Kinamama nyie mapenzi yenu hayana kifani wala mpinzani

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Nimejitahidi(mimi na ndugu zangu wa tumbo moja) kumfanyia mama yetu kila linalowezekana ili maisha yake ya utu uzima yawe ya furaha na yasio na changamoto nyingi za kimaisha kama ambavyo alikua nazo wakati anatulea na kutukuza wanawe

Kuna jambo moja tu linanistaajabisha kuhusu mama yangu na sina hakika kama nalifurahia au nakereka nalo au ni dalili ya hali gani ambayo siielewi vizuri wakuu ila linanishangaza sana siku zote

Kwa kadri ninavyojaribu kuzidisha mapenzi yangu kwa mama kwa kumfanyia jambo hili au lile, kubwa au dogo ili mradi tu aridhike na awe mwenye furaha na awe radhi na mimi najikuta kwa kila hali simfikii upendo wake kwangu!. Yeye kakaa tu katulia hana makuu hata kidogo, kwake ni shukrani na dua juu yetu wanae na tabasabu usoni mwake!

Natafakari naona pamoja na makeke na kujipendekeza kwangu(kwetu) ili nimfurahishe mama bado kaniacha mbaali sana kwa mapenzi ya kunipenda mwanae. Sina namna ya kuilezea hali hii ila nikajaribu kujiweka katika nafasi yake ndipo nikailewa kiasi hali hii

Nikajenga picha kwa mwanangu kwamba akija akikua halafu aje anifanyie mambo mazuri kiasi gani kwa kunipenda baba yake hawezi nishinda mimi mapenzi yangu kweke! Hii ni ajabu katika maajabu ya Mungu. Nijitahidi nimfanyie wema kupita wakwake juu yangu namkuta yupo mbele maili kadhaa mbele yangu na siwezi mfikia. Wamama wooote na wabarikiwe
 
Leo na mimi nimeshika na kuiwai nafasi ya mtu humu ndani [emoji23][emoji23]
 
Kiukweli hakuna ambacho tunaweza kumlipa na kikaweza kufunika yale yote waliyotufanyia.

Kikubwa tuwajali kwa kile tunachojaaliwa.
 
Last edited by a moderator:
Ukiona Mama hana shukrani, achana nae fanya yako.

Mimi sioni sababu ya kumshukuru mzazi yoyote kwakua hatukua na makubaliano ya yeye kunileta kwenye dunia hii iliyo jaa uovu.

Kwahiyo pale atakapo niletea longolongo nampotezea tu.

Kama unayafurahia maisha ya dunia na mzazi alikutendea mema, mpende sana, vinginevyoo mpotezee
 
Word!
 
Seriously mkuu!!!?😳🙄😵???
 
Back
Top Bottom