Kinana alikuwa sahihi, hawa askari wa barabarani ni majipu!

Kinana alikuwa sahihi, hawa askari wa barabarani ni majipu!

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,022
Reaction score
3,919
Nazidi kusema hii nchi ni ngumu sana. Kila mtu alieshika sehemu anajifanya kuwa na mamlaka bila kujali sheria imekaaje.

Hii kitu imetokea hapa Bugurun sheli gari za Kawe-Buza. Gari imesimamishwa ghafla na askari, dereva anaambiwa peleka gari kituoni, dereva kagoma kauliza kosa langu ni nini mbona siambiwi na hapa nina abiria?

Polisi wanapigiana simu kutoka sheli kuja tulipo wakawa kama watatu wanataka dereva ashuke,bahati mbaya au nzuri dereva ni mchaga hataki kushuka mpaka aambiwe kosa lake ni nini.

Na polisi hawataki kusema kosa la dereva basi tafrani hapa gari imepaki pembeni.Nikakumbuka katibu mwenezi alisema hawa maaskar wapungue barabari kumbe alikuwa kweli aiseee. Sasa hapa nawaza nauli yangu ndio hii hii nikisema nishuke nipande gari nyingine ntaenda kulipa nini huko, si ndio kupata aibu mjini huku, ngoja nione tunaishia wapi na mwanagu dereva wa Marangu huyu hatoi hata mia.
 
Ukiona hivyo basi ujue huyo dereva hajatoa/amegoma kutoa marejesho yake ya siku. Hakuna kingine.

Hao jamaa hata kama gari imetoka yard, bado wataitafutia makosa mpaka mwisho wa siku wakutoe upepo.
 
Yaani binadamu unaishi kwa hela za dhulma. Eti una mke umeoa kwa hela za rushwa. Umejenga kwa hela za madereva. Unawalipia Ada wanao kwa hela za wizi. Una biashara kwa hela za lazima. Da! kweli kuna watu wana roho mbaya na ngumu.
 
Back
Top Bottom