Si mara moja wala mara mbili nimepata kusikia ubishi ni chuo gani bora kati ya Mzumbe University na UDSM! Hii wala si aina ya mada ambazo navutiwa nazo lakini nimelazimika kujitumbukiza baada ya kukutana na mtoto wa sister angu ambae anatarajia kujiunga SUA mwezi ujao! Kimsingi, she is not comfortable with SUA; nilipomuuliza ni kwanini akadai kwamba SUA si bora ukilinganisha na Mzumbe au UDSM! Yeye chaguo lake ni Mzumbe kwavile anaamini ndio chuo bora kwa hapa TZ! Yaani Mzumbe ni bora kuliko SUA au UDSM!
Tukiacha ushabiki (wa kwamba chuo ulichosoma ndio bora) pembeni, ubora wa Mzumbe hauufikii ule wa SUA achilia mbali UDSM! Ukweli ambao ni mchungu kuumeza ni kwamba SUA ni bora kuliko Mzumbe na UDSM ni bora kuliko SUA!
Najua siwezi pata shida kuwashawishi watu kwamba UDSM ni bora kuliko Mzumbe; lakini naweza hata kutupiwa mawe kujaribu kuwaambia wadau kwamba SUA ni bora kuliko Mzumbe! Kwavile ni ngumu kuwashawishi watu (sio wana JF pekee; bali hata wale walio nje ya JF) kuamini kwamba SUA ni bora kuliko Mzumbe lakini ni rahisi kuwashawishi watu kwamba UDSM ni bora kuliko Mzumbe; basi ni bora nikaijadili Mzumbe na SUA!
Awali ya yote ningependa ku-declare kwamba nami ni product ya SUA ingawaje sitarajii kuwa bias katika maoni yangu!
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya umaarufu na ubora! Hakuna ubishi kwamba Mzumbe ni maarufu mno kuliko SUA! Sababu za jambo hili nitalieleza baadae. Wakati SUA ipo within the circumference of Morogoro township(about 2.5 km from town centre); Mzumbe ipo some miles away from the township! Lakini pamoja na kwamba Mzumbe ipo mbali sana na mji kuliko SUA; lakini wakazi wengi wa Morogoro mjini wanaifahamu Mzumbe kuliko SUA! Ni umaarufu huu wa kutisha wa Mzumbe ndio unaofikia watu wazani kwamba Mzumbe ni bora(nazungumzia ubora wa elimu) pengine kuliko UDSM!!!
Kwanini naamini kwamba SUA ni bora kuliko Mzumbe!! Sina hakika ni vigezo gani muhimu vya kuzingatia katika kuangalia ni chuo gani bora ukilinganisha na vingine! Hata hivyo, vyovyote iwavyo, bado suala zima la wahadhiri (lecturers) wenye sifa linaweza kuwa ni moja ya vigezo muhimu. Pamoja na wahadhiri, kigezo kingine muhimu kinaweza kuwa facilities (mahabara-for versities with science subjects, lecture halls, libraries, books etc!)
Kabla sijaandika thread hii, nilianza kuzipitia prospectus za Mzumbe na SUA. Kitu nilichogundua, department nyingi za SUA, uwiano wa Wahadhiri wenye PhD na wale wenye Masters umepishana mno! What I mean ni kwamba wenye PhD(tena wengi wao ni Senior Lecturers-kwa maana kwamba wamechukua PhD hizo miaka kadhaa iliyopita na wana uzoefu wa kutosha) ni wengi mno, zaidi ya 80% ya wale wenye Masters! Si hivyo tu, wengi wao wamechukulia Masters na PhD zao ama UK au Australia na wachache German na USA!
Nilijaribu kutafakari uwepo wa idadi kubwa maradufu ya wahadhiri wenye PhD ukilinganisha na wale wenye Masters! Kwa mtizamo wangu, nimeona mambo mawili yamechangia SUA kuwa na PhD holders wengi. Kwanza, kuna kila dalili kwamba wale waliokuwa wanasoma shahada zao za kwanza (ambazo nyingi zake enzi hizo ni za Kilimo) walikuwa hawataki kufanya kazi zinazoendana na fani yao! Kama si hivyo, basi inawezekana kabisa hata hizo ajira zenyewe kwao kupata ilikuwa shida kwavile hatukuwa na kilimo cha ku-accomodate graduates! Kwahiyo si ajabu, wengi wao walikuwa wana-opt kurudi tena darasani na kuchukua Masters na PhD! Sababu nyingine ni kwamba, I guess wafadhili wengi walipendelea zaidi kuisaidia TZ kwenye suala zima la maendeleo ya kilimo, hivyo hii iliwapatia graduates wa SUA kupata scholarship kirahisi kwenda nje ya nchi kusoma!
Likewise, SUA wana some monopoly power kutokana na kuwa the sole agricultural university in TZ! Hivyo basi, msomi yeyote wa kilimo na forestry anaye-opt kuwa lecturer atakuwa hana option(otherwise, ata-enjoy limited option) zaidi ya kwenda SUA! Hii nayo ina-play kama comparative advantage kwa SUA kuweza kuhodhi idadi kubwa ya wasomi wa aina yake tofauti na wasomi wa fani zingine!
In contrast, Mzumbe hawana neema hii iliyopo SUA! Hata ukiangalia prospectus yao, wahadhiri wenye Masters ndio wengi zaidi kuliko wale wenye PhD!
Hili nalo halijatokea kwa bahati mbaya, bali ni la kihistoria! Mzumbe imekuwa University miaka michache tu iliyopita-about 20 years tangu SUA iwe full university! (SUA ilikuwa independent University on July 1984, lakini kabla ya hapo kilikuwa kinatoa university degrees kwa mgongo wa UDSM! c.f the former Muhimbili/UCLAS na UDSM or DUCE/MUCE na UDSM!) Kabla ya hapo Mzumbe ilikuwa ni Chuo cha uongozi! Kutokana na hilo, nature (aina) ya wanafunzi iliokuwa inadahili si wale ambao baadae wangeweza kuendeleza elimu yao na kuwa ma-lecturers! Wengi wao walitoka na maofisini na baada ya kuhitimu, walirejea makazini kuendelea na ajira zao. Hivyo, hawakuwa na sababu ya kuendelea kujitesa kwa kusoma elimu za juu (Masters+PhD) wakati walikuja pale kwa lengo tu la kung'arisha CV zao!
Hata baada ya kuwa university about 7 years ago, Mzumbe wamekosa monopoly power waliyokuwa nayo SUA kwakuwa nyingi ya programu zake zinapatikana kwenye vyuo vingine kama UDSM na IFM ambavyo vinafanana kwa umaarufu na Mzumbe. Na utitiri wa vyuo unaoibuka hivi sasa na kujizolea umaarufu tena pengine kuliko hiyo SUA unakuwa kikwazo kingine cha Mzumbe kupata wahadhiri wengi wenye sifa (PhD holders) kwavile wana option ya kwenda UDSM, UDOM, IFM, Tumaini, SAUT n.k!
Hivyo basi, utaona kwamba, kwa kigezo cha wahadhiri wenye sifa, Mzumbe inagalagazwa vibaya mno na SUA na UDSM! Yeyote atakayeacha ushabiki, bila shaka ataubaini ukweli huu in a second!
Kwa hapa sioni sababu ya kujadili suala la Maabara kwavile nature ya programmes za Mzumbe sio zile zinazohitaji maabara. Labda suala la tafiti(researches conducted)! Ingawaje sina defending points, bado sitapata shida kusema SUA wamefanya tafiti nyingi zaidi kuliko Mzumbe! Pamoja na mambo mengine, nature ya programmes za SUA zina-attract kufanya researces ( na research funds) zaidi kuliko zile za Mzumbe. Umri wa vyuo hivi nao unaweza kuwa hoja ya kuifanya SUA iwe imefanya tafiti nyingi kuliko Mzumbe!
Kwanini Mzumbe ni maarufu mno kuliko SUA?! Jibu lake ni jepesi mno! Program za asili pale Mzumbe ni za wapiga domo(Wanasiasa)! Wengi wao ni wale waliosomea masomo ya arts ambao kwa asili ni wapiga domo! Na ndio maana hadi leo hii endapo watu tutaulizwa ni wasomi gani wanatoka UDSM, basi wengi wetu tutawataja wale wanaotoka departments za History, Political Science na Law kwavile ndio pekee wanaopenda kuuza sura kwenye TV na vyombo vingine vya habari! Ni nani anaweza kututajia wasomi toka Faculty of Engineering ya UDSM? Kuna ma-PhD holders kibao lakini hawafahamiki! Ni nani anaweza kututajia wasomi wa Muhimbili University? Ni nani anaweza kututajia wasomi wa Ardhi University? Ni wa-TZ wangapi wanafahamu juu ya kuwepo kwa Muhimbili na Ardhi ya University? Nature ya taaluma zao si za kupiga domo! Leo hii Ikulu ikilipuliwa, Profesa Baregu au Profesa Xavery watakaa chonjo kusubiria mwaliko wa vyombo vya habari ili wahojiwe na wao kutoa maoni yao jambo ambalo halitatokea kwa ma-profesa wa ama SUA, Ardhi au Muhimbili!
Hivyo basi, kinachoibeba Mzumbe sio ubora wa chuo, bali ni umaarufu wake uliotokana na sababu nilizoainisha hapo juu!