifu.”
15Kisha akawatelemsha dirishani kwa kamba, kwa kuwa nyumba yake aliyokuwa anaishi ilikuwa sehemu ya ukuta wa mji. 16Alikuwa amewaambia, “Nendeni vilimani ili wale wafuatiliaji wasiwapate. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watakaporudi, hatimaye mwende zenu.”
17Wale watu wakamwambia, “Hiki kiapo ulichotuapisha hakitatufunga, 18isipokuwa, hapo tutakapoingia katika nchi hii, utakuwa umefunga hii kamba nyekundu dirishani pale ulipotutelemshia na kama utakuwa umewaleta baba yako na mama yako, ndugu zako na jamaa yako yote ndani ya nyumba yako. 19Ikiwa mtu ye yote atatoka nje ya nyumba yako akaenda mtaani, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe, hatutawajibika. Lakini yule ambaye atakuwa ndani pamoja nawe, kama mkono wa mtu ye yote ukiwa juu yake damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu. 20Lakini ikiwa utatoa habari ya shughuli yetu tunayofanya, tutakuwa tumefunguliwa kutoka kwenye kiapo hiki ulichotufanya tuape.”
21Naye akajibu, “Nimekubali. Na iwe kama mnavyosema.” Kwa hiyo akaagana nao, nao wakaondoka. Yeye akaifunga ile kamba nyekundu dirishani.
22Walipoondoka, wakaelekea vilimani na kukaa huko siku tatu, hadi wale waliokuwa wakiwafuatilia wakawa wamewatafuta njia nzima na kurudi pasipo kuwapata. 23Ndipo wale wapelelezi wawili wakaanza kurudi. Wakashuka kutoka kule vilimani, wakavuka mto na kuja kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kumweleza kila kitu kilichowatokea. 24Wakamwambia Yoshua, “Hakika BWANA ametupa nchi yote mikononi mwetu; watu wote wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yetu.”
 
Calabash pale Mwenge
La Chaaz Sinza
4 Wayz Kinondoni
Ukienda hizi bar, kila mtu anajitapa usalama.

Ukiona hivyo, pata picha kuwa KILA MTU POPTE PALE ALIPO, anapenda SANA kuwa salama, kwa maana kuwa anpenda SANA kuonekana kwa wengine kuwa ni mwema na pia, anayeweza kutegemewa na wengine kwa ajili ya usalama wao. Kwa hiyo ukikuta mtu alishakuwa au ni jambazi, ni nje ya matarajio yake, na hata yeye mwenyewe anakuwa hapendi kuwa jambazi ila analazimika. Kwa hiyo MUNGU alimuumba kila mmoja wetu ili awe mwema sana, na kila mmoja anapenda kuwa mwema sana, na ukikuta hayuko hivyo, basi ni nje ya matarjio yake!
 
Kabisa
 
Sasa ikitokea kwenye matukio kama hayo,ya watu wengine nje ya serikali kufanya utekaji,ama mauaji si ndio interegencia kwa maana ya usalama ndio wawe wameyafanyia kazi kabla kufikia huko?
 
Sawa mkuu. Umenipa funzo pia,kwamba tukio la utekaji au mauaji au namna nyingine yoyote mbaya inaweza ikawa ni maadui zetu kitaifa,kutoka hata nje ya nchi?. Labda wanaweza wakawa maadui wa kiuchumi hivi?. Kwa namna hiyo inatubidi tujiimarishe sana kiinteregencia. Maana kwa namna yoyote kwa kipindi tulichopo adui mkubwa anaweza kuwa ni wa kiuchumi. Mfano kenya na sisi kuhusu kugombea kuwahi nani awe na bandari yenye kina kirefu inayoweza kufikiwa na meli kubwa. Hii ni vita kubwa pia nafikiri. Japo sisi kama tuna nafasi. Ningefurahi sana kujengwa hii bandari kuliko kitu chochote kwanza. Tungeachana hata na ndege,tungewekeza nguvu kwenye ujenzi wa hii bandari ksbb hata mwananchi wa kawaida angeiona faida yake kwa haraka. Maana hii bandari ingeifanya jiji la Dar kuwa sawa na dubai ya Afrika mashariki na kati. Vile vile tungekamata Rwanda,Burundi,DRC,Malawi,Zambia,Uganda n.k upande wa mizigo yao kutoka nje,na mizigo yao kwenda nje
 
Huu ni upotoshaji wa kijinga kabisa,na ni urongo,undefinedtofautisha mambo ya mafia na mambo mengine, undefinedngoja waku-trace kama hujaimba haleluya kwa huu upotoshaji.
Lete ukweli wako kama huu upotoshaji~ kama huna kaa kimya usibweke ukaitwa Mbwa. USITISHE WATU.
 
Reconnaissence patrol. Hii iko jeshini ili kupata taarifa za adui kuwa ana silaha gani, jeshi lake likoje, mazingira yakoje, njia ya kuingilia n.k
 
Reconnaissence patrol. Hii iko jeshini ili kupata taarifa za adui kuwa ana silaha gani, jeshi lake likoje, mazingira yakoje, njia ya kuingilia n.k
Muhimu nilichotaka ukione hapa ni kwamba, kahaba Rahabu aliwadanganya maadui wa Jeshi la Joshua, ili kuwalinda akina Joshua. Huyu mtu aliyeanzisha thread hii kuna sehemu alisema kuwa wakati mwingine ni vizuri ukadawanganya rivals wako kwa maslahi mapana ya Nchi yako. Rahabu alifanya kitu ambacho kwa namna fulani kinafanana na hicho
 
Hi ishu ya kashogi ilisukwa vizur tu lakin kama zilivyofeli za kina ulimboka nayo ilifeli....walijaribu kuudangny ulimweng kuwa kashogi alitok salam ubalozini
 
Hi ishu ya kashogi ilisukwa vizur tu lakin kama zilivyofeli za kina ulimboka nayo ilifeli....walijaribu kuudangny ulimweng kuwa kashogi alitok salam ubalozini

Ingawa ilifeli lakini pia Mbs hakujali kama ni vigumu kuuwa mtu kwenye Ubalozi wake akijua fika ni hatari
Camera zinaonyesha akiingia ubalozini na mke wake mtarajiwa aliambiwa asubiri nje wakijua kuwa ndio mwisho wake huo
Anajiamini kwa USA kuwa hawezi kufanywa kitu
It’s so sad
 
Kuna vitu unavihisi labda inawezekana kutokana na hearsay..
Kuna mambo unayachanganya.
Anyway sio mbaya
 
Haya material ninayo miaka mingi sana, nimeamua kutoa darasa huru
mkuu utagunduaje watu hao walau kwa ishara tu ya nje ili uwe makini naye

na unawezaje kumkwepa ili usiingie kwenye target yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…