Elections 2010 Kinana: Chadema ni chama cha kibepari na kimwinyi

Elections 2010 Kinana: Chadema ni chama cha kibepari na kimwinyi

Kuna kitu kimoja tu simple Kinana anashindwa kujua, au labda anajua lakini anajishaua tu. Kwa nini kampeni za mwaka huu ni ngumu sana kuliko za 2005? What went wrong Kinana? As a campaign manager, labda mgombea wako hauziki, au umeshindwa kubuni strategy nzuri za kumnadi mgombea wako. Hizi attack za kijinga kwa Chadema haziwezi kumbadilisha mbeba moramu wa pale Mbokomu ambaye ameshakata shauri kumpigia kura Dr Slaa kubadili kura yake na kumpigia mgombea wako. Kama JK angelikuwa amefanya mema mnayotetea kipindi chake cha 2005-2010, nadhani Kinana ungekuwa unaburudika na trupa kule Arusha wala usingekuwa na shida inayokupata sasa ya kujibu kila dongo linaloelekezwa kwako kwa majibu hafifu na ya kizandiki. As a matter of fact kutouzika kwa JK kumekufanya uende out of your comfort zone kutetea uchafu, and you know what, jamii inakuona kama kichekesho na umezidi kuchukiwa!!

Umekosea kuhusu suala la Dr Slaa kuwa kwenye kamati ya kuboresha maslahi ya wabunge. Kasome Hansard-- well Sita alikataa isiingizwe kwenye hansard za bunge (ubabe) pale alipomfokea Slaa na kumuamuru akae chini siku Dr Slaa alipolalamika kuhusu mishahara mikubwa ya wabunge--sijui Kinana ulikuwa wapi-- au ndio ulikuwa unasindikiza yale makontena yako yenye nyara za serekali?

Mshahara ni haki ya mtu, hata kama hukubaliani nao, na Dr Slaa ana haki ya kuchukua ujira huo hata kama hakubaliani nao. Na kuwapa NGO mshahara usiokubaliana nao sio njia muafaka kuonyesha kutokubaliana kwako, bali huo ni ujinga. Ina maana NGO's ndio za kupokea dhuluma, hebu zitake NGO radhi tafadhali.

Kwani wafanyakazi wanaodai kima cha chini ni kidogo, mbona wanachukua hicho wanacholipwa na hawasusi? Na wanazidi kudai haki yao?Kususa sio njia ya kutatua tatizo, kusema ukweli ndio njia sahihi hata kama unashiriki jambo lenyewe. Kukataa kuchukua mshara ni utovu wa nidhamu na sidhani kama ni kitendo cha kiungwana. Ni sawa na kuwaambia waliongeliwa kwenye kura za maoni ya ccm wasuse kuikampenia ccm,. Dawa ni kubabana huko CCM hadi mnapozidiwa mnawaangukia kama mlivyomuangukia Mwakalebela na Bashe. Bado mmesahau kumuangukia Mzee Malecela

Mbona hukujibu kuhusu Sita kujenga ofisi ya spika wa bunge au ofisi ya bunge huko Urambo-- Kinana, please umesoma Havard, act as an elite, lol, yaani fedha zinakufanya unakosa utu wako na kuwa mjinga kuliko hata hao unaowanadi, oh Tanzania,
 
Since walipoenda kula CHAZA kule zenji hawakuanza kupractice ambacho waasisi wa CHADEMA walikiamini kabla ya vyama vingi?

CCM ndiyo GHILIBA nambari wani kwani wana katiba inayosema na kutetea misingi ya ujamaa na kujitegemea lakini wanakumbatia na kutekeleza sera za kibepari tena ubepari mamboleo
 
Kinana alishafilisika sera kichwani siku nyingi sana, anachokifanya sasa ni kutetea maslahi binafsi ya biashara zake za kiharamia
 
Chama cha Kibepari ni kile kinachotumia mabango makubwa ya biashara katika kampeni. Ni kile kinachotumia mabailioni kwenye kampeni wakati wanafunzi wanakaa chini. Ni kile ambacho serikali yake inatumia magari ya milioni 200 wakati wazazi wanalala mzungu wa pili na nne kwenye wodi zao. Hivi katika dunia ya leo kuna ujamaa kweli?


Havard nini bwana CCM hata ukiwa na degree ya mbinguni bado haitatumika. CCM kuna maprofesor wangapi? wanatusaidia nini? Wameacha kazi za professional ambazo nchi hii imewasomesha iliwaitumikie wamekimbilia politikis na kwenda kuwa chini ya Bosi KIRAZA kama kikwete wakimshika miguu ili wapewe uwaziri,ukuu wa mkoa wilaya n.k. Kinana anatufanya sisi mabwege tuendelee kufikiria ujamaa huku wao wakitesa kibepari kwa jasho la walalahoi! Mwambieni siku zao zimehasabika na zimepungua mno! kama wao watapenya na kuondoka kabla ya siku hiyo kufika, watoto wao wataonja joto ya jiwe. Watoto wetu na uzee wetu tutatesa kama Lazaro huku wao na watoto wao wakiomba japo maji ya kunywa. Wamelianzisha wenyewe nilazima malipo hapahapa duniani haitasubiri YESU arudi! Wanganga wa kienyeji ndo wanachezea ikulu eti kumlinda Raisi...... Hasira ya Mungu haiko mbali nilazima kitokee kitu si Muda mrefu! We well Keep on praying until GOD answers! Tumeonewa vyakutosha, tumedhulumiwa vya kutosha sasa
Mungu inusuru Tanzania na uongozi wa kishetani kama huu! basi
 
KInana bado anatsewa na ukweli wa utafiti wao na vyombo vya serikali na kuona kwamna Slaa is ahead for 45% na Kikwete is 41%
Hawajajua how to change it hata sasa na siku zinaisha . Wakichelewa sana wakienda kwenye ramli tena itakuwa more .
 
Back
Top Bottom