Pre GE2025 Kinana anakiri hadharani kuwa yaliyotokea 2019 na 2020 hayatajirudia. Atuambie pia uhalali wa chaguzi zile

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2023
Posts
1,483
Reaction score
2,392
Ni aibu kubwa kwa chama kinachojisifia kuwa kinapendwa na wananchi na kupigiwa kura za ushindi katika chaguzi. Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mzee Kinana, amekuwa akiwaambia wananchi kuwa uchaguzi ujao utakuwa huru na haki na hakitajirudia kile kilichojitokeza katika uchaguzi wa 2019 na 2020.

Kauli hiyo amekuwa akiirudia mara kwa mara lakini hataki kuifafanua. Kama kweli Mzee Kinana anakiri kuwa kilichotokea hakitajirudia, ni wazi kuwa kilikuwa sio halali, hivyo tunamtaka Mzee Kinana akifafanue kilichotokea na akiri hadharani kuwa ule uchaguzi haukuwa halali kwa kile kilichotokea na CCM iwaombe radhi wananchi kwa tukio lile, kwani ni aibu kwa taifa kuwahadaa wananchi wake na kuwakosesha viongozi waliowachagua ili wawaletee maendeleo.

CCM ni kansa ya koo.

====

Pia soma: Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?
 
Msiwaamini CCM, msiwaamini katu. Kama waliahidi kwenye maridhiano kuwa kutakuwa na katiba mpya , etc etc badaye wakageuka, msiwaamini. Tafuteni mbinu za kulinda kura na kila kitu
 
Nili mheshimu sana Kinana ila amezsska na hoja zake ni za kitoto. Ccm mpumzizhini aka lee wajukuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…