Kinana kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa?

Kinana kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa?

Makumbele

Member
Joined
May 9, 2009
Posts
77
Reaction score
431
Wakuu,

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa ni nafasi kubwa ndani ya chama hicho na kimsingi ndiye mchora ramani ya mwelekeo wa chama hicho.

Mzee Mangula (Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa wa sasa) yupo katika siku zake za mwisho katika nafasi hiyo.

Kumekuwa na utamaduni ndani ya CCM kwa sehemu kubwa Makamu Mwenyekiti wa chama mara nyingi anatokana na Makatibu wakuu wastaafu.

Mfano Mzee Kawawa, alikuwa Katibu Mkuu then akaja kuwa Makamu Mwenyekiti, Msekwa alikuwa Katibu Mkuu, akaja kuwa Makamu Mwenyekiti, Mzee Mangula alikuwa Katibu Mkuu, akaja kuwa Makamu Mwenyekiti.

Mzee Kinana alikuwa Katibu Mkuu, si ajabu atakuwa next Makamu Mwenyekiti baada ya Mangula.

Je, CCM ikiwa mikononi mwa mzee Kinana itaweza kutaradadi tena? Nini tutarajie kitabadilika?

NOTE: Wapinzani walishamsafisha Kinana na “tuhuma za Ujangili” > Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba radhi
 
Tuwe na subira huku tukijua kuwa Tanzania iko imara.

Rais Samia Suluhu Hassan ni rais makini na mwerevu. Tena jasiri na aliyepikwa na kuiva katika kuliongoza taifa hili

Lala salama kipenzi chetu Rais John Pombe Magufuli 💔🙏
 
Huyu ile kamati ya Bashiru ya kuchunguza Mali ilisema kaiba mali za chama. Sasa anarudi tena. Hatari hii, Bashiru arudi tu akafundishe maana Kinana akirudi ni balaa tupu.
 
Kinana, hakuna, hapana, noooooo! Hata kama wote wanachama wote wamekwisha, bado kinana hapaswi hata kufikiliwa! Jamani tembo wetu walikuwa wanaishi kwa amani sana na kuzaana, mnataka kuwaambia nini tena pamoja na twiga wetu jamani!
 
Back
Top Bottom