Kinachohitaji maandalizi usisubiri mpaka kiwe dharura

Kinachohitaji maandalizi usisubiri mpaka kiwe dharura

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
KINACHOHITAJI MAANDALIZI USISUBIRI MPAKA KIWE DHARURA.


Hili linatugharimu wengi kujikuta tunafanya dharura ambayo haikupaswa kuwa kama maandalizi yangefanyika vilivyo kabla.

Yapo mambo mengi ambayo tunayafanya kama DHARURA ilihali tulikuwa na muda wa kutosha kujiandaa kwayo na siku zote DHARURA huwa inaumiza kwa sababu inakuwa haina maandalizi tosherevu na hupoteza utulivu.

Kuoa/kuolewa mpaka sherehe ( harusi) sio dharura ni mipango inawekwa kufikia tukio hilo lakini wengi hapo ukiwaona utadhani kama wameshitukuzwa hivi kuanzia michango mpaka mambo mengine , tena kwenye michango hapo mpaka urafiki unaisha yaani muhusika analazimisha mumsaidie kama vile nyie ndio wahusika .


Kustaafu kazini sio dharura ila wengi tunafanya dharura ndio maana unakuta mtu ikibaki miaka mitano ndio unamkuta juu juu kutafuta biashara zipi afanye kumudu maisha ya blla mshahara na kwa sababu umefanya dharura kukosea kutakuwa kwa asilimia kubwa.

Kusomesha pia sio dharura ila ukiifanya dharura utaishi maisha magumu sana sababu ulikuwa na miaka ya kujiandaa kabla mtoto hajafikisha umri wa kwenda shule na ingefaa uwe tayari umejua uwezo wako ukoje kumudu shule ipi.


ACHA DHARURA IHUDUMIWE KAMA DHARURA ILA KINACHOTAKA MAANDALIZI USIGEUZE KIWE DHARURA

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako
 
Mkuu Mswahili haachi asili Kujiandaa kabla ya tukio huo mfumo wa kizungu.. Sisi waswahili. Tukio bila heka heka halinogi.. Ushawahi kuona mtoto wa kiswahili huko kayumba akiwa anaenda shule asubuhi!! Mama yake anamuandaa kama anaenda vitani...
 
Back
Top Bottom