Kuna mahala nimesikia kuwa mlevi huyumba yumba kwa kuwa kasi ya mzunguko wa damu yake huwa kubwa. Hii ni kwa sababu pombe hiyo husababisha mabadiliko hayo
Je, ni kweli kuwa hali ya mlevi kuyumba yumba husababishwa na ongezeko la kasi ya msukumo wa damu? Na sio pombe kuathiri mishipa ya fahamu?
Je, ni kweli kuwa hali ya mlevi kuyumba yumba husababishwa na ongezeko la kasi ya msukumo wa damu? Na sio pombe kuathiri mishipa ya fahamu?
- Tunachokijua
- Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), pombe huathiri saikolojia na kuzalisha tabia za utegemezi. Ni kinywaji kinachotajwa na fasihi za kale kuwa kimeanza kutumika tangu zamani sana.
Hutengenezwa kwa kusindika aina fulani za fangasi, sukari au aina fulani ya wanga unaojulikana kama Starch.
Unywaji wa pombe uliopindukia husabisha zaidi ya magonjwa 200 mwilini, lakini inapotumika kwa kiasi kidogo huhusishwa na kupunguza nafasi ya kuugua magonjwa ya moyo, kiharusi na kisukari.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Mayoclinic, unywaji mdogo wa pombe hutambulika kama;
- Mililita 350 za bia kwa wanawake na mililita 700 kwa wanaume.
- Mililita 148 za divai kwa wanawake na mililita 296 kwa wanaume.
- Mililita 44 za spirit kwa wanawake na mililita 88 kwa wanaume.
Kuongezeka kwa msukumo wa damu ndio sababu ya kuyumba kwa mlevi wa pombe?
JamiiForums imefuatilia madai haya kutoka vyanzo mbalimbali pamoja na kuzungumza na wataalam kadhaa wa afya.
Katika ufuatiliaji huu tumebaini mambo yafuatayo;
- Sio kweli kuwa kuyumba kwa mlevi husababishwa na ongezeko la msukumo wa damu kama mtoa hoja anavyodai.
- Kwa mujibu wa Taasisi ya Vestibular Disorders Association, pombe huharibu uwiano na ujazo wa vimiminika vinavyopatikana kwenye sikio la kati hivyo kumfanya mlevi ayumbe.
- Sehemu ya ubongo inayohusika na kutunza usawa wa mwili na mijongeo ya misuli hasa sehemu ya mikono na miguu maarufu kama cerebellum hupoteza udhibiti wa kazi hiyo hivyo kumfanya mtu atembee kwa kuyumba.
Hivyo, kwa kuzingatia rejea hizi, madai ya mlevi wa pombe kuyumba kwa sababu ya kuongezeka kwa msukumo wa damu yanathibitika kuwa ni uzushi usio na hoja zilizojengwa kwenye taarifa sahihi za kisayansi.