Tetesi: Kinana hajapenda kuendelea na kazi ila hana namna

Tetesi: Kinana hajapenda kuendelea na kazi ila hana namna

Bavicha bwana kwa hiyo mnaamini kuwa Magufuli hakuwasiliana kabla Na Kinana kuhusu kuendelea Na majukumu yake.?

Mnaamini Kinana Na CCM nzima walikuwa hawajui Magufuli atafanya maamuzi gani kuhusu sekretari nzima ya CCM.?

CCM wanajua siasa za ndani Na siasa za majukwaani......ndio maana swala la Magufuli kuwa alikataa hiyo nafasi amelazimishwa hiyo ilikuwa chenga ya mwili kwa wazandiki Na wasio jua siasa za CCM.
 
Kutoka katika viunga vya mkutano wa CCM kukabidhiwa chama kwa Rais Pombe,
Wadau wa CCM wanaomfahamu Kinana wameweka wazi kuwa Kinana kalazimishwa kufanya kazi za ukatibu mkuu pasi ridhaa yake.

"Tunaomjua Kinana amechukizwa kwanza kwa kusomwa barua yake ya kujiuzulu hadharani na kujibiwa kuwa aendelee na kazi ya ukatibu hili hali ameshaamua kuendelea na shuhuli zake nyingine" alisikika kada mashuhuri wa CCM akisema hayo.

"Kitendo cha kumjibu Kinana barua yake jukwaani ilikua ni kumuaibisha kwani asingeweza kupata nafasi ya kumuambia rais kuwa hawezi tena kuendelea na kazi hiyo na tunao mjua Kinana alichukizwa na maamuzi yale "alinena maneno hayo mama maarufu na kada wa chama aliyekuwepo jukwaa kuu.

My take:

Ni dhahiri mwenyekiti mpya wa CCM alijua sehemu pekee ya kumbana Kinana asifurukute ni kuijibu barua ile jukwaani.


Kwa Nini unamnenea mtu ambacho yeye hajasema? Hii inaonyesha uhodari wako wa kutunga uongo.
 
Upinzani umebakia kujadili na kuibukia matukio tu siku hizi. Kwa mtindo huu tusahau kuiondoa CCM madarakani!!! Watu wa calibre ya Dr Slaa wako wapi ili kuupa uhai upinzani ??!!
 
Hawa CCM nao wasituletee sanaa yao ya 'demokrasia'.

Tuliambiwa ati hata JPM nae hakuutaka uenyekiti! Na sasa manasema na Kinana nae hakutaka! Maana yake nini? Kwa hiyo CCM kwa sasa inaongozwa na watu waliolazimishwa kuongoza? Hii maana yake ni nini kwa mustakabali wa nchi yetu? Hasa kwa kuzingatia kuwa CCM ndio chama kinachounda serikali kwa sasa?
 
angejidai kukataa jamaa angekumbushia habar za mali asili ya wale tembo wa tanapa.
 
Hili mbona lilikua wazi tangia jana. Sura yake ilikua inaonyesha wazi kwamba hakutaka kuendelea.
 
Kwa hiyo kada maarufu ndio msemaji wa hisia za kinana, hapa hauhitaji elimu ya veta kujua kuwa aliyeandika kanywa kiroba cha mwendokasi
 
Back
Top Bottom