Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Magufuli hawezi kuunda serikali imara ambayo ina watu waadilifu kwasababu hao mawaziri atakaowateua wanatokana na wabunge waliopata ubunge wao kwa njia ya rushwa na ndio hao hao wanaomshauri nani wa kuwa mawaziri; mfano mzuri ni huyo January Makamba ambaye rekodi yake toka shule ya sekondari na mpaka alipogombea ubunge mara ya kwanza ni ya kutokuwa na maadili ya kutukuka!! Akiwa sekondari aliiba mtihani na katika kugombea ubunge mara ya kwanza vielelzo viliwekwa mitandaoni kuonesha kwamba alikopa fedha kwa shemeji yake mzungu na kumuahidi kuwa angezirudisha baada ya yeye kuteuliwa kuwa waziri wa madini!!

Serikali itakayoteuliwa na UKAWA iwapo mgombea wao Lowassa atashinda itakuwa na mawaziri wenye uwezo na waadilifu kwa sababu watakuwa wameteuliwa kutokana na wananchi ambao sio wabunge !!! Kumbuka kuwa ukawa wameahidi kutupa katiba itakayotokana na mapendekezo ya wananchi kama ilivyotolewa na jaji Warioba. Kuunda baraza la mawaziri sio lazima lifanyike mara baada ya kuchaguliwa bali linaweza kuahirishwa huku serikali ikiendeshwa na makatibu wakuu. Kipengele cha kuwa na mawaziri wasio wabunge kinaweza kubadilishwa na bunge under emergency legislstion mpaka hapo katiba tuitakayo itakapopatikana!!

Wale wanaompakazia Lowassa kuwa ni fisadi hivyo ataunda serikali iliyosheheni marafiki zake wafanyabiashara wanakosea kwani wakumbuke kwamba Lowassa akifanikiwa kuwa Rais atathibitiwa na katiba ya wananchi ambayo ina checks na balances ambazo hazimpi nafasi ya kufanya mambo kama atakavyokuwa anataka!! Ukisoma rasimu ya katiba ya Warioba ambayo UKAWA wameahidi kuiptisha utakuta kuwa taasisi nyingi imara zitakuwepo kuimalisha utawala bora ikiwemo MAHAKAMA ambayo mkuu wake ataidhinishwa na bunge tofauti na sasa; taasisi za kupapambana na rushwa zitakuwa huru na sio chini ya Rais hivyo kuweza kuthibiti rushwa bila kuingiliwa; viongozi wa taasisi zote nyeti itabidi wachujwe na kuthibitiwa na bunge ambalo nalo pia wajumbe wake watakuwa na ukomo!!! Hivyo ukawa wana nafasi nzuri ya kutupatia serikali bora kuliko ccm ambao wao wanataka status quo [ ccm ni vile vile!!!] Naomba kutoa hoja.

Haya ni maoni yako tu Ndugu. Km Lowasa anajua cha kufanya angezungumza haya hsdharani kwa kinywa chake why is he afraid to talk about this?? Anaongea Juu Juu tu km anaongea na wasiojua siasa! Kufanya hivo watu tutarudi chadema tumpe kura zetu laa sivyo wewe huwezi kumzungumzia Lowasa yeye ndo aseme ili tunshtaki kwa maneno yake period!!! Wameshatu manipulate vyakutosha
 
Haya ni maoni yako tu Ndugu. Km Lowasa anajua cha kufanya angezungumza haya hsdharani kwa kinywa chake why is he afraid to talk about this?? Anaongea Juu Juu tu km anaongea na wasiojua siasa! Kufanya hivo watu tutarudi chadema tumpe kura zetu laa sivyo wewe huwezi kumzungumzia Lowasa yeye ndo aseme ili tunshtaki kwa maneno yake period!!! Wameshatu manipulate vyakutosha

Mnataka aseme mara ngapi kuwa akiingia madarakani atawapatia wananchi katiba waitakayo!! Nyie wengine mmepumbazwa na ahadi za magamba hamuoni wala hamsikii sababu ya kuushabikia Mwenge!!
 
Back
Top Bottom