Nilijaribu kutafakari uwepo wa idadi kubwa maradufu ya wahadhiri wenye PhD ukilinganisha na wale wenye Masters! Kwa mtizamo wangu, nimeona mambo mawili yamechangia SUA kuwa na PhD holders wengi. Kwanza, kuna kila dalili kwamba wale waliokuwa wanasoma shahada zao za kwanza (ambazo nyingi zake enzi hizo ni za Kilimo) walikuwa hawataki kufanya kazi zinazoendana na fani yao! Kama si hivyo, basi inawezekana kabisa hata hizo ajira zenyewe kwao kupata ilikuwa shida kwavile hatukuwa na kilimo cha ku-accomodate graduates! Kwahiyo si ajabu, wengi wao walikuwa wana-opt kurudi tena darasani na kuchukua Masters na PhD! Sababu nyingine ni kwamba, I guess wafadhili wengi walipendelea zaidi kuisaidia TZ kwenye suala zima la maendeleo ya kilimo, hivyo hii iliwapatia graduates wa SUA kupata scholarship kirahisi kwenda nje ya nchi kusoma!