Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Hapo penye red,kama habari hii ni kweli,ni matokeo ya kulipa fadhila
kwa wasomi hao waliotuhadaa watanzania kwa tafiti zenye malengo
ya kuwabeba baadhi ya wagombea ili kufanikisha dhamira zao za kuja baada ya uchaguzi kulipwa fadhira.
kwa kuongwa vyeo na fedha za umma kwa kisingizio cha kufanya tafiti.

Na hapa ndipo wananchi tunatakiwa kuamka,kujikomboa wenyewe kwa
kufanya kitu kinaitwa ''trial and error'' bila kusubiri hao wanaojiita wasomi
huku wakishikishwa kitu kidogo wanaukana usomi wao na kuitukana taaluma yao
ilimradi mkono uende kinywani.

Hata mahospitalini uchunguzi ukishindikana wanafanya majaribio ya dawa
ni ipi inaweza kuua vimelea.Sasa watanzania tuamue kufanya yetu
pasipo kuwasikiliza wasomi ilimradi tusivunje sheria,Mpaka sasa
naamini kukiondoa chama tawala madarakani siyo uvunjifu wa sheria
Tufanye majaribio kwa vyama vingine walau kwa miaka hii mitano.
endapo nao wataharibu hatutakuwa na la kujuta kwani hata tukiweka
waliopo wanaendelea kuharibu.Hayo makosa yetu tutayarekebisha kwa uchaguzi ujao.

Shime vijana na wazee wanaojitambua,tuungane
tuutokomeze ukoloni maboleo,na kura yako ndo
silaha yenye kufanikisha hilo pasipokumwaga damu yoyote.
 
Mimi namkubali sana Magufuli. Lakini nimekuwa na wazo hili tangia zamani kuwa sehemu aliyopo sio sahihi. Hili la leo linajidhihirisha. Aidha, hana timu nzuri ya kampeni au mwenyewe amepanic. Kama una ilani ya chama na una kitengo cha sera na mipango cha chama basi hakuwa na haja ya kutangaza hii issue. Wanaonesha uzaifu. Kwa mfano tunafahamu ukawa wana washauri hawa wa kisera akiwemo wale madokta tuliowahi kuwasikia katika kipindi cha mikimikiki. Magufuli na timu yenu angalieni makosa ya namna hii na msifikri mtaonekana na mipango kabambe bali huu ni udhaifu
 
Kesho wanaenda kulikana hili tamko,watamtafuta dogo aliyetunga huu uzushi...jopo la kupambana na Lowasa&Sumaye,heeh heeh
 


Hii balaa zaidi ya gharika! Kwisha ccm imebaki porojo mtaani
 
hayo ni mawazo yake... Hivyo yeye anavyoamini. Si lazima kumbeza ktk hilo. Huo ni mtazamo wake...
 
#Hapakazitu. Tarehe 26/10/2015 alfajiri kabla ya Jogoo hajawika watu watasaga meno kwa kutoamini kilichotokea Tanzania!

Acha kusema takataka wewe,matokeo ya urais minimum mda wa kutangaza ni masaa 72.sasa wewe sijui utakua unashangilia matokeo yapi???
 
nakumbuka msemo wa babu zetu kwamba siku ya kufa nyani miti yote huteleza lakini pia msemo usemao mfa maji hakosi kutapatapa. mwaka huu CCM mtatapatapa sana. kulikoni leo Mkapa na kiwekwe aaze kampeni? halafu mbona havunji baraza la mawaziri? mwaka huu imekula kwenu nasikitika hata bilioni 32 mlizpanga kugawa kwa watu zilitoka CWT jitazameni sana maana mtatumia halafu hamtashinda mtadaiwa na chama. najua kwa chama cha walimu kinavyolalamikia madai ya walimu wasingeweza kuwapeni lazima mmeshinikiza sana na vitisho juu. Pole sana J makamba. na ufahamu tu kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuzuia mpango wa Mungu wa kuwapa Watz haki yao ya kufaid keki ya Taifa hili.
 

Ndio tatizo la kukariri. Haya yote yalisha ainishwa na Lowassa mapema ya asubuhi. Namna ya kupunguza matumizi ili kuboresha huduma. Kuondoa kodi za usumbufu nk.

Bahati mbaya sana huyo Makamba mwenyewe ndio wale wale wa-kuibia (Rejea Galanos). Wakati akiyataja hayo na kuyatafutia Consultants, Lowassa (UKAWA) ndio talk yake kila anapo panda jukwaani. Mambo haya yalishafanyiwa kazi na kuwa ya kisera zaidi.

Hii inatuonyesha kwamba, CCM haikuwa na sera ilipokuwa inaingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi. Kwamba, sera ni ya kichwa cha mtu na si jambo la kitaasisi. Leo hii unaunda jopo la watu wa kukushauri namna ya kuunda na kuondoza serikali!!!???
 

Kamwage damu ya familia yako
 
Huko ni kuweweseka. Hamna sera kila kitu mna pre empty sera za ukawa. I don't like you.
 
hahahaa

Kupata kituko hicho tuma neno HAPAGIZATU kwenda 15666

 
Tarehe ifike tu hiki kiwewe cha watawala kiishe. Lowassa oyeeee
 
Tupo tangu kale, CCM ile ile, wapinzani tupa kule...Maghufuli-#jembe-#jembe-,-#CCM-namba moja, naipenda mwenzio...
 
wamechoka sana hawa ccm aisee, eti unamsikia magufuli akisema nikiingia madarakani watendaji wa tanesco wanaokata umeme nawatupa nje. kwani serikali iloyopo sasa ni ya chama gani na yeye anagombea kwa chama kipi? eti riz1anasema safari hii sisiem imelamba dume akimaanisha uteuzi wa magofuli. maana yake anataka kutuambia uteuzi wa baba yake ccm ililamba jike? kama kina jk na mkapa watajiingiza kwenye kampeni cha kuzingatia ni hiki 1:wasitumie mali za serikali 2: watueleze pesa ya epa iko wapi 3:nani aliyeviua viwanda ambavyo magufuli anavilalamikia. kwa nini suala la umeme halijawa historia kama alivyokaririwa ji akijinadi. kwa nini jk hakutekeleza masharti 23 Kama alivyo agizwa na bunge ktk sakata la richmond. 6: mkapa yupo hiari kupelekwa mahakamani kwa mauaji ya wapemba? nk.
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…