KInachoponza Simba ni rangi nyekundu, isiyo ya kizalendo

Mleta uzi umetema nondo tupu, huu ni ukweli usiopingika.
Wasipobadili rangi, hakyanani hawatachukua ubingwa wowote kamwe.
Rangi hii nyekundu ni kinyume kabisa na serikali ya Tanzania, maana hata Air Tanzania hawaitaki kabisa kwenye ndege zake, CCM hawataki kusikia, passport hawataki kuniona, NIDA hawaitaki kabisaaaaaa, leseni za magari hawataki kuisikia, nhif ndiyo kabisaaaaaa.
 
Wewe ni muathirika wa elimu mbovu na propaganda uchwara inayotolewa na CCM na umeathirika kweli kweli.

Hatukupingi ila tunakuonea huruma. Zinduka, bado haujachelewa.
 
Kuna siku nilipata bahati mbaya ya kuangalia Bongo muvi kwenye basi! Nikaona mganga wa kienyeji amevaa shuka jekundu!!
Exactly!!! Hakuna mganga bila kitambaa chekundu Na kaniki. Hakuna shetani bila rangi nyekundu, hakuna freemason bila rangi nyekundu.
 
Kuna kitu kinaitwa bahati. Kuna wakati mchezo unaamuliwa na bahati. Kuna siku magoli yote yote yanakula nguzo TU.
 
Wakivaa rangi nyeupe Yanga itafungwa au watatoa sare.
 
Hizo ni propaganda zisizo na mashiko,kwa hiyo kipindi wanachukua makombe ya ligi ilikuwa wanavaa jezi gani?

Al ahly wanavaa jezi nyekundu mbona wana mafanikio makubwa

NB.RANGI YA JEZI SIYO ISHU KIKUBWA NI MIKAKATI YA TIMU,UENDESHAJI NA UWEKEZAJI.
Walichukua makombe kwakuwa Yanga walikuwa na timu mbovu sana na kukosa mdhamini. Na TFF ilikuwa upande wao baada ya kuondoka Malinzi. Alahly wanatumia pesa na mbinu chafu.
 
Ndilo tatizo la kufugwa na dada yako. Umeshiba kiporo cha makande ya shemeji yako unakuja kucheua mbele ya wanaume humu jf.Takataka kabisaaaa!
 
Duh.. Hii kali kuliko..😂😂😂😂
 
Walichukua makombe kwakuwa Yanga walikuwa na timu mbovu sana na kukosa mdhamini. Na TFF ilikuwa upande wao baada ya kuondoka Malinzi. Alahly wanatumia pesa na mbinu chafu.
Kwahiyo tutegemee YANGA wakileta kombe la KLABU BINGWA?
 
Kwahiyo tutegemee YANGA wakileta kombe la KLABU BINGWA?

Kwahiyo tutegemee YANGA wakileta kombe la KLABU BINGWA?
Yanga ikiendelea hivi itakuwa ya kwanza kucheza finali za kilabu bingwa Inshallah. Rangi zake zinavutia taasisi nyingi ndani na nje ya nchi. Ni rangi za kiiungwana; humble kiasi kwamba kila Taasisi haioni shida kushirikiana nayo. Hata serikali yetu imekwepa sana rangi nyekundu kwenye huduma zake. Hata Bank zinazotumia rangi nyekundu kama NBC zinahangaika sana sokoni kuliko banks zenye rangi nyingine kama NMB, CRDB, Stanbic, etc. Simba kwavyovyote vile lazima itembelee nyota ya Yanga kwa nja ya checks and balance (kulwa na doto) vinginevyo huenda usingeliona goli la mama au serikali kutoa ndege kwa klabu. Lakini huwezi kutoa ngege kwa Yanga na kuacha kuipa Simba. Serikali imeiacha rangi nyekundu itumike sehemu hatari kama zimamoto, FFU au jeshini kidogooo sana kwenye parade na vikosi hatarihatari tu.

Nadhani historically Simba ilianzishwa na watu ambao hawakuitakia mema Tanganyika na harakati zake za kudai Uhuru ili kuondokana na fedheha ya kutawaliwa na weupe. Historia kama hii bado inatembea kwenye mishipa ya damu ya watanzania wazalendo. Nimefurahi kuona simba sasa hivi wanavaa jezi za rangi nyingine kama blue, zambarau mbali na zile za kikoloni za nyekundu na nyeupe; ni heri waendelee na mwelekeo huu. Ukimwangalia usoni mtu kama Waziri mkuu utagundua kuwa hayuko comfortable kuvaa raqngi nyekundu japo yeye ni mshabiki wa timu hiyo.
 
Hakuna Timu duniani iliyoizidi Al Ahly kwa makombe inashikililia rekodi hiyo hiyo ya Dunia licha ya kutumia jezi hiyo hiyo nyekundu
unadhani kwanini wanabeba mapipa ya kwenye ndege? Timu gani kubwa inafanya hivyo? Al-Ahly ni timu ya kishirikina, faraki na fitina nyingi michezoni
 
Ndilo tatizo la kufugwa na dada yako. Umeshiba kiporo cha makande ya shemeji yako unakuja kucheua mbele ya wanaume humu jf.Takataka kabisaaaa!
Sifa kubwa ya Simba ni uchawi, wanaroga sana sawa na unavyoziona timu za Uarabuni kama Misri. Afrika nzima inajua kuwa simba wanahusudu uchawi na kuamini kwenye uchawi. Ilizoeleka kuwa uchawi wa simba una uhusiano na mvua; mvua ikinyesha siku ya mehi ni simba inashinda mpaka ikazoeleka hivyo. Kiongozi wa Simba lazima na uhusiano na wachawi wakubwa na atachaguliwa kwa sifa hiyo. Walienda kuroga katikati ya uwanja kule South Afrika, Al-Ahly inakuja na mapipa yao kuogopa uchawi wa simba, timu zinapita milango isiyotakiwa kuogopa uchawi wa simba, timu zinakataa kuingia vyumba vya kubadilishia nguo kwasababu ya uchawi wa Simba, viwanja vinaharibika kwasababu simba wanafukia uchawi uwanjani. Juzijuzi waliroga hadi Kapombe mtoto wa watu akaanguka kiwanjani kabla ya mechi, juzi kabisa wameroga hadi wapinzani wao JKT Tanzania wakapata ajali mbaya sana.

Kwanini mambo haya hayasemwi kwa uwazi?
 
unadhani kwanini wanabeba mapipa ya kwenye ndege? Timu gani kubwa inafanya hivyo? Al-Ahly ni timu ya kishirikina, faraki na fitina nyingi michezoni
Gharama ya timu kama Real Madrid kucheza mechi moja ya kombe la dunia level ya club ni sawa na thamani ya kombe lenyewe,, unahisi kwenye kusafiri kwao wanabeba jezi tu?? Timu husafiri ni kila kitu chao na huwezi kuipangia nini cha kubeba na kama ushirikina ungekuwepo kwenye football timu zisingeshukq daraja, kwa hiyo mpira utabaki kuwa jambo la wazi
 
umeyasikia ya Simba tu au kisa timu zingine hujawahi kusikia? nikikuambia Aston Villa, Chelsea na Wolves walishawahi kupata mashtaka ya namna hiyo, Utakubali?
 
Zima bange bro, wazee wakazi hao!
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Mipang'ang'a SC.
4. Malalamiko (Lialia) SC.
5. Makelele SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyaunyau (mapaka) SC.
8. Mwakarobo SC.
9. Mikia SC.
10. Miso Misonda SC.
11. Manyang'au SC.
12. Mazumbukuku SC.
13. Mazombi SC.
14. Kinyume nyume SC.
15. Ngada SC.
16. Kolowizard SC
17. Zuwena SC.
18. Bebwabebwa (Mbeleko) SC.
19. Panya roads SC.
20. Kikanuni SC.
21. Kufa Kiume SC
22. Ubaya ubwege SC.
23. 5imba SC.
24. Visingizio SC (Visababu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…