Kinachoibeba Mzumbe university na kuonekana ni bora

mkuu samahani kutoka nje ya mada, nilitaka kufahamu ukimaliza kozi za agriculture engineering na irrigation and water resources engineering unapangiwa kazi na serikali au unatafuta mwenyewe?????

Nani akutafute?thubutuu,kuna course ya kutafutwa cku hz,huo udaktar mpaka uombe sio upo nyumban waje wakugongee..
 
Mbna mnahangaika kwa v2 vsvyo kuwa na maana,ukisha jua ni bora what for now,,Cku ynu ya kuzikwa 2tawazika na vyuo venu bora.from SOIL TO SOIL university
 
Kujituma ni suala binafsi kati ya mtu na mtu,mfano wafanyakazi wawili waliosoma UDSM mmoja akajituma na wa pili akawa hajitumi na ni kozi moja wamesoma.
 
NasDaz

Mkuu hapa pengine ungelinganisha vyuo vyenyewe kwa vyenyewe vinavyoshabiana kutokana na programmes zinazotolewa na vyuo kama starting point. Bahati mbaya SUA iko unique kuwa chuo pekee kinachotoa programmes zenye mwelekeo wa Kilimo na Mifugo ingawa imeanza kuingiza programmes unazoziita za kina "domo kaya. Kwa programmes ambazo ni "mpya" hapo SUA na zipo MZUMBE nadiriki kuungana na ndugu yako ni heri aende MZUMBE kwa vile wana uzoefu wa kufundisha programmes hizo kwa muda mrefu ukilinganisha na SUA. pamoja na kwamba MZUMBE huko nyuma ikianza ilikuwa inakodi baadhi ya walimu toka SUA kama SUA ilivyokuwa inakodi walimu to UDSM.


Mkuu sio kuhisi bali huo ndo ukweli wenyewe na nadiriki kusema kuwa miaka michache baada ya uhuru Kilimo na Mifugo ilikuwa na graduates hadi PhD wengi zaidi kuliko fani nyingine. Awamu ya kwanza ilikiinua Kilimo partly katika kuelimisha zaidi. Hata mishahara ilikuwa mikubwa - Graduate alikuwa anapata mshahara sawa na Diploma holder kutoka Bukalasa Uganda na Egerton College kenya ambayo sasa ni University. SUA ilikuwa ukiwa Tutorial Assistant ni lazima usome (scholarships zilikuwa kebekebe). scholaships kibao wizara ya Kilimo ilikuwa inapata toka kwa wafadhili mbalimbali.


Kweli kabisa


Sikubaliani na hili. Hawa unaowaita "domo kaya" wanajitokeza kusaidia kutukwamua kwenye sticky points katika kulifanya Taifa liende.
Nachelea kusema kuna wataalamu/wasomi wengi SUA lakini wana-SHY OUT kujitokeza hadharani kulisaidia Taifa katika kufuta njia za kulikwamua taifa hili katika masuala mbalimbali ya kijamii, uchumi na kilimo(mazao na mifugo) ambayo taifa linakabiliwa nalo - badala yake wanaachia wanasiasa wanatoa majibu yenye utata - sio kosa lao bali hawa wataalamu wetu wana soni au HAWAJIAMINI kutoa utatuzi wao kwa masuala ya kitaifa.

Farady alipogundua nishati ya umeme alimwalika waziri mkuu wa enzi hizo uingereza kwenye maonesho. waziri mkuu akamwambia na hii ni nini na ina faida gani kama sio kupoteezana wakati. Farady kwa unyenyekevu akamwambia waziri mku kuwa faida yake utakuja iona UTAKAVYOKUJA KUSANYA KODI NA NCHI KUJIPATIA MAPATO kwa uchache. Wataalam wetu wafanye hivyo wasiogope watakuwa labeled kuwa ni DOMO KAYA.
 
Halafu mnavokuwa mnalinganisha hivyo vyuo vyenu hebu kiweke UDSM pembeni kwa Tanzania na Afrika mashariki nzima hakuna kinachokifikia kwa ubora... kwa maana kwa utafiti wa mwaka 2013 kilikuwa chuo cha 4 Afrika kikizidiwa na vyuo vitatu vya south Africa tu..... Endeleeni na mjadala wako wa Mzumbe na Sua ukipenda ongeza Udom.....tena afadhali ungesema Kairuki ambacho afadhali kipo kwenye top twenty za Africa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…