Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Leo nimejikuta nacheka sanaaa.. Mwenyekiti wa Kampeni ya Urais ya Kikwete Bw. Kinana akihojiwa mapema leo asubuhi na ITV amevisihi vyama vingine visiwaeleze sana mambo mabaya na yenye kubebesha lawama serikali ya Kikwete kwani kwa kufanya hivyo wanawachanganya wananchi. "Tuna matatizo mengi ya afya, elimu, maji, miundombinu hivyo tuzungumzie sera zaidi tutafanya nini" amesema Kinana.
Je vyama vingine vitamsikiliza na kuacha kuzungumzia mambo ya kashfa au ubovu na kuanza kueneza sera tu? Je kuna umuhimu wa kuwajulisha wananchi mambo yaliyokwenda kombo miaka mitano iliyopita?
Je vyama vingine vitamsikiliza na kuacha kuzungumzia mambo ya kashfa au ubovu na kuanza kueneza sera tu? Je kuna umuhimu wa kuwajulisha wananchi mambo yaliyokwenda kombo miaka mitano iliyopita?