Kinachotukwamisha kama taifa kusonga mbele

Kinachotukwamisha kama taifa kusonga mbele

Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2012
Posts
2,438
Reaction score
6,313
Kwa Miongo kadhaa Tanzania kama nchi inayojitegemea, inapiga hatua kwa mwendo wa kobe.

Kuna mambo ukiangalia ni aibu sana, yani mpaka leo hii tunahangaika na mashimo ya choo, madawati, na vitu vingine ambavyo ni aibu hata kuvitaja.

Kama Taifa naona tuna changamoto hizi kubwa:

1. Ufisadi
2. Rushwa
3. Namba 1 na 2 zinazalisha uvujaji wa kodi na mapato.

Tanzania sio ya kukusanya Trillion 2 mbili kwa mwezi, kuna chenga nyingi, kuna wizi mwingi, kuna rushwa nyingi, na hizi zote zinapelekea ukusanyaji hafifu wa mapato ya serikali.

Tanzania hii kodi zikikusanywa vizuri kwa East Africa tunapiku nchi zote.

Nieleweke ninaposema zikikusanywa vizuri simaanishi wakamue watu kwenye tozo la hasha, hapa nazungumzia zile zinakwepwa.

Wanaosumbuliwa na kodi ni wafanyabiashara wadogo, wafanya biashara wakubwa wanapeta tu, kodi ya milioni 400 inakwepwa kwa ofisa kupewa rushwa ya million 10 tu, zigo mtaangushiwa nyinyi wa chini.

Mbaya zaidi wanaotakiwa kusimamia hizi sera ndio hao hao panya wa mezani nao wanakula na kusaza.

Yote haya yanachangia kuzorota kwa maendeleo ya taifa kwa nyanja zote kama uchumi, elimu, afya, miundo mbinu nk.

Nini kifanyike?
Kiuhalisia cha kufanyika hamna maana hata akija mtu msafi mmoja atakumbana na wachafu 1000, sasa 1 vs 1000 hapo moja lazima ishindwe mana itapigwa vita vibaya mno.

Kuna baadhi ya taasisi kama wewe ni mcha Mungu, mtu msafi, huwezi kudumu ni aidha utahamishwa kazini au duniani.

Wizi na ufisadi upo ngazi zote za juu mpaka kwenye shina kule, hata wewe unaeandika risiti feki ya tax ambayo hujapanda ili ukarejeshewe pesa ofisini kwako bado upo kwenye mjumuisho huu.

Hitimisho
Tanzania ni taifa lenye uwezo mkubwa kiuchumi, ila uwezo wa waendeshaji wa taifa umejikita kwenye wizi na ubinafsi.

Nakubaliana na wazungu tuna IQ ndogo, zingalikua kubwa tungetumia fursa na uwezo wetu kupiga hatua 10 zaidi, ila kwakua tunataka kuiba iba basi ngoja tubaki kusindikiza dunia.

Facts check
Leo ukimwangalia mbunge awe ndugu yako au mtu yeyote yule, jicho unalomwangalia nalo sio lile la kibunge la uwakilishi wa wananchi bali utaona ni mtu aliepatia maisha anapiga pesa tu, sasa hili jicho hata yeye mbunge huliona hivyohivyo wakati anagombea kiti, sio kwamba ana uchungu na wananchi ila ni fursa kubwa kiuchumi kwake, biashara zake na familia yake, hivyohivyo kwa mawaziri, na wengineo.

Taifa la wezi.
 
Mimi naona njia pekee ni kuiondoa tu CCM madarakani kwa njia yoyote ile. Kiukweli hawa jamaa hawajawahi kuwa na mapenzi na nchi yetu! Isipokuwa wao wenyewe, watoto wao, marafiki zao, vimada wao, na chama chao.
 
Hakuna cha katiba mpya , hii nchi ni kubwa mno zinatakiwa zitoke nchi kumi humu , mambo yataenda Sawa , bila hvyo hamna kitu, hata ukiiondoa CCM , utamweka Nani , ?? Wapinzani hawa hawa ambao hawaaminiki Kwa wananchi, labda waje wapinzan wengine , mbaya zaidi huwez tofautisha CCM na vyombo vya dola
 
Katiba mpya watu walewale wenye mitazamo na nidhamu zao zilezile, chama kipya ambacho kitaweka mbele masilahi ya nchi kwanza kuliko ya chama..mmh
 
Hakuna cha katiba mpya , hii nchi ni kubwa mno zinatakiwa zitoke nchi kumi humu , mambo yataenda Sawa , bila hvyo hamna kitu, hata ukiiondoa CCM , utamweka Nani , ?? Wapinzani hawa hawa ambao hawaaminiki Kwa wananchi, labda waje wapinzan wengine , mbaya zaidi huwez tofautisha CCM na vyombo vya dola
Naunga mkono hoja,hiyo dawa ndio mujarabu kabisaaa!
 
Hakuna cha katiba mpya , hii nchi ni kubwa mno zinatakiwa zitoke nchi kumi humu , mambo yataenda Sawa , bila hvyo hamna kitu, hata ukiiondoa CCM , utamweka Nani , ?? Wapinzani hawa hawa ambao hawaaminiki Kwa wananchi, labda waje wapinzan wengine , mbaya zaidi huwez tofautisha CCM na vyombo vya dola
Ukubwa wa nchi unafuta vipi wizi na ufisadi, mwizi ni mwizi tu awe padogo ama awe pakubwa.
 
Wizi na utapeli na rushwa ni maisha mliojijengea wenyewe hamuwezi ubadili hata siku moja

Kuhusu ukisanyaji wa kodi kwa kubangaiza kwa walala hoi pia ni umasikini wa fikra na kutotaka kujiendeleza kielimu zaidi

Mnapeleka watoto shule za ads kubwa na utasikia ooh shule fulana imetoa wahitimu bora na ufaulu mzuri
Ufaulu huo ni wa kukariri tu

Angalia wenzetu wanasoma ili wafanye kitu au watengeneze kitu ila sisi hovyoooo

Shule zote ziwe za kutoa wanafunzi wenye uwezo wa kufanya kitu sio kuiba tu na kubebana

Mtu anatamba mtoto anasoma FEZA akimaliza shule anapachikwa mahali tofauti na alichokariri kwa mamilioni

Screenshot_20220928-094141_Chrome.jpg
 
Katiba mpya bila utashi bado hapatakuwa na jipya.
Nikweli kabisa.
Inahitajika nguvu kubwa sana kusimamia utawala bora.
Maana uchafu uliopo ni mwingi sana.

Ukitafuta waadilifu utapata mmoja katika 100.

Sheria ngumu za kikatili zisizo na huruma ndio zitanyoosha watu.
 
Ni nchi tu imekosa viongozi makini na wanaotanguliza taifa mbele.
Katiba hii iliyopo tu inatosha kunyoosha nchi ikawa kama rula, hili litafanikiwa tu kama kiongozi akiwa makini na akiweka kando maslahi yake na marafiki zake.

Ofisi ya TAKUKURU na DPP pamoja na mahakama zikiachwa zikawa huru kama Katiba na sheria nyingine zinavyotaka hii nchi inanyooka na kuwa kama rula.

Hizo ofisi mbili zikipata viongozi wasiocheka na kima katika utekelezaji wa majukumu yao, hakuna kiongozi atakayejaribu kucheza na mali ya Umma.

Rais kazi yake inakuwa ni kupokea taarifa ya CAG na kuzipatia hizo ofisi. Hizi ni ofisi muhimu sana katika kupambana na uozo mwingi.
 
Siku zote nimekuwa nikisisitiza tuende China tukajifunze namna ya kuendesha nchi na kufanya mapinduzi ya kiuchumi kwa miaka 30+, Au tuajiri wachina katika sekta kubwa za nchi kwa miaka 10 mpaka 20+ watujengee nchi kwa ushirikiano na wazawa .

: China imefika hapo ilipo kwa jasho na damu sisi tunataka tufike dunia aliyopo China kwa kazi na bata 😆 hiki ni kichekesho cha karne kabisa😆.
 
Shida inaanzia mbali, kiongozi anawekwa na kundi lake, kwa kutarajia kulambishana asali baada ya kushika hatamu.
 
Siku zote nimekuwa nikisisitiza tuende China tukajifunze namna ya kuendesha nchi na kufanya mapinduzi ya kiuchumi kwa miaka 30+, Au tuajiri wachina katika sekta kubwa za nchi kwa miaka 10 mpaka 20+ watujengee nchi kwa ushirikiano na wazawa .

: China imefika hapo ilipo kwa jasho na damu sisi tunataka tufike dunia aliyopo China kwa kazi na bata 😆 hiki ni kichekesho cha karne kabisa😆.
Inabidi kunyonga nyonga kidogo watu tena wazito ili adabu ikae mahala pake.
 
Kila Rais anaekuja madarakani kuna kakundi chake hawezi kukagusa, akikagusa naye anachafuka. (Tatizo hili)
 
Inabidi kunyonga nyonga kidogo watu tena wazito ili adabu ikae mahala pake.
Juzi tu hapa China kahukumiwa kunyongwa waziri mstaafu wa haki kwa kosa la kula rushwa, lakini kwetu mwizi wa kiserikali ana kuambia Billion ni pesa ya mboga halafu tunataka tufike waliopo hawa watoto wa Mao hakika bado tuna safari ndefu sana ya miaka 1000 ijayo kuamka kwenye huu usingizi wa ndoto za mchana.
 
Back
Top Bottom