SoC01 Kinachokwamisha Vijana Kufanikiwa

SoC01 Kinachokwamisha Vijana Kufanikiwa

Stories of Change - 2021 Competition

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
OIP.-9XornlgwNyQT1Igu_LaSAHaEK

Taswira kwa hisani ya Google

Utangulizi.
Vijana wengi (siyo wote) sehemu nyingi za dunia wako kwy mkwamo wa maisha pasina kujali wamesoma au la madhali wote wako kwy kundi la ujana. Vikwazo vinavyowakabili vijana wasipate maisha bora viko katika sura mbili, moja vikwazo vya kimfumo na pili ni vikwazo binafsi.

VIKWAZO VYA KIMFUMO.
Wahusika wa kundi hili ni Srkl & jamii kw ujumla ambao ndiyo wameweka mfumo unaowazuia vijana walio wengi wasipige hatua nzuri katika mchakato wa kusaka maisha bora. Aidha, pana mitazamo mi-2 kinzani ya vijana & watu wazima.

Srkl.
Sera nyingi za vijana duniani zinaandikwa, zinaratibiwa, zinarekebishwa na Srkl ikihusisha kundi dogo tu la vijana wanaoitwa wasomi huku kundi kubwa la vijana wasiosoma walioko vijijini & mijini wakiachwa nje ya mchakato na kusubiri kupewa ili watekeleze wasichokijuwa. Siku zote fursa zinamfuata mwenye maarifa ya kuwepo kwazo. Rais Kabila (hayati) alipotaka kuandika katiba ya DR Congo aliweka sharti kwmb lazima na lazima itaandikwe kw mawazo-jumuishi ya walio mijini & vijijini, wasomi & wasiosoma bila kujali kwmb katiba ni hati ya kisomi. Sambamba na hilo, Muungano wa Jamhuri za Wakulima wa Kisovieti USSR ilipoundwa, walihusishwa wakulima & wafanyakazi, wasomi & wasiosoma hadi wakapata taifa imara duniani USSR, hawakubaguana kw viwango vya elimu, ukwasi wala jiografia ya wanakoishi. Kw Tz hili limeshindikana ndiyo maana hata rasimu ya katiba ya Warioba ambayo kimsingi ndiyo ilitokana na mawazo ya wananchi wote maskini & matajiri, wasomi & wajinga, wa mijini & wa vijijini haikupita kikwazo cha Bunge Maalum la Katiba.

Jamii.
Jamii pana inawatazama vijana walio wengi kuwa ni kundi ambalo bado linahitaji kuongozwa tu kwmb halijawa tayari kuongozwa, hili nalo ni tatizo lililoweka mizizi kw kundi la wanawake kwmb jamii inawatazama hivyo km vijana pia kwmb hawawezi kuongoza. Huu ni upotofu mkubwa, kwanini, kw vigezo vya kihistoria Afrika tulikuwa na bado tunao hata leo vijana wadogo kabisa tena mahala pengine hata chini ya umri wa miaka 18 wanaongoza jamii zao. Abiy Ahmed (43) Waziri Mkuu & Amiri Jeshi Mkuu wa Ethiopia; Andry Rajoelina (45) Rais wa Madagascar; Mfalme Mswati III wa eSwatini (aliingia kazini akiwa na umri wa miaka 18 na siku 6 tu); David Cameron (44) Waziri Mkuu wa Uingereza alizaliwa 1966 aliingia ikulu 2010; Emmanuel Macron (40) Rais wa Ufaransa alizaliwa 1977 aliingia ikulu 2017.

Mtazamo wa Vijana kw Watu Wazima.

Vijana wanawatazama watu wazima km kikwazo cha wao kutorithi nafasi za uongozi, kutopata kazi za ajira, kutorithi mali za familia nk. Watu wazima wanawatazama vijana km rika la watu wenye pupa, wasio na hofu, wenye maamuzi ya gharama wasiyoweza kuimudu, wepesi kurubuniwa na maadui, wasio na uzalendo (wanaoweza kuhujumu nchi, jamii au familia zao kw dhamana za madaraka yao), wanaojijali peke yao, wasio na utu wala wasio tayari kuchukuliana mizigo na wenye uhitaji, kwmb ni watu ambao bado wanatakiwa kuendelea kukulia nafasi za dhamana chini ya uangalizi wa watu wazima. Vijana nao wana mtazamo wa majibu-ya-fadhila kw mtazamo huo wa watu wazima kwmb ni rika ambalo halina jipya, wamepitwa na wakati, wanaishi maisha ya analogia katika nyakati za digitali, maisha yao ni mechanical badala ya electronical. Bahati mbaya sana hakuna ajuaye km sera mbili za vijana na wazee zinatanzuaje migogoro hii ya kimitazamo baina ya makundi haya mawili.

Utekelezaji & Uratibu wa Usambazaji wa Elimu ya Sera ya Vijana.
Elimu juu ya sera ya vijana imesambazwa kw kiwango kidogo sana. Wengi hawajui sera yao inaongelea nini juu yao, inawaathirije kw matokeo chanya na hivyo kufanya agenda ya vijana kukwama. Sera ya vijana imefanyiwa marekebisho kadhaa lakini bado matunda ya utekelezaji wake hayajamfikia kijana wa jamii ya wafugaji kule chini porini achilia vijana wa mijini. Ili sera hii iweze kuwafikia wote na kuielewa kiufasaha ninashauri utengenezwe mtaala wa masomo ambao utafundisha sera ya vijana km somo kw ngazi ya sekondari hadi elimu ya juu na kw jinsi hii wengi watafikiwa na wataielewa kiufasaha na kuwa mabalozi wazuri wa kusambaza na kutekeleza elimu ya sera hii kw wale wataoikosa kwy ngazi hizo za elimu na ambao hawa watakuwa hawakufikiwa na Srkl katika zoezi la kutoa elimu ya sera yenyewe. Aidha, kw makusudi kabisa, Srkl iandae programu za masomo kw njia ya mitandao jamii kw sababu humo ndimo wamo vijana 99% wakiwemo wa jamii za wafugaji, lakini itakuwa rahisi kw Srkl kuwafikia vijana wengi kw sekunde moja tu ya kubofya kitufe cha kutuma ujumbe kwy simu za viganjani. Masomo yawe ni kw vielelezo 75% maana vijana hawapendi texts.

Mlundikano wa Sera.

Vijana wote duniani wanapitia furushi la sera mbalimbali ambazo hizo zinaacha athari kwb ambazo wanahama nazo kwenda kwy rika lingine. Mfano, duniani kuna sera za kitaifa & kimataifa katika sekta zote husika, pia kuna sera za watoto, vijana, wanawake, wazee na katika hizi vijana wa kike ni wahanga zaidi kw sababu wao ni wadau wa sera za wanawake & vijana achilia zile za watoto & wazee.

Sera za Vijana Duniani Hazina Uwezo wa Kudhibiti Matumizi Mabaya ya Vijana.
Km ilivyo kw ajira za watoto kushindikana kudhibitiwa na mifumo iliyopo ya sheria, miongozo, kanuni, mikataba ya kimataifa, maazimio & sera, vijana nao sera zao zimekosa uwezo wa kuzuia walanguzi wa vijana kuwachukuwa na kuwatumia kw maslahi yao kisha kuwaacha pasina kuwahakikishia hatima zao. Walanguzi hawa wamo wanasiasa wa wastani wanaotafuta washabiki, makundi ya wanamgambo na waasi, waajiri wa sekta za viwanda, migodi, ulinzi na nyumba za ibada nk.

VIKWAZO VYA KIBINAFSI.

  • Ni ukweli usiokanushika kwmb vijana wenyewe wana vikwazo wanavyojitengenezea wenyewe katika mchakato wa kutafuta maisha bora ambavyo hivyo vimewakwamisha asilani na hawana ubunifu wa kujitanzua wenyewe kwmb wanasubiri watanzuliwe na maarifa & nguvu za mifumo (sera) ambayo wao hawakushiriki kuitengeneza:-

  • Vijana wengi wamekwamishwa na ubinafsi na kutaka kukaa juu ya wenzao (umimi) apate yeye tu. Srkl imepiga kelele nyingi za vijana kukaa katika makundi ya ushirika lakini matokeo ya uhamasishaji huu ni madogo sana. Vijana wanathamini dhana ya vikundi pale tu wanapofanya shughuli za uhalifu (kifo cha wengi ni harusi). Mark wa FB wenzake walimkimbia. Falsafa ya Mkate (Bread Philosophy) ni Sote Tupate. Aliyebuni mkate alikuwa na roho ya ubinafsi (umimi), alikuja kupingwa na aliyebuni kanuni-ya-slesi (Slice Formula) ya kugawa mkate ambaye alikuwa na roho ya ukarimu (usisi). Mgunduzi wa mkate alikuwa Mbepari, mgunduzi wa slesi alikuwa Mjamaa. Awali mkate mmoja ulishibisha mtu mmoja na baadaye ikatengenezwa kanuni ya slesi ambapo mkate huo huo mmoja sasa unashibisha wengi.

  • Vijana wengi wamedharau umuhimu wa historia katika kupata mafanikio, fursa ambayo wangetumia kujuwa namna ya kuendeleza njia walizotumia wazee wao kufanikiwa. Rais wa SMZ Dkt. Mwinyi, Rais Karume (Mstf), Rais Uhuru, Rais Kabila (Mstf), Rais Kim Jong-Un wa KKZ wote hawakupuuza wala kutupilia mbali fursa, uwezo & umuhimu wa historia ya familia zao katika kushika madaraka ya nchi. Walitembea na historia vichwani mwao hadi wakatinga Ikulu. Historia inam-shepu mtu, inamuongoza dira ipi afuate, ndiyo maana husingeweza kuwakuta hao kwy pool, vijiwe, maskani, chimbo, ghetto badala ya shuleni, maktaba za umma, vikao vya chama nk, wala hukuwakuta wakivalia bendera nusu mlingoti, Tshirt za Bob akiwa na mmea kwy viganja vyake bali katika ujana wao walivalia mavazi ambayo leo wangeonekana ni washamba lakini wao walichagua kuvalia kiitifaki. Rais Kim Jong-Un alikuzwa kwy historia ya ukoo wake katika kupata mafanikio. Alipata urais toka kw babake rais Kim Jong-Il ambaye naye huyu babake alipata urais toka kw babake rais Kim Il-Sung (yaani babu wa Kim Jong-Un). Kim Jong-Il alimvalisha mwanaye Kim Jong-Un mavazi ya cheo cha Jenerali wa Jeshi akiwa na umri wa miaka 8 tu na kuamuru akague gwaride la heshima na kupigiwa saluti, zaidi akampa pasipoti ya Uchina (kuzichanganya CIA & FBI) ili akasomee taaluma ya juu ya kijeshi ughaibuni. Leo ndiye rais wa KKZ. Vijana wengi hawataki historia! Hawajui hata wazazi wao walipataje ukwasi, walisomaje, wamepitia changamoto zipi nk.

  • Vijana walio wengi wanaishi leo (hawajui wanatakiwa waishi leo & kesho ili waendeleze vizazi dunia isibaki patupu), tofauti na wazee wa leo ambao wao enzi za ujana wao waliishi kipindi hicho na kipindi kilichofuata ambacho ndicho hiki.

Durusu za Rejea za Mwandishi wa Makala Hii Toka Kwy Vitabu Vyake:
“Revitalization of disgruntled workforce can never ever be achieved by improved remuneration package as Western life taste which has aggravated national culture, has misled the workforce to believe that only and only illegal earnings are the ones with ability to change lives in a positive way [extravagance] and the opposite is true for statutory earnings thus, even if salaries are revised to reflect on the real costs of living, still they believe it won’t have positive impact in the standards of living they want to reflect on globalization which is driven by stiff competition for wealth accumulation. Majwala D.O, (2015)”

“Mfumo mpya wa dunia umeleta matamanio ya ladha ya maisha ya kimagharibi (ambako tayari kuna maporomoko makubwa ya kutisha ya kiimani & kimaadili) ambayo yamevamia mataifa machanga kw kasi kubwa ya kushinda kasi ya udhibiti wake ambapo watu katika jamii za nchi zilizoathirika wametumbukia na kuzama kabisa katika ufisadi kw kutumia vibaya nafasi na dhamana zao ndani ya jamii zao kupotosha haki na kujipatia mapato ya aibu (haramu) kw nia ya kugharamia msukumo mkali unaowaka ndani yao wa matamanio (lust) ya ladha ya maisha hayo ya kimagharibi. Majwala D.O, (2017)”

Naomba kura.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom