brighton chuwa
Member
- Sep 12, 2015
- 31
- 7
Umoja ni Ushindi na viongozi hawa wanthibitisha msemo huu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwahiyo unatuambia ili iweje?? Peleka kwenye tovuti ya ccm
Ht mkiongeza namba ya mikutano,ht mkiandika uwongo,ht mkiongeza chumvi mpk na sukari lkn ccm haishindi mwaka huuu na rais ni lowasa ht viongoz wa juu wa ccm wanalijua hilo vzr sn
Yaani mnachunguza wakati mlisema matatizo ya watanzania mnayajuwa...!!!
Anyway baneni matumizi na ongezeni juhudi kwenye haya
1. Fungeni wote wa mishahara hewa
2. Halmashauri zenye hati chafu watieni ndani wote
3. Kamata wakwepa kodi wote
4. Futa misamaha ya kodi
Funny enough hata huku Chato Magufuli hakubaliki kama Lowassa
Acha mikwara hewa weweMnaona mnaidiwa mnaanza kumlilia refa, ninyi mmevunja sheria ngapi hadi sasa!! Na kwa taarifa yako tu ni kuwa nimestaafu siasa kabla hata hujajua maana ya siasa, au kwako pushapu ndiyo siasa safi na matusi kwa mgombea upinzani ndiyo siasa safi, mmewakamata wangapi kutoka majukwaa yenu wanaotukana hadharani?...katika niliyoyaandika onyesha matusi!! matusi yako wapi hapo? mnapewa ushauri ninyi mnatafsiri kuwa ni matusi kwa kuwa tu haupendi?Wewe unaona kuna busara katika jambo hilo? tusipokosoa unadhani nini kitafanyika? Mlianza kwa kutaka majina ya wote walioshindwa kwenye kura za maoni yaletwe ili muwatafutie kazi..kuna utimamu katika hilo?PakiJinja, nakushauri utafute kazi ya kufanya. naona unajifunza siasa ila hujuwi madhara yake. kama una chuki, uchungu vile hadi unatoa matusi. jihadhari mkono wa dola mrefu sana. chunga sana, tuko nyakati za majeruhi. bado siku 13. hutavumiliwa. matokeo yatakushangaza lakini itakuwa imetoka.
Tunapenda kuwataarifu wanachama wetu na umma wa Watanzania kuhusu masuala yafuatayo:
Mwenendo wa Kampeni za CCM
Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mgombea Mwenza, Ndugu Samia Hassan Suluhu, wameendelea kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini..
Hadi jana, tarehe 10.10.2015, Dkt. Magufuli alikuwa amekwishatembelea Mikoa 22 na Majimbo 203. Amekwishafanya mikutano mikubwa rasmi 240 na mikutano 865 ya kusimamishwa na wananchi njiani, hasa wananchi wa vijijini. Dkt. Magufuli amekuwa akitumia usafiri wa barabarani, ambapo hadi sasa ametembea kilomita 31,467 kwa barabara kuu, barabara za mikoa, barabara za wilaya, barabara za mlisho (feeder roads), na barabara za mijini na vijijini.
Watu wengi wamekuwa wanajitokeza kwenye mikutano yetu. Lakini la muhimu zaidi ni hamasa na matumaini wanayopata baada ya kumuona jukwaani na kumsikiliza Dkt. Magufuli. Wananchi wanapoondoka kwenye mikutano yetu ya kampeni wanakuwa wamepata fursa ya kumsikia mgombea wetu kwa kitambo kinachotosheleza, wamemuelewa, wameelewa sera za CCM na wameshawishika kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi.
Tunaingia katika ngwe ya mwisho ya kampeni zetu. Tangu kampeni zianze hadi sasa, ushindi wa CCM unajidhihirisha. Hata hivyo, katika kujihakikishia ushindi na kuongeza kiwango cha ushindi, katika ngwe hii ya mwisho, tumeanza kampeni nzito.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameanza ziara ya kampeni katika majimbo 64. Vilevile, viongozi wengine wa CCM, akiwemo Rais na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa, nao wataanza safari za kuzunguka nchi nzima kumuongezea kura Dkt. Magufuli na wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.
Tutatumia helikopta nne kwa ajili ya shughuli hii. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wataendelea kutumia usafiri wa gari hadi mwisho wa kampeni, isipokuwa pale tu itakapokuwa hakuna budi.
Maandalizi ya Kuleta Mabadiliko ya Haraka na ya Kweli
Pia, tunapenda kutoa taarifa kwamba, mgombea wetu, Dkt. John Pombe Magufuli, ameunda jopo la wanataaluma na wataalamu huru magwiji wazalendo wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini kuanzia siku ya kwanza atakayokuwa madarakani.
Dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:
1. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;
2. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;
3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali;
4. Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa.
5. Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania;
6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.
7. Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.
8. Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.
9. Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;
10. Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.
Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.
Imetolewa na:-
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni
Acha mikwara hewa weweMnaona mnaidiwa mnaanza kumlilia refa, ninyi mmevunja sheria ngapi hadi sasa!! Na kwa taarifa yako tu ni kuwa nimestaafu siasa kabla hata hujajua maana ya siasa, au kwako pushapu ndiyo siasa safi na matusi kwa mgombea upinzani ndiyo siasa safi, mmewakamata wangapi kutoka majukwaa yenu wanaotukana hadharani?...katika niliyoyaandika onyesha matusi!! matusi yako wapi hapo? mnapewa ushauri ninyi mnatafsiri kuwa ni matusi kwa kuwa tu haupendi?Wewe unaona kuna busara katika jambo hilo? tusipokosoa unadhani nini kitafanyika? Mlianza kwa kutaka majina ya wote walioshindwa kwenye kura za maoni yaletwe ili muwatafutie kazi..kuna utimamu katika hilo?
Ni ninu kitakachofuata hapo kipindi hiki cha kampeni kama hatutasimama kama hivi na kupaza sauti? si mtatuundia baraza la mawaziri, mtatutelia IGP, mtatuteulia mkuu wa majeshi n.k? Elewni tu kuwa mnachoanza kufanya ni vurugu na hatutawaacha muivuruge nchi in the name of campaign. Au mnadhani sheria mnazijua ninyi tu?
Endeleni kuota; mkizinduka Magufuli atakuwa kashaapishwa tayari