Kinachomuondoa Didier Gomez Da Rosa ni Mshahara mkubwa, siyo kipigo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Huyu ni miongoni mwa makocha wanaolipwa hela nyingi, si kocha wa bei rahisi, halipwi kama Kishingo. Ni kocha wa mshahara kama wa Uchebe.

Ikumbukwe kwamba MO halipi mshahara wa kocha wa Simba kutoka mfukoni mwake kama wengi wanavyodhani , alilipa kutokana na fungu ambalo Simba walikuwa wanapata kutoka kwenye michuano ya Club bingwa ya CAF, ukishindwa kuqualify kwenye makundi basi unafungashiwa virago, maana hela ya kukulipa iko kwenye hayo hayo makundi, hivi ndivyo alivyoondolewa Uchebe, baada ya kuondolewa kwenye mashindano kwa kushindwa kuingia kwenye makundi ikawa ngumu kuwa naye kwa vile hakuna wa kumlipa. Zile porojo zingine ulikuwa uzushi tu

Kuna mtu kutoka ndani ya bodi ya Simba alishanitonya kitambo kwamba ili Gomez aendelee kubaki ni lazima aendelee kuwemo kwenye makundi ya ligi ya mabingwa, maana ni kocha anayelipwa hela nyingi na MO hana uwezo wala moyo wa kutumia hela kutoka mfukoni mwake kulipa mshahara.

Itaendelea ...
 
Da Rosa kuondolewa ilikuwa ni suala la muda tu, kwanza hana cheti kinachotakiwa na CAF ili akae kwenye benchi la ufundi, hivyo Simba imeingia gharama kumuongeza kocha mwingine amnaye anakuja kufanya majukumu ya Gomes.

Kuwalipa wawili mshahara kwa kazi ambayo ingetakiwa kufanywa na mmoja nilijua siku za Gomes Simba zinahesabika, naamini alikuwa anatafutiwa sababu tu, na sababu yenyewe ndio imepatikana jana.

NB. Tarehe 27, saa moja usiku, vs Polisi Tanzania, waamke mapema isijekuwa lawama juu ya lawama.
 
Huyu ni miongoni mwa makocha wanaolipwa hela nyingi, si kocha wa bei rahisi, halipwi kama Kishingo. Ni kocha wa mshahara kama wa Uchebe.

Ikumbukwe kwamba MO halipi mshahara wa kocha wa Simba kutoka mfukoni mwake kama wengi wanavyodhani , alilipa kutokana na fungu ambalo Simba walikuwa wanapata kutoka kwenye michuano ya Club bingwa ya CAF, ukishindwa kuqualify kwenye makundi basi unafungashiwa virago, maana hela ya kukulipa iko kwenye hayo hayo makundi, hivi ndivyo alivyoondolewa Uchebe, baada ya kuondolewa kwenye mashindano kwa kushindwa kuingia kwenye makundi ikawa ngumu kuwa naye kwa vile hakuna wa kumlipa. Zile porojo zingine ulikuwa uzushi tu

Kuna mtu kutoka ndani ya bodi ya Simba alishanitonya kitambo kwamba ili Gomez aendelee kubaki ni lazima aendelee kuwemo kwenye makundi ya ligi ya mabingwa, maana ni kocha anayelipwa hela nyingi na MO hana uwezo wala moyo wa kutumia hela kutoka mfukoni mwake kulipa mshahara.

Itaendelea ...
Tuambie analipwa kiasi gani?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
🙌🙌🙌

IMG-20211025-WA0099.jpg
 
Back
Top Bottom