Kinachoniuma mimi Mwananchi ni jasho langu kuwatajirisha wanasiasa

Kinachoniuma mimi Mwananchi ni jasho langu kuwatajirisha wanasiasa

Kinachoniuma mimi ni hela za jasho langu ndizo zinazowapa utajiri wanasiasa.

Yaani mavazi ya raisi, safari za nje za raisi, magari ya wabunge na mishahara ya wabunge vyote ni jasho la wananchi.

Lakini kama hiyo haitoshi, tumeongezewa kodi na tozo nyingine ambazo nazo zitaliwa na wanasiasa.

Wanasiasa hamuoni aibu kula jasho la wananchi masikini?

Magufuli alijua sisi ni masikini na ndio maana alipunguza tozo na kutumia rasilimali za taifa kupata hela.

Kwanini mnaogopa kutumia rasilimali zetu kupata hela?

Yaani misaada yote inayokuja nchini hakuna hata mmoja unaoenda kulipa mishahara mikubwa ya wanasiasa, gharama zote hizo za mishahara ya wabunge zaidi ya 270 inalipwa na kodi za wananchi.

Bado hamtosheki mnaona hamjatukamua vizuri.

Kama una kula hela ya mwananchi kuwa na ujasiri wa kupambana na makampuni makubwa yanayotunyonya kwenye mikataba ya madini.

Uoga wa viongozi wetu ni hatari kwa usalama wa taifa letu.

Mtaondolewa madarakani kwa mapinduzi, kila uvumilivu una kikomo chake.

Na mkome kabisa, CCM ya kijani hadi bungeni[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Pole Sana ndugu ndo Mana hawataki katiba mpya hawataki kuwajibika kwa Wananchi.Juwa mcumilivu kufkia 2025 Nchi hii itakua nzur Sana kwa Sababu tutakua tumepata katiba mpya na tutakua viongozi wenye maono makubwa .
muda ukipotea haurudi, siku moja lina saa 24, mwaka mmoja una karibu siku 366, miaka 4 ina siku 1460, ambazo ni saa 35040. Kuvumilia muda wote huu tutakufa kwa ugonjwa wa moyo. Kabla ya 2025 nitakufa na mtu.
 
waziri anasema hela za tozo zimeelekezwa kwenye vituo vya afya na elimu, jana benki ya dunia imetoa mkopo wa zaidi ya trilioni 1 kwa ajili ya elimu na afya, muda wa kutoana roho umekaribia.
AM1hnY.jpg
 
Back
Top Bottom