Kinachotakiwa Tanzania: Judges and Magistrates Vetting Board (JMVB)

WildCard

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2008
Posts
7,505
Reaction score
2,416
Nia ya kuanzisha chombo hiki ni kurudisha matumaini kwenye chombo hiki muhimu cha DOLA cha utoaji wa HAKI. Tumeshuhudia hukumu nyingi za hovyo, zenye utata mwingi, zenye kuacha maswali mengi huku zikigharimu fedha nyingi za walipakodi wa nchi hii. Tumeshuhudia pia ucheleweshwaji wa kesi nyingi. Rushwa imekivuruga chombo hiki kwa muda mrefu. Mahakama pia imetumika vibaya na watawala wetu. Teuzi za Majaji pia zimekuwa za utata mara kwa mara.

Tusisubiri Katiba Mpya. Hili linaweza kufanyika kwa ACT ya Bunge tu. Kesi ya Lema imetufumbua macho wengi.
 
What a great point! Juzi na jana (kwenye nyuzi nyingine) nilisema na ninarudia tena: KUNA TATIZO KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA; period.

Inaonekana hawa "junior" judges wako highly incompetent ukiongeza na rushwa na "UBABE WA KISIASA" mambo yanakuwa even worse. Haiwezekani kesi nyingi zinazoamuliwa na Mahakama Kuu zikienda Rufaa zinatupiliwa mbali kiasi hiki - hakika tuhuma za Mh. Tundu Lissu zinazidi kuthibitika regardless wanaombeza na kumkejeli.

Chukulia mfano mdogo tu wa shauri lililoamuliwa jana na Mahakama ya Rufaa iliyotupilia mbali hukumu ya Mahama Kuu juu ya ubunge wa Arusha - 2010. Kilichotengua hukumu ni kitu kidogo sana "locus standi"; kama "jaji" mzima wa Mahama Kuu hajui "locus standi" basi kuna tatizo tena kubwa kuliko inavyoweza kuelezwa na tatizo lenyewe linaanzia tangu huko kwa Mamlaka za Uteuzi wa Majaji. Nakuunga mkono 100%.

Enzi za Mwalimu ukikatiwa hukumu na Hakimu Mkazi itasimama hivyo hivyo hadi Mahakama ya Rufaa sana sana jopo la majaji saba likongozwa na Jaji Mkuu (full bench) litaona vijikasoro vidogo vidogo sana ambavyo haviwezi kuathiri mwenendo wa shauri zima hivyo watakachofanya ni KUIKAZIA hukumu.

Je, Wah. Mahakimu wetu wa enzi zile walikuwa competent kuliko baadhi ya Majaji wetu wa Mahakama Kuu wa enzi hizi? Sijui! Ninachojua kuna tatizo ambalo linahitaji kutatuliwa kwa haraka. Hiki chombo cha utoaji haki sio cha kufanyia mzaha au majaribio kiasi hicho.
 
Watu wengi Tanzania wanadhani tutaondoka kwenye huu uozo tuliomo kwa kuiondoa CCM madarakani. Hili sio kweli sana. Muhimu ni kuunda TAASISI imara ili tuwaondoe watu wenye nguvu kwenye vyombo vya maamuzi. Mfumo mzima wa mahakama unahitaji kufumuliwa na kusukwa upya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…